Rajabu Matimbwa kutoka TANU 1954 hadi CCM 1977

Rajabu Matimbwa kutoka TANU 1954 hadi CCM 1977

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
RAJAB MATIMBWA MWANACHAMA NA MWANA KWAYA YA TANU 1954 NA MWANACHAMA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) 1977

Sijui kwanini siku zote ninapowataja wanachaa wa TANU ile ya mwaka wa 1954 huwa namsahau Rajab Matimbwa.

Hivi karibuni nikamkumbuka Athmani Matenga, Mama Maria Nyerere na Bilal Rehai Waikela kama wanachama wa TANU ya 1954 ninaowafahamu kuwa wako hai huwa namsahau Rajab Matimbwa huyo hapo chini.

Mzee Rajab Matimbwa alikuwa mmoja wa waasisi wa kwaya ya TANU pale New Street mfadhili wa kwaya ile akiwa John Rupia ambae aliwapa sehemu nyuma ya ofisi ya TANU uani kufanya mazoezi yao ya kuimba.

Nilikuwa natembea maktaba na nikakuta picha hii ambayo nilipiga na Mzee Rajab mwaka wa 2016 na nikaona pia shahada yake ya kiapo kama mwanachama wa CCM.

Picha ya kiapo iko hapo chini.

Nimeona niweke machache katika yale amayo nimepata kuaandika kuhusu mzalendo na mpigania uhuru huyu wa Tanganyika.


Rajab Matimbwa katoka Chole, Uzaramo kaja Dar es Salaam kijana mdogo kutafuta maisha.

Rajab Matimbwa Bi. Titi ni shangazi yake na akikaa nyumbani kwake Shauri Moyo.

Harakati za kudai uhuru zilipoanza Dar es es Salaam Rajab akajikuta ana kibarua cha kuuza maji kwenye bomba moja lililokuwa linatazamana na ofisi ya TANU New Street (Sasa Lumumba Avenue).

Kabla ya kufanya kazi ya kuuza maji tayari Rajab alishapewa kibarua na John Rupia cha kuuza mgahawa pembeni ya Pugu Road na ikatokea akaelewana vizuri sana na Mzee Rupia na familia yake yote akawa mtoto wa nyumbani.

Rajab anawakumbuka watoto wa Mzee Rupia, Paul na dada yake Kipanya, Mpuya (Stephen) na kaka yao mkubwa Albano.

Mzee Rupia alikuwa na lori lake limeandikwa, ''Msichoke,'' likibeba mijengo.

(Nimeweka picha ya lori hilo hapo chini ikimuonyesha John Rupia na hili lori lake ''Msichoke'').

Mikutano ya hadhara ya TANU ilipoanza Rajab aliwakusanya vijana wenzake wanne wakaanzisha kwaya ya kwanza ya TANU Rajab akiwa kiongozi na mtunzi mkuu wa nyimbo za kuhamasisha watu kujiunga na TANU na nyimbo za kuwasema Waingereza.

Wanakwaya wenzake walikuwa Said, Abdallah, Juma, Binoga na Katumbwele.

Said akatunga nyimbo ya kwanza iliyokuwa ikisema, '' Watanganyika njooni tuchanganyike tukisifie chama chetu cha TANU Mola akipenda tupate uhuru.''

Rajab akatunga, ''Sikia wana kuteseka nchi ni shida tupu yatukalia sisi Watanganyika tunateseka kutawaliwa ni fedheha.''

Hizi nyimbo zilipokuwa zikiimbwa pale Mnazi Mmoja kabla Nyerere hajapanda jukwaani zilikuwa zikiwajaza hamasa wananchi.

Kwaya hii ilitunga nyimbo nyingi sana ambazo nyingine hadi leo bado zinaimbwa kama ile nyimbo maarufu, ''Tazama Ramani.''

Screenshot_20220302-230455_Facebook.jpg
 
Lory lilikua aina gani hili ningependa kufahamu wakulungwa
 
Back
Top Bottom