Ramadhan imekwisha, tuendelee na ujenzi wa taifa

Ramadhan imekwisha, tuendelee na ujenzi wa taifa

Mpekuzi Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2018
Posts
650
Reaction score
1,016
Pasaka imeenda
Ramadhan imekwisha

Sasa turudi kwenye ujenzi wa Taifa. Kuna waliokuwa wanafanya mashindano kulisha iftar, iftar ilikuwa sio Ibada Tena bali mashindano.

Uvaaji wa Baragashia na kanzu ukawa fasheni kwa haraka haraka ungeingia tanzania kama huijui ungesema upo kwenye Taifa la ki "circular" kama Afghanistan au Uzibekhistan.

Tunashukuru Mungu Tumemaliza salama, Sasa turudi kwenye ujenzi wa Taifa na wanaotakiwa kuwajibika wawajibike kikweli kweli Taifa lisonge mbele
 
Tanzania hii hii eti kuna watu walikuwa wanakamatwa kwa sababu ya kula mchana. Sijui tangu lini tumekuwa taifa la sheria za kidini. Baada ya jamii kuhoji sana, ikabambikwa kesi ya bangi. Kwa hiyo naunga mkono kwamba mambo yameisha, sasa tuendelee na kazi iendelee.
 
Eid Mubarak kwa ndugu zetu waislamu wote.

Jambo la msingi ni kufuata mafundisho yaliyo patikana kwenye mwezi wa Ramadan.
Hakika waislamu wote haswa wanawake walikuwa wanavaa mavazi ya heshima n.k basi yafuatwe hayo.
 
Mjinga kweli wewe yaani mjinga mnoo tena ondoa laana zako hapa.....
Aliyekwambia ramadhani ilikua ni kizuizi cha maendeleo nani?
Shubaamit!!!!!
 
Kuna utamaduni unaingia kwa kasi mpaka kwenye vyombo vya serikali kufuturisha bila aibu kana kwamba nchi inaongozwa kwa misingi ya imani ya dini fulani.

Huu udini ukimea mpaka ndani ya idara za serikali italeta mtafaruku kwa kuwa nchi haiongozwi kidini. Ifta za nini kwenye taasisi hizo wakati hicho chakula ni cha ibada ya dini?

Ngoja wengine tukemee kwa kuwa si utamaduni wa taifa hili kuingiza imani za dini fulani kwenye vyombo vyake waziwazi au kwa namna yeyote ile.

Hii sio nchi ya kidini, hizo futari ziandaliwe huko wahusika wa dini hiyo wanakokutana kumuabudu Mungu wao.

Haileti sura nzuri kwa taifa la kisekula kuingiza ibada za dini fulani ndani ya taasisi zake huo ni ushetani
 
Kuna utamaduni unaingia kwa kasi mpaka kwenye vyombo vya serikali kufuturisha bila aibu kana kwamba nchi inaongozwa kwa misingi ya imani ya dini fulani. Huu udini ukimea mpaka ndani ya idara za serikali italeta mtafaruku kwa kuwa nchi haiongozwi kidini. Ifta za nini kwenye taasisi hizo wakati hicho chakula ni cha ibada ya dini? Ngoja wengine tukemee kwa kuwa si utamaduni wa taifa hili kuingiza imani za dini fulani kwenye vyombo vyake waziwazi au kwa namna yeyote ile. Hii sio nchi ya kidini, hizo futari ziandaliwe huko wahusika wa dini hiyo wanakokutana kumuabudu mungu wao. Haileti sura nzuri kwa taifa la kisekula kuingiza ibada za dini fulani ndani ya taasisi zake huo ni ushetani
Eid mubarak kafiri jisikieni huru karibuni tunyweni na tuleni vilivyovizuri
 
Uvaaji wa Baragashia na kanzu ukawa fasheni kwa haraka haraka ungeingia tanzania kama huijui ungesema upo kwenye Taifa la ki "circular" kama Afghanistan au Uzibekhistan
Aisee! Mkuu ilikuwa unaumizwa na vitu vidogo sana. Ungepotezea tu kwa kuwa Kila mtu ana Imani na itikadi zake
 
Nasisitiza Dhambi na Tamaa iendelee kuchukiwa japo shetani kafunguliwa rasmi ila tujikaze tu tukatae kiti moto, pisi na pombe hata kama shibe itatupeleka vibaya kiasi gani.
 
Back
Top Bottom