Ramadhan Special Thread

Skip to main content



Search form​




Ukurasa Wa Kwanza /Fiqh Ya Swawm Ya Ramadhwaan Kutoka Kitabu 'Al-Wajiyz Fiy Fiqhis-Sunnah Wal-Kitaabil-'Aziyz

Fiqh Ya Swawm Ya Ramadhwaan Kutoka Kitabu 'Al-Wajiyz Fiy Fiqhis-Sunnah Wal-Kitaabil-'Aziyz​

Ramadhaan-Swawm

Fiqh Ya Swawm Ya Ramadhwaan
Kutoka Kitabu 'Al-Wajiyz Fiy Fiqhis-Sunnah Wal-Kitaabil-'Aziyz

Alhidaaya.com


Kufunga mwezi wa Ramadhwaan ni moja katika nguzo za Dini yetu ya Kiislamu na moja katika mambo ya lazima yampasayo kila Muislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Anasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: 183]

Baada ya Aayah hii Allaah (Subhaanahu wa Ta´aalaa) Anasema tena:

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; na ili mkamilishe idadi na ili mumkabbir Allaah kwa kuwa Amekuongozeni na ili mpate kushukuru. [Al-Baqarah: 185]


Ibn ´Umar (Radhwiya Allaahu ´anhuma) alimsikia Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Uislaam umejengewa katika (nguzo) tano: Kuthibitisha kidhati kuwa hakuna Rabb apasae kuabudiwa kwa Haqq ila Allaah, na kuthibitisha kidhati kuwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) ni Rasuli Wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kutekeleza ´Ibaadah ya Hajj kwa mwenye uwezo, na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhwaan.” [Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim].

Waislamu wote wamekubaliana kuwa kufunga mwezi wa Ramadhwaan ni wajibu wa kila Muislamu na kuwa ni moja katika (nguzo) za Uislaam na ni jambo lenye kujulikana katika Dini yetu kwa kutekelezwa kwake. Yeyote atakayekanusha ´Ibaadah hii ya Kufunga mwezi wa Ramadhwaan kuwa si wajibu kwa kila Muislamu atakuwa amekufuru Kufru ambayo inamtoa katika Uislaam.

Uzuri Wa Kutekeleza ´Ibaadah Ya Kufunga Mwezi Wa Ramadhwaan

Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ´anhu) alimsikia Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi sallam) akisema:

“Yeyote atakayefunga mwezi wa Ramadhwaan kwa Imani na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah basi Allaah Atamsamehe madhambi yake yote yaliyopita.” [Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim, An-Nasaaiy na Ibn Maajah].

Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ´anhu) amesema tena, alimsikia Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:

“Allaah amesema: “Kila ‘Amali ya mwanaadam ni yake yeye mja Wangu ila Swawm. Ni yangu Mimi na mimi ndiye Nitakayemlipa mja Wangu.”

Swawm ni kinga. Itakapofikia siku mmoja wenu amefunga ajiepushe na kufanya kitendo cha jimai na mabishano na watu. Na yeyote atakayetaka kupigana naye basi amwambie “Mimi nimefunga.” Naapa kwa jina la Allaah, Harufu inayotoka katika mdomo wa mwenye kufunga ni nzuri kwa Allaah kuliko harufu ya Misk. Kwa Mwenye kufunga ana furaha mbili: Furaha anapofungua Swawm yake na furaha pale atakapoonana na Rabb Ameridhika kwa kufunga kwake.” [Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim na An-Nasaaiy]

Sahl ibn S’ad (Radhwiya Allaahu ´anhu) alimsikia Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:

‘’Jannah kuna mlango unaitwa Ar-Rayyaan. Wale wenye kufunga wataingia Jannah kupitia lango huu siku ya Qiyaamah na hakuna mwengine atakayepita katika mlango huu ila (wafungaji). Itaambiwa: ‘’Wako wapi waliokuwa wakifunga?” Watasimama na watapita katika mlango huu na watakapomalizika kuingia wote (wafungaji) utafungwa na hakuna mwengine atakayepita hapo tena.“ [Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim, At-At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na An-Nasaaiy].

Kufunga Mwezi Wa Ramadhwaan Ni Wajibu Pale Mwezi Unapoonekana

Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ´anhu) amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi sallam) akisema:
“Fungeni kwa kuona au kuandama mwezi wa Ramadhwaan na fungueni (malizeni) kufunga mwezi wa Ramadhwaan kwa kuona mwezi na msipouona mwezi basi timizeni siku thelathini.” [Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy, Muslim, na An-Nasaaiy].

