Kibongo bongo hata media yenyewe ingepigwa X wengine wakafuta.Katika hali ya kushangaza,
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta ametumia sikukuu za Christmas na Mwaka mpya kumtakia heri ya sikukuu hizo mbunge wa upinzani Millie Odhiambo ambaye mapema mwezi huu alimtukana kwa njia ya video kupitia Runinga na baadae mitandao ya kijamii....
Kitendo hicho Kiliwashangaza waKenya wengi waliodhani kuwa huenda Mbunge huyo angeshtakiwa kwa kitendo hicho ila Raisi huyo alidai Ukiwa baba wa familia lazima ukomae Kichwa na uwe mvumilivu kwani kila mtoto ana Tabia yake.
Naomba mnichagulie gereza la kumfunga huyo ikitokea Tz. ...
True. ..unafahamu ukichukulia kila kitu simple hakuna litakalo kusumbua ila ukijifanya wewe hukosolew au kukutana na dhihaka hutoenda mbele. ..Na Uhuru alivyoichukulia ile issue kishkaji itakuwa haina effect yoyote ndani ya miez kadhaa watu wameshaisahau
Ila visasi vya bwana mkubwa hadi anaingia kaburini watu hawatamsahau.
Na asiombe 2020 washindwe kuchakachua kura.
" Raisi huyo alidai Ukiwa baba wa familia lazima ukomae Kichwa na uwe mvumilivu kwani kila mtoto ana Tabia yake."
Hayo ni maneno ya kuonyesha ukomavu wa kisiasa, nafikiri mzee Kenyatta alipatia kumpa jina la UHURU na kwa kweli amelitendea haki jina lake