kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,833
- 23,276
Hili walilofanya gazeti la mwananchi lilikuwa ni kusudio kuu la kujaribu kuzidi kumtukana Raisi Samia kupitia mtangulizi wake marehemu Magufuli.
Kama walivyosema familia kila anayemdhihaki marehemu Magufuli wao hawatamjibu watamuachia Mungu ajibu dhihaka zao,
Nina hakika kuna kigogo alitumia kwa makusudi gazeti la mwananchi kuanzisha upuuzi wa kupiga kura kuwalinganisha Raisi Samia na watangulizi wake.
Lakini lengo kuu ikiwa ni Magufuli,leo ghafla Mwananchi wanaomba radhi eti njia zilizotumiwa kumpata mshindi sio sahihi.
Je, hilo lishindano lilipoanza hamkuona njia mlizotumia?
Waziri wa habari ni mmojawapo mwenye makando kando na marehemu akishirikiana na ndugu yake wa yamini ila Mwenyezi Mungu anawamumbua na hawatashinda kwa lolote lile walilodhamiria juu ya marehemu, kwa kuwa hawezi kujibu matusi yao na kejeli.
Ushauri Raisi Samia watu wakisema ukweli mnawaita kamati ya maadili kuwatisha hao wasaidizi wako wawili wana mpango wa siri kukuhujumu, hata hizi kura wao ndio walitoa wazo kupima upepo, ila wamevutwa na kupeperushwa na kuogofywa na walichokiona .
Hivyo jitahidi kusafisha nyumba kabla ya uchaguzi vijana wanakuhujumu yaani wewe ni wa kushindanishwa na marehemu na ukashindwa ,haijapata kutokea labda ni zile kura za twitter kufananishwa mtu na andazi likashinda andazi.
Fukuza usiogope majina ya familia zao, Mkiambiwa ukweli mnapeleka watu kamati za maadili mbona wao wanasema mengi ya kichochezi hatujasikia kupelekwa kamati ya maadili.
Kiuhalisia usiposafisha hao watu uchaguzi utakuwa na kazi ngumu utakuwa ndie raisi wa kwanza kushindwa uchaguzi kwa kukumbatia watu wanaokung'ong'a!
Kumbuka kama waliweza kupigiana simu wakaweza kumsengenya Raisi wa nchi akiwa Mwenyekiti wao wa chama vipi leo hii wewe hawawezi kulifanya hilo?
Mama akili kichwani mwako!