RamaDBK LTD Japanese Car Exporter

moto2012

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
2,271
Reaction score
1,493
Wadau naombeni msaada wa kuwajua Hawa jamaa, nataka kununua gari kutoka kwao, naomba kujulishwa hawajamaa ni wa kuaminika? Na condition ya magari yao ipoje? On average ni Siku ngapi nitasubiri? Msaada tafadhali kwa wenye uzoefu nao
 
Kwa hakika RAMA DBK Ltd ni kampuni ya zamani na wanauza magari yenye condition nzuri sana. Nimekuwa mteja wao toka miaka ya 1990s hadi miaka michache nyuma niliposita kuagiza magari baada ya kustaafu biashara yangu. Bei zao zinakuwa juu zaidi ya magari ya mekampuni mengine ya huko Japan lakini ni watu Trusted na magari yao condition zake safi sana.
 
Ni kampuni ya kuaminika na wana magari mazuri. Mimi pia ni mteja wao ,nimenunua magari mawili ,yalikuja na hali nzuri sijapata usumbufu. Muda kwa order ni kama wiki 3 hivi mali inafika bandarini. Kwa bei wako juu, ila ubora ulinifanya nirudi tena kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…