Mwezi Wa Ramadhwaan Unathibitishwaje Kuonekana Kwake?

Mwezi wa Ramadhwaan unathibitishwa kuonekana kwake na mtu mmoja mwenye kujulikana kwa ukweli na kumcha kwake Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) au kwa kutimiza siku thelathini za mwezi wa Sha’abaan.

Ibn ´Umar amesema watu walikuwa wakitafuta kuandama kwa mwezi. nikamjulisha Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa mimi nimeuona mwezi. Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) akafunga na akaamrisha watu wafunge.” [Hadiyth Swahiyh. Angalia Kitaab I’rwa al-Ghaliyl na. 908 na Imeripotiwa na Abu Daawuwd].

Ikiwa mwezi haukuandama, kwa sababu ya kufunikwa na mawingu au kwa sababu nyingine basi hapo mwezi wa Sha’abaan utatimizwa kwa siku thelathini kama alivyoripoti Abu Hurayrah katika Hadiyth iliyo hapo juu.

Lakini mwezi wa Shawwaal unatangazwa kuonekana kwa mashahidi wawili.’ ´Abdur-Rahmaan bin Zayd bin Al-Khatwaab amesema: “Nilipokuwa nikikhutubia siku ambayo ni ya shaka (kama mwezi wa Ramadhwaan kama umekwisha ama la), nikasema: “Nilikaa na Swahaba zake Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) nikawauliza wao. Wakaniambia mimi kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alisema:

‘’Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi na tekelezeni ´Ibaadah ya Hajj kwa haki zake. Ikiwa kuna mawingu basi timizeni siku thelathini. Na Ikiwa Waislamu wawili watachukua kiapo kwa kuonekana kwa mwezi basi fungeni na mfungue kwa kushuhudia kwao mwezi.’’ [Hadiyth Swahiyh. Angalia Kitaab cha Shaykh Al-Albaaniy, Swahiyh al-Jamiy’ Asw-Swaghiyr na. 3811. Pia Imeripotiwa na Imaam Ahmad na An-Nasaaiy bila kipande kinachosema ‘’Waislamu wawili.’’].

Mtawala wa Makkah, Al-Haarith bin Hatwiyb amesema:

“ Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) alituambia sisi tekelezeni ´Ibaadah ya Hajj kwa haki zake munapouona mwezi. Na ikiwa hamkuuona mwezi lakini mashahidi wawili wa kuaminika wakishuhudia kwa kuona mwezi tunatekeleza ´Ibaadah ya Hajj kutokana na ushahidi wao.’’ [Hadiyth Swahiyh angalia Shaykh Al-Albaaniy, Swahiyh Sunan Abiy-Daawuwd, na. 205. Imeripotiwa na Abu Daawuwd].

Tukiangalia ripoti mbili hizi,

’’Ikiwa waislamu wawili watachukua kiapo kwa kuona mwezi, basi fungeni na fungueni’’ katika Hadiyth ya Abdur-Rahmaan bin Zayd na:

‘’Na ikiwa hamkuuona mwezi lakini watu wawili wenye kujulikana kwa ukweli wakasema wameuona mwezi tunatimiza haki za ´Ibaadah ya Hajj kutokana na ushahidi wao.’’ katika Hadiyth ya Al-Haarith wanaonyesha kwa kutilia mkazo, kuwa haifai kuanza kufunga au kumaliza kufunga kutokamana na ushahidi wa mtu mmoja pekee. Juu ya hilo, tangu kuanza kwa kufunga imeondolewa uzito kutokana na ushahidi (uliotolewa hapo juu), inawacha suala la kumaliza kufunga, ambalo halina ushahidi kwamba linatoshelezwa kwa ushahidi wa mtu mmoja pekee. Huu ni ufupi wa mjadala unaopatikana katika Kitabu ‘Tuhfah Al-Ahwadhiy’ [Mjalada wa 3, uk. 373-3749].

Tanbihi: Ikiwa mtu atauona mwezi yeye peke yake, hafungi mpaka watu wafunge na hamalizi kufunga mpaka watu wamalize kufunga kama ilivyoripotiwa na Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ´anhu), kwamba amesema Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam):

‘’Swawm (kufunga) ni siku ambayo watu wanafunga. Na kumaliza kufunga ni siku ambayo watu wanamaliza kufunga. Na kuchinja ni katika siku ambayo watu wanachinja.’’ [Hadiyth Swahiyh. Angalia Swahiyh Al-Jami’ Asw-Swaghiyr, na. 3869]. Imehifadhiwa na Imaam At-At-Tirmidhiy ambaye amesema: ‘’Baadhi ya ‘Ulamaa wanaifasiri Hadiyth hii kwa maana: “Kuanza kufunga na kumaliza kufunga kunatekelezwa na watu wote kwa pamoja na wakati mmoja.”

