Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Raisi wa Urusi Vladimir Putin jioni ya jana ametoa salamu za pole kwa familia ya Yevgevy Prigozhin ambae alifariki katika ajali ya ndege ndogo binafsi akiwa na abiria wengine 9.
Raisi Putin amesema alimfahamu Prigozhin kwa tangu miaka ya 90 na kwamba kiongozi huyo wa Kundi la askari wa kukodi la Wagner alikuwa ni mtu mwenye historia yenye utata.
Putin aliendelea kumuelezea Prigozhin kwamba ni mfanyabiashara mwenye kipaji ambae alipata mafanikio binafsi na kwamba alikuwa na maslahi barani Afrika.
Raisi huyo wa Urusi akasema kwamba ni kutokana na mafanikio hayo ya Prigozhin akamuomab asaidie harakati za kuipigania Urusi na kwamba jana Prigozhin alikuwa Moscow kuzungumza baadhi ya watu kabla ya tukio hilo la kuanguka kwa ndege.
Hata hivyo Putin amesema Prigozhin amefanya makosa makubwa maishani mwake.
Na huo ukawa mwisho wa mahojiano ya Raisi Putin.
Msikilize Raisi Vladimir Putin.