Rally ARUSHA

Steph Curry

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
5,936
Reaction score
4,707
Leo kuna mbio za magari kule Arusha.. Sijui ni kwanini huu mchezo hauna Updates huku au ndio zile fikra za mchezo wa wahindi. Mlioko Arusha tunaomba Updates wengine tumeshindwa kuja huko. Washiriki maarufu wa Tz watakuwepo akiwemo bingwa Babu Pandya na Raj Deere

<strong><span style="font-family:comic sans ms;">
CC: Bigjahman kingkongIII

Last edited by a moderator:
Ndo najiandaa kuelekea kibo palace yanapoanzia leo saa nane mchana.rally sio mchezo wa kiindi baalai ni wa wote
 
Ndo najiandaa kuelekea kibo palace yanapoanzia leo saa nane mchana.rally sio mchezo wa kiindi baalai ni wa wote

Mkuu utatushushia Updates aisee..
twentyfourseven upo??
 
Last edited by a moderator:
Ojare Arnold > Rally of Tanzania
PROVISIONAL ENTRY LIST FOR THE UP COMING U-TRACK NANE NANE
RALLY 2015.
1. ONKAR RAI (EVO 10) KENYA
2. TEVJEER RAI (PORCHE 911) KENYA
3 JASSI CHATTHE (EVO 10) KENYA
4.GERALD MILLER (EVO 9) TANZANIA
5.GRUPAL SANDHU (EVO 10) TANZANIA
6. SHAFIN KHAN (EVO 9) TANZANIA
7. ASAD KHAN (KALULU) (N10) KENYA
8.RANDEEP SINGH ( EVO 9) TANZANIA
9. DHARAM PANDYA (EVO 9) TANZANIA
10.ALISTAIR CAVENAGH (PORCHE 911) KENYA
11. KAILESH CHOULAN ( FORD ESCORT MK II) KENYA
12.LARRY HORN (PORCHE 911) TANZANIA
13.JAYANT SHAH(PORCHE 911) TANZANIA
14. GURJIT DHANI (N10) TANZANIA
15. RAJPAL DHANI (N10) TANZANIA
16. KIRIT PANDYA ( GC8) TANZANIA
17. BINESH HARIA( GC8) TANZANIA
18. RAYMOND KAIRUKI (SUBARU LEGACY EX - AZAR ANWAR) KENYA
19. SALVATORY MCHARO ( GC8) TANZANIA
20. TEJI BALA (EVO 4) TANZANIA
21.ERFAN ALADIN (EVO 9) TANZANIA
22. FAISAL NANYANI (N11) TANZANIA
23. JAMIL KHAN (N12) TANZANIA
24. JUMA SHABANI (N10) TANZANIA
25. RAFIQUE DIN MOHAMED (PEUGOT 505 V8) TANZANIA
26. VICTOR ROGATH (SUBARU LEGACY) TANZANIA
27.HAKIM (GC8) TANZANIA
28. ABDUL (FORD EX MDABI) TANZANIA
29. KELVIN TAYLOR (TOYOTA CELICA GT4) TANZANIA
30. BOB TAYLOR (SUBARU LEGACY) TANZANIA
 
Naona Babu Pandya kaja kivingine.. Last time nilimwona akitumia Subaru..

Huyo Tevjeer si ndo yule bingwa wa Kenya??
 
Uyo dharam pandya ni Mtoto wa kirit pandya babu,dharam ndo anaongoza kwa point apa tanzania akifatiwa nadhan na babu miller aliyeshinda rally ya africa juz kat iliyofanyikia dar au chali flan wa Moshi jina limenitoka kidogo
 
Huyo Chalii wa Moshi ni Muhindi?? Huyo Salva Mcharo ni wa Arusha au??

Mbio za mwaka jana Kirit na Mwanaye walikuwa gari moja.. Nadhani mmoja alikuwa navigator
 
Uyo Bro wa Moshi anaitwa gurjit dhani, mcharo ni wa Moshi na ni mtamu kweli,dharam alikuwa na gar yake mwenyewe na kirit alikuwa na gar yake mwenyewe pia
 
Ila madereva wakali wanaotesa tz wako Arusha na kilimanjaro ngoja Dar na tanga moro wengi mabishoo dharam ndo anawabeba,na Gar kali ya rally ni mistubish evo
 
Uyo Bro wa Moshi anaitwa gurjit dhani, mcharo ni wa Moshi na ni mtamu kweli,dharam alikuwa na gar yake mwenyewe na kirit alikuwa na gar yake mwenyewe pia

Gurjit Dhani huyo jamaa kama namfahamu hivi.. Nadhani babake ni veteran nae alikimbizaga sana wakati wake..

Nadhani ni hao hao, wahindi flani hivi wanakaa pale Majengo Moshi
 
Ila madereva wakali wanaotesa tz wako Arusha na kilimanjaro ngoja Dar na tanga moro wengi mabishoo dharam ndo anawabeba,na Gar kali ya rally ni mistubish evo

Sure asee.. Hapa Dar ni watoto wa kihindi tu tofauti na Arusha, Moshi mpaka machalii blacks pia wanashiriki. Miaka miwili mbele nadhani tutakuwa na madereva wengi weusi kutoka Arusha na Moshi..

Nimeona Dharam anatumia Evo nyeupe leo..
 
Hii michezo haifanyiki mara kwa mara ndo maana inakuwa ngumu kuifuatilia.
Pia wanaoicheza wengi ni wahindi, hawapo humu. Facebook wana page yao inaitwa Rally in Tanzania. Kuke updates zote zipo.
 
Hii michezo haifanyiki mara kwa mara ndo maana inakuwa ngumu kuifuatilia.
Pia wanaoicheza wengi ni wahindi, hawapo humu. Facebook wana page yao inaitwa Rally in Tanzania. Kuke updates zote zipo.

Ni kweli mkuu lakini hilo la kutofanyika mara kwa mara sidhani kama ni kigezo kikubwa kiivo..

Alafu pia kuhusu wahindi, inaonekana hivo kwakuwa wengi ndio madereva ila kuna mashabiki wengi sana waswahili sana sana Arusha na Moshi. Rally za Dar ndio waswahili wanaoenda kufatilia ni wachache..
 
Tarizo ni udhamini asee wengi wnajitegemea mwenyewe tofauti na jirani zetu mf kenya wanamauzamini ya maana, kama uyo chantte rally ya dar alikuwepo na akapata ajali gari ikafa lkn leo si unaona yupo ingekuwa kibongo uyo lbd mpka mwakani,wengi tz they do for love tena ni wazalendo kweli maana gari ya rally kuihudumia inaitaji kibunda ndefu et na zote wanatoa mifukoni mwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…