Nani Anawajibika Kufunga

‘Ulamaa wamekubaliana kufunga ni wajibu kwa mwenye akili timamu, Baleghe, mwenye afya na mkazi wa mji. Tukiongezea wanawake waliotwaharika na hedhi na nifasi.

Kwa wale ambao Swawm si wajibu juu yao ni wale ambao hawana akili timamu, hawajabaleghe.

Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Kalamu (kurekodiwa ‘amali) imeinuliwa (hairekodi) kwa watu watatu: anayepatwa na usingizi mpaka aamke, mtoto mpaka afike umri wa kubaleghe, na aliorukwa na akili mpaka atakapopata akili timamu.” [Hadiyth imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jami´, na. 3513 na Imerikodiwa na Abu Daawuwd].

Ama kwa wale wasioweza kufunga ni kutokamana na maneno Yake Allaah:

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ
Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. [Al-Baqarah: 185]

Ikiwa mgonjwa au msafiri atafunga basi inawatosheleza, ama wakichukua ruhsa ya kula hapo wameondolewa uzito. Ama wakiamua kufunga kwa kuwa wanataka kufunga hapo pia wako sawa.

Ni kupi bora: Kutofunga au Kufunga?

Ikiwa mgonjwa au msafiri hawatoona tabu yoyote katika kufunga, basi kufunga kunapendekezwa. Ama wakikhofia kupata tabu kutokamana na kufunga, basi hapo kutofunga kunapendekezwa.

Abu Sa’iyd al-Khudriy ameelezea:

‘’Tulikuwa vitani na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa Ramadhwaan. Wengine katika sisi walikuwa wamefunga na wengine walivunja Swawm zao. Wale waliofunga hawakuwaona waliovunja Swawm zao kuwa wako makosani na waliokula pia hawakuwaona waliofunga kuwa wako na makosa. Waliona wenye uwezo wa kufunga (walifunga) na hilo ni jambo zuri. Na ambao hawakuweza kufunga walivunja Swawm zao kwa udhaifu wa kufunga (hawakufunga) na hili pia ni jambo zuri.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Sunan At-At-Tirmidhiy na. 574. Pia imerikodiwa na Imaam Muslim].

Ushahidi wa wanawake wasio Twahara kuwa hawafungi ni Hadiyth ya Abu Sa´iyd ambayo Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

’’Je, si kwa kesi kwamba anapopatwa na damu yake ya mwezi, haswali wala hafungi? huo ni upungufu katika Dini yake.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy, katika Mukhtaswar Swahiyh Al-Al-Bukhaariy na. 951. Imerikodiwa na Imaam Al-Al-Bukhaariy].

Ikiwa mwanamke asiyo Twahara atafunga basi swawm yake haikubaliki kwani katika masharti ya kukubalika swawm ya mwanamke ni awe katika Twahara. Mwanamke pia itamlazimu alipe siku alizokosa kufunga. ´Aaishah (Radhwiya Allaahu ´anhu) amesema:

“Tulipokuwa tukipatwa na siku zetu za ada wakati wa Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) tuliamrishwa kulipa Swawm za siku tuliokosa kufunga na hatukuamrishwa kulipa Swalah tulizokosa.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Sunan At-Tirmidhiy na.630. Imerikodiwa na Imaam Muslim, Abu Dawuud, At-Tirmidhiy na An-An-Nasaaiy].

Yanayomlazimu Mtu Mzima Na Mwenye Ugonjwa Wa Kuendelea

Asioweza kufunga, kwa ajili ya utu uzima au kwa ajili sababu nyenginezo, hatofunga badili yake atalisha maskini mmoja kwa kila siku aliokosa kufunga. Allaah (Subhanahu wa Ta’aalaa) Amesema:
وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ
“Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. (kwa kila siku).” [Al-Baqarah: 184)

‘Atwaa’ amesema alimsikiya Ibn ´Abbaas akisoma Aayah hii kisha akasema ‘’Haikuondolewa. Inawahusu watu wazima waume kwa wake ambao hawawezi kufunga. Ndio watalisha masikini mmoja kwa kila siku ambayo hawakufunga.” [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl na.912 na Imerikodiwa na Imaam Al-Bukhaariy].

Mwanamke Mja Mzito (Mwenye Mimba) Au Mwenye Kunyonyesha

Mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha ambaye hana uwezo wa kufunga ama ambaye anahofia afya ya mtoto wake anaweza asifunge, atalisha maskini mmoja na hawajibiki kuilipa siku aliyokula. Ibn ´Abbaas amesema:

“Ruhusa amepewa mtu mzima mume au mke ambapo wataoneleya tabu kufunga, hawatofunga ambapo hawatopendeleya kufunga na watalisha maskini mmoja kwa kila siku ya kufunga. Kisha hawatalipa siku walizokosa kufunga hii iliondolewa baada ya Aayah hii:

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ
Na kwa wale wanaoiweza lakini kwa mashaka na kutaabika watoe fidia; kulisha masikini. [Al-Baqarah: 184]

Baada ya hapo ikahakikishwa kuwa mtu mzima mume au mke ambao hawawezi kufunga na mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha, ikiwa watahofia, hawatafunga na watalisha maskini kwa kila siku ambayo hawakufunga. [Msururu wa Riwaayah hii ni madhubuti imeripotiwa na Al-Bayhaqiy]. Pia imerikodiwa kuwa alisema, ikiwa wakati wa Ramadhwaan mwanamke mwenye mimba anahofia afya yake, au mwenye kunyonyesha anahofia afya ya mtoto wake, hawatafunga na watalisha maskini mmoja kwa kila siku ambayo hawakufunga na hawatalipa siku hizo kwa kufunga. [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl mjallad 4 uk.19].

Nafi’iy alisema ’Mmoja katika mabanati wa Ibn ´Umar aliolewa na mwanamume wa ki-Quraysh. Akapata mimba na wakati wa Ramadhwaan anashikwa na kiu sana. Ibn ´Umar akamwambiya funguwa swawm yako na ulishe masikini kwa kila siku.’’ [Msururu wa Riwaayah ni Swahiyh na Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl mjallad 4 uk.20. Imerikodiwa na ad-Daraqutniy].

Kiwango gani cha chakula anawajibika kulisha?

Imeelezwa kwamba Anas Ibn Malik alidhoofika sana na hakuweza kufunga mwaka mzima akatayarisha sufuriya Thariyd (Mkate na nyama uliolowana katika supu) kisha akaalika masikini thelathini akawalisha mpaka wakaridhika’’. [Msururu wa Riwaayah hii ni Swahiyh pia imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl, mjallad 4 uk.21 imerikodiwa na ad-Daraqutniy].

Yaliyo Muhimu Kwa Ujumla Wa Kutekeleza ´Ibaadah Ya Swawm (Kufunga)

1). Niyyah.

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amesema:

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاء وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ وَذَلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ
Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara. [Al- Bayyinah: 05]

Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

’’Kila kitendo hulipwa (kutokana na) niyyah na kila mtu ni lili alilonuwiya.’’

Na niyyah mahala pake ni moyoni. Niyyah ya kufunga ni lazima iwe moyoni kila usiku kabla ya wakati wa Fajr kuingiya.

Hafsah (Radhwiya Allaahu ´anha) amesema Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

‘’Hana swawm asiyenuwia kufunga kabla ya fajr.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jamiy´ as-Saghiyr, na.6238. Pia imerikodiwa na Abu Dawuud, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy].

2). Kujiepusha katika masiku ya kuamka na swawm na chochote chenye kubatilisha swawm yako (tangu wakati wa adhaana ya pili) na usiku mpaka kutakapopambauka (Jua kuchomoza).

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَكُلُواْ وَاشْرَبُواْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّواْ الصِّيَامَ إِلَى الَّليْلِ
Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku. [Al-Baqarah: 187].

Mambo Sita Yanayobatilisha Swawm

a). na b). Kula au kunywa kwa kukusudia.

c). Kujitapisha kusudi.

d). na f). Mwanamke atakapopata ada yake mwezi akiwa katika swawm.

g). Kitendo cha Jimai.

Mambo Yaliyopendekezwa Kwa Mwenye Swawm

Imependekezwa kwa mwenye kufunga afuate Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) katika kujitayarisha na swawm yake nayo ni haya yafuatayo;


i. Kula daku

Amehadithia Anas (Radhwiya Allaahu ´anhu) Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
‘’Kuleni daku, kwani kula huko daku kuna baraka.” [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Nasaa’y na Ibn Maajah].

Na ‘’kuleni daku’’ hata kama kwa kunywa maji inatosheleza. ´Abdullaah Ibn ´Amr amehadithia Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

’’Kuleni daku japo kwa kunwa tama la maji.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jamiy´ as-Swaghiyr na.2945 imeripotiwa na Ibn Hibbaan].

Pia Imependekezwa kuchelewesha kula daku. Amehadithiya Anas kutoka kwa Zayd ibn Thabit ambaye amesema:

‘’Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) alikula daku kisha akatoka kwenda kuswali. Anas akamuuliza “Kulikuwa na muda gani baina chakula cha daku na adhaana?” Akajibu: “Ilikuwa kiasi cha kusoma Aayah khamsini za Qur-aan". [Imeripotiwa na Imam Al-Bukhaariy na Muslim].

Pia ameruhusiwa amalize chakula chake anaposikia Adhaana ya Fajr. Abu Hurayrah amehadithia Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Endapo mmoja wenu atasikiya adhaana na mkononi mwake ana kinywaji, asirudishe kinywaji hicho mpaka aridhike nacho.’’(yaani anywe mpaka amalize haja yake). [Imesahihishwa na Shaykh al-Albaaniy katika al-Jami' as-Swaghiyr na.607].

ii. Kujiepusha na maneno ya Upuuzi na mambo yasofaidisha Swawm yako.

Amehadithia Abu Hurayrah Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

’’Ikiwa mmoja wenu yuko ndani ya swawm ajiepushe na kitendo cha jimai na mabishano. Na kukitoka mmoja anataka kupigana nawe basi mwambiye ‘’Mimi Nimefunga’’. [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim na An-Nasaaiy]. Tena amehadithiya Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:

’’Yeyote ambaye hatowacha kusema uongo na kutenda kwa uongo basi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) hana haja yake kwa kuwacha chakula chake na kinywaji chake’’. [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika mukhtasar Swahiyh Al-Al-Bukhaariy na.921].

iii. Kuwa na moyo kutoa na kujifunza Kusoma Qur-aan

Ibn ´Abbaas amesema:’’Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa mwenye moyo wa kutoa mali katika watu wote na akifanya vizuri kabisa. Alikuwa akitoa zaidi katika mwezi wa Ramadhwaan anapoonana na Malaika wa Allaah Jibriyl (´alayhis-salaam). Jibriyl anaonana naye kila usiku wa Ramadhwaan mpaka mwezi umalizike. Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) atasoma naye Qur-aan. Anapoonana na Jibriyl, alikuwa na moyo zaidi wa kufanya mema kuliko kuifadisha swawm yake’’. [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim].

iv. Kukimbilia (kuharakisha) kufungua swawm

Sahl Ibn Sa'd amehadithiya Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:

’’Watu watakuwa katika kheri endapo watakimbilia kufungua swawm zao’’.

v. Kufungua Swawm na yale yaliotajwa katika Hadiyth ikiwa ni rahisi kufanya hivo.

Anas amehadithia Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifunguwa swawm yake na Tende zilioiva kabla kusali. Kama si zilioiva alikuwa akifungua na Tende kavu. Kama hiyo pia haikupatikana basi alikuwa akifunguwa na kinywaji cha maji. [Ni Hadiyth Hasan Swahiyh katika al-Jamiy´ as-Swaghiyr na.2065]

Mambo Yanayofaa Kufanywa Na Mwenye Kufunga


· Anaruhusiwa kujisuuza kichwa na maji ya baridi.


· Kusukutua na maji bila kuyamiza na kutiya maji puani bila kuingiya ndani ya mwili.


· Kuumikwa ama kutoa damu kwa ajili ya matibabu.


· Kumbusu au kumgusa mke wako bila matamanio kwa mwenye kuweza kujizuwiya.


· Mwenye kuamka asubuhi na akiwa katika janaba.


· Kuchelewesha kufungua swawm mpaka saa ya kula daku.


· Kutumia mswaki, manukato, wanja, dawa ya macho na kudungwa sindano kwa ajili ya matibabu.








 
Skip to main content



Search form​




Ukurasa Wa Kwanza /Mwezi Wa Ramadhwaan Imeteremshwa Qur-aan - Jichumie Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan

Mwezi Wa Ramadhwaan Imeteremshwa Qur-aan - Jichumie Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan​

Ramadhaan-Swawm

Mwezi Wa Ramadhwaan Imeteremshwa Qur-aan
Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan

Alhidaaya.com


Ndugu Muislamu, jitahidi utekeleze ‘ibaadah hii adhimu kwa wingi ya kusoma na kuhifadhi Qur-aan kwa sababu fadhila na thawabu zake ni nyingi na ‘adhimu mