Rajab Athmani Matimbwa muasisi wa kwaya ya TANU 1954

Rajab Athmani Matimbwa muasisi wa kwaya ya TANU 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
DSCN1014.JPG

Rajab Athmani Matimbwa
Rajab Matimbwa katoka Chole, Uzaramo kaja Dar es Salaam kijana mdogo kutafuta maisha.

Rajab, Bi. Titi ni shangazi yake na akikaa nyumbani kwake Shauri Moyo.

Harakati za kudai uhuru zilipoanza Dar es es Salaam Rajab akajikuta ana kibarua cha kuuza maji kwenye bomba moja lililokuwa linatazamana na ofisi ya TANU New Street (Sasa Lumumba Avenue).

Kabla ya kufanya kazi ya kuuza maji tayari Rajab alishapewa kibarua na John Rupia cha kuuza mgahawa pembeni ya Pugu Road na ikatokea akaelewana vizuri sana na Mzee Rupia na familia yake yote akawa mtoto wa nyumbani.

Rajab anawakumbuka watoto wa Mzee Rupia, Paul na dada yake Kipanya, Mpuya (Stephen) na kaka yao mkubwa Albano.

Mzee Rupia alikuwa na lori lake limeandikwa, ''Msichoke,'' likibeba mijengo.

Mikutano ya hadhara ya TANU ilipoanza Rajab aliwakusanya vijana wenzake wanne wakaanzisha kwaya ya kwanza ya TANU Rajab akiwa kiongozi na mtunzi mkuu wa nyimbo za kuhamasisha watu kujiunga na TANU na nyimbo za kuwasema Waingereza.

Wanakwaya wenzake walikuwa Said, Abdallah, Juma, Binoga na Katumbwele.

Said akatunga nyimbo ya kwanza iliyokuwa ikisema, '' Watanganyika njooni tuchanganyike tukisifie chama chetu cha TANU Mola akipenda tupate uhuru.''

Rajab akatunga, ''Sikia wana kuteseka nchi ni shida tupu yatukalia sisi Watanganyika tunateseka kutawaliwa ni fedheha.''

Hizi nyimbo zilipokuwa zikiimbwa pale Mnazi Mmoja kabla Nyerere hajapanda jukwaani zilikuwa zikiwajaza hamasa wananchi.

Kwaya hii ilitunga nyimbo nyingi sana ambazo nyingine hadi leo bado zinaimbwa kama ile nyimbo maarufu, ''Tazama Ramani.''
 
Rajab anaonekana umri umechukua nafasi yake.Siku hizi anafanya nini ?.
 
Mkuu Mohamed Said nijuavyomimi wimbo "Tazama ramani" ulitungwa na kuimbwa na Brig Mosses Nnauye.Ikiwa sivyo niko tayari kusahihishwa.
 
Mkuu Mohamed Said nijuavyomimi wimbo "Tazama ramani" ulitungwa na kuimbwa na Brig Mosses Nnauye.Ikiwa sivyo niko tayari kusahihishwa.
Ngongo,
Inawezekana labda huo uliotungwa na Moses Nnauye si huu niliokuwanao mimi.

Nimerekodi nyimbo chache alizoniimbia Mzee Matimbwa nitausikiliza huu kama
ndiyo huo kisha nitakufahamisha.

Nakushukuru kwa taarifa hii.
 
Mkuu Mohamed Said nijuavyomimi wimbo "Tazama ramani" ulitungwa na kuimbwa na Brig Mosses Nnauye.Ikiwa sivyo niko tayari kusahihishwa.

Ngongo,
Hapa nasikiliza mazungumzo yangu na Mzee Rajad Matimbwa.

Katika haya mazungumzo anasema kuwa nyimbo hii, ''Tazama
Ramani,'' aiitunga yeye mwaka wa 1955 na kuna kisa katika utunzi
wake.

Mzee Rajab anasema Said Chamwenyewe mmoja wa viongozi
wa TANU pale makao makuu alikamatwa kwa kuua tembo Rufiji.

Said Chamwenyewe enzi zile akijulikana kwa uwindaji kama huu.

Alipofikishwa mahakamani alihukumiwa kifungo na hili likawa ni pigo
kwa TANU.

Hii beti ameniimbia Mzee Rajab na naiweka hapa chini:

''Tazama ramani utaona nchi nzuri yenye mito na mabonde mega
na mipaka majira yetu hayo yangekuwa hivi sasa utumwa wa nchi
TANU itaukomesha...''

*hili neno mega sijui maana yake.

Mzee Rajab anasema neno walilotumia mwaka wa 1955 ni ''TANU
itaukomesha,'' baadae wakabadili ikawa, ''Nyerere ataukomesha.''

Mzee Rajab alisema walitaka kumuonyesha Muingereza dhulma
yake ya kumfunga Mtanganyika kwa kutumia mali yake mwenyewe.

Bila shaka akiwa na maana kuwa vipi mtu aadhibiwe kwa kutumia
chake?

Mzee Rajab anasema Mzee Rupia aliwaruhusu kujenga kibanda
chao cha makuti nyuma ya ofisi ya TANU na hapo ndipo walipokuwa
wao wakikutana na kufanya mazoezi ya nyimbo zao hapo na nyimbo
hii ilitungwa katika kibanda hicho.

Chamwenyewe ndiye mwana TANU wa kwanza kuleta wanachama
wa kwanza wa TANU kutoka Rufiji baada ya Waingereza kukataa bila
ya sababu ya maan kuisajili TANU kwa kisingizio cha kuwa TANU haina
wanachama.

Alikuwa akienda Rufiji kwa baiskeli akiuza kadi za TANU kijiji baada
yakijiji na akirudi anakabidhi fedha kwa Iddi Faizi Mafongo mweka
hazina wa TANU Makao Makuu.

er3mN_wkwF353N0AAsbIXj4m6-3WKo4MbV1iG1xRpQIxIuKMEuppS-jUVWnP7xDLNtg4nqeyUpH7otXtLrqMJeXpwB_Q1E7oAJ_c1ZqEEB9VUqn4nywG5eW4VX9Sh_1A7xWZ16BPTFL9SMt6cFdcwCMeFGFp57GHq4tU3ya7BO6AB1ivRK8cAyUrnNRnwoAjnj-_zvrqiJZ4dL2kRBH3YkBhuy3hncjafCx_76pB-un2ay3l250aPbXqxYcqzwASH0oQuGOOIvvSh16RURA_-9jKnTZ3nSF42AHDb1ov12G9lpSHz1PdtNfmK-PNuP0wB1rA3o1kyDJao3g-Sk3FdsYbG3buJ-Hf_OUv8AgiItdiDUbe6p4jHvQncc0E1SpNF7699lok8BlOJxEe58zLN-t6n6jZ77YZW-bJXFNhVO2lzkTVYfa3vrqtLy6wq_j9915S1ACFb85ffMO7O-5uJ1Rsal1lCqzNqJcPPfAConUih_3aO9PX_s0gYAITJRtkXSoSZUOtR8pYU2Y2p0NPG9qvgH9iPsJ8bgp2vWPgONV25qpFdaWnEV7BxMvAYGVL0x46OBtOoLUqCMvN-YZePRdd4xTNCLU=w876-h657-no

Wa nne kulia ndiye Said Chamwenyewe
 
Back
Top Bottom