Raisi Magufuli likatae pendekezo la kuwashughulikia mitume na lile la kujenga makanisa mpaka kwenye vituo vya usafiri wa Mwendokasi.

Kwani unateseka?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu Kwanza nikupongeze kwa kuonesha uwezo wako mkubwa wa kufikiri,umeongea vyema Sana na ukweli usiopingika katika sehemu kubwa ya maelezo yako ispokuwa Kuna sehemu chache ni vyema tukawekana sawa.

Sehemu Kama kwamba Mtume Muhammad hakutajwa kwenye biblia nikufahamishe tu kidogo kwamba Muhammad Ametajwa kwenye biblia..sema kwenye biblia Kuna namna mbili za kusoma Aya..Kuna Aya ambazo rahisi kuzifasili au kwa maana nyingine zinajifasili zenyewe na Kuna Aya ambazo ni ngumu kuzifasili lazma mtu fulani ambaye amejawa na roho wa Mungu akufasilie,hivyo nikueleze tu Muhammad yupo kwenye biblia sema wewe ndiye amabye umeshindwa kumuona ndani ya biblia.

Jambo jengine Muhammad ndiye mwisho wa manabii na mwisho wa mitume ni kweli kabisa amefunga milango ya manabii wapya Bali hakufunga milango ya manabii ambao hawakufa kurudi, Mfano halisi tulio wengi Kati ya waislamu na wakristu tunafahamu kwamba nabii issa anarudi na tunamsubiri je Kama Muhammad ni Mwisho wa manabii tunatafsiri vipi hapo?
Au kitabu Cha kiislam kinaitwa albidaya wannihaya kimetabiri ujio mwingine kabisa wa nabii ilyasa/elia kurudi na kuja kwake ni kuja kubainisha fitina za mpinga christu kabla ya kurudi kwa yesu nayo tunaitafsiri vipi?
Ni kweli kabisa waislamu wengi hawajamuelewa Hamza Bali wanakurupuka na jazba zao ambazo mi naziita za kipumbavu kabisa,hawataki kukaa chini na kuelekezwa kwa kutulia Bali utakuta asilimia kubwa ni wabishi Sana na wanajua kila kitu Yani wanaviburi ambavyo vitawaponza.

Bali pia nimesikia huyo mzee wa bakwata akisema kwamba Kama ni utume angestahili kupewa Mufti zuberi huo ni upuuzi kabisa ambao nimeshangazwa nao,Yani watu wamejiweka position kubwa Sana hata za kutaka kumshauri Mungu Cha kufanya kasahau kwamba Mwenyezi Mungu humpa cheo amtakaye!!

Otherwise nikushukuru Umejitahidi Sana na umeongea vizuri Sana na nakupa pongezi kubwa Sana kwa udadavuaji wako,ni watu wachache Sana wenye fikra Kama zako.
Nakupenda Sana ndugu yangu.
 

mbona mabaa ya pombe yanajengwa kila sehemu husemi; unatoa hoja ndeefu haina maana mgalatia wewe


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ila una kumbuka ya nabii Tito, Wakristo, walichukia kufanya yale anayoyafanya, kwa nukuu za Bibilia kitu kilichoonwa na Wakristo, ni upotoshaji, kwa kuwa aliyokua akiyafanya hayaendani na Bibilia ambayo yeye alikua akiyanukuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vema sana mkuu!
Viongozi wengine wa dini hawajitambui kabisa.
Kuhusu mtume Muhamad, huyu utume wake hakutumwa na Mungu bali Mungu alikuwa ni shahidi wakati Muhamad anatumwa [soma Q'uran 4:79]. Alitumwa na nani? Sijui!
 
Binafsi naomba kumtetea gwajima kwa namna nilivyomuelewa alipotoa ombi lake...

kwanza kabisa kwa uelewa wangu ni kuwa kuna dhana ambayo waumini wa dini ya kiislamu wanayo kuwa dini yao ndio dini pekee ya haki, hivyo ni watu wenye ajenda za kuhitaji kuangaliwa kipekee na pengine tamaduni zao tu ndio watanzania wote tuziishi, utakumbuka waliwahi kuhitaji mahakama za kadhi zitambulike kikatiba, na wengine hata hutamani nchi iongozwe na sharia..utakumbuka hoja za kuchinja... sasa wanakwenda kwenye misikiti..

ubaya wa mambo haya ukiyaangalaia kwa miktadha wa kitaifa hayana tija bali kutugawa na kuleta mitafaruku tu, kwani kwa hoja za msingi kabisa wakikataliwa mahitaji yao haya huishia kulaumu na kusema wanaonewa...

kwa nini namtetea gwajima?

tena na maaskofu wengine wa kikristo walipaswa kufanya kama alivyofanya ili kuwaonyesha waislamu kuwa watanzania wote wana haki hivyo waislamu wasipende kutendewa kwa upekee peke yao.

kama ulimsikiliza vizuri gwajima alijaribu kusema kuwa kutokana na ombi hilo na wakristo pia wakiomba maana yake pale airport patakuwa ni fujo za ibada tu... na maana yake ni kwamba mzee baba bora apuuze tu hilo ombi

kimsingi alitumia njia ya kidplomasia ku counter hilo jambo maana duh...haya mambo haya ni chenga chenga tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi nimemuelewa hivyo wala hakuna mkristo anaetaka uwanja wa ndege pawe na kanisa, ila hapo kaonesha kuwa wote tuna haki hivyo maana yake hata mabudha na dini nyingine zote nao wataomba, sasa Rais aangalie kama anao uwezo wa kuruhusu jambo hilo au la.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Serikali ikicheka cheka ofisi zote za uma zitajengwa misikiti na nyumba nyinginezo za ibada
 
Ni kwani sababu tumegeuza Falsafa ya dini kuwa mashindano au Mbio za Marathoni. Wengine wanafikiria Makanisa mengine yamekuwa kutokana na kubebwa.

Exactly Mkuu dini sasa imekua ni mashindano tupu

Na hata hao wanaotaka wapewe nafasi (vyumba au viwanja kabisa) vya kufanyia shughuli zao za kiimani, ukiwatafakari kwa makini utagundua msukumo wa madai hayo ni mashindano tu-hakuna kuabudi kwa dhati

Ndugu zetu hao huamini kwamba kujenga nyumba yao ya ibada/au kutengewa sehemu ya kuswali kwenye maeneo ya uma ni sifa na ukubwa 'ukuu'

Wanaamini uwepo wa nyumba hizo utadhihirisha ukuu wa dini yako katika nchii au dhidi ya serikali (rejea madai yao dhidi ya the so called mfumo kristo)

Full stop! again.
 

Muda wote wanatafuta kuonekana dini yao inaenea kila sehemu. Kwao cha umuhimu ni wingi na sio ubora.
 
Nakuunga mkono hoja yako Mr .@SANCTUS ANACLETUS

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gwajima hajaomba yajengwe makanisa,...alichosema ni kuwa na Wakristo nao wanaabudu sio J2 tu,akijibu hoja kwamba kama patajengwa msikiti basi na Wakristo nao watahitaji kufikiliwa na ndio maana alitumia kauli"KUWEKA RECORD SAWA".....maana yake kama hawa watahitaji msikiti na hawa watahitaji kanisa.....kuna watu hawajafurahi kuona viongozi wa DINI hajasema vile wanavyotaka wao,..ni jambo la ajabu sana na huo sio uhuru wa mawazo,sio kwamba unachowaza wewe na mwingine anawaza hivyo,tuishi kwa kuheshimu wazo la mwingine hata kama wewe hupendi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…