Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Moja ya mifupa ambayo imeishinda CCM kuitafuna ni kumteua mwanamke kuwa Waziri Mkuu. Mfupa huo kaka yetu Dr. Slaa ambaye tunatarajia kumvika joho la Urais wetu hivi karibuni nimepata tetesi ameamua kuhakikisha anautafuna huo mfupa kwa kumteua mwanamke wa kwanza katika historia yetu ya nchi yetu kuwa Waziri Mkuu.
Kwenye hili, CCM wao wamekuwa magwiji wa ngebe na porojo tu na hakuna utekelezaji wa vitendo. Sasa mchapakazi Dr. Slaa atakapotinga Ikulu atafuta hii aibu kwenye taifa letu la kutokuwa na mwanamke kwenye ngazi za juu za uongozi wa taifa hili.
Mimi ninapendekeza ayafikirie majina haya matatu kwa sababu nitakazozitaja hapo baadaye kidogo:-
1) Prof. Anna Tibaijuka........................CCM
2) Ms. Anna Makinda............................CCM
3) Dr. Asha Rose Migiro........................CCM
Sababu zangu za kuwapendekeza akina mama hawa kutoka CCM ni:-
Kwanza, kupunguza misuguano iliyojionyesha kwenye chaguzi hii kati ya CCM na Chadema,
Pili, ni matarajio yangu kuwa CCM bado itakuwa na wabunge wengi zaidi Bungeni na hivyo kutowashirikisha kabisa italeta ugumu katika kupitisha miswada ya serikali bungeni,
Tatu, ni mahitaji ya kikatiba ya kuwa kwa vile kama matarajio yangu yatakwenda saawia basi CCM ndiyo itakayoongoza kwa wabunge wengi Bungeni na hivyo ni haki yao kutoa Waziri Mkuu na kuteua mwanamke kuwa Waziri Mkuu kutoka CCM Dr. Slaa atakuwa kawafunga CCM bao la kisigino kabisa.......chuki zitoke wapi baada ya kuwaenzi hivyo?
Nne, akina mama ni viongozi wazuri na huona mbali sana na kwenye kipindi hiki cha mpito kutoka utawala wa kiimla kwenda kwenye utawala wa kidemokrasia busara zao tutazihitaji sana. Wanawake wana subira na ni wa vumilivu na wengi wao siyo waroho wa madaraka au kujiingiza kwenye aibu za kusaka mali na mara nyingi wapo tayari kujinyima ili kulinda uhai wa jamii.
Hatutagemea kati ya hawa niliowapendekeza kuhusishwa na tuhuma za wizi na ubadhirifu wa mali ya umma kama baadhi ya wanaume ilivyowatokea siku za karibuni...
Ni vyema nanyi wanajamvi mkatumia nafasi hii kuiangalia nafasi hii ya uwaziri Mkuu imwangukie nani yule.....sote tunajua hakuna kama mama.........au vipi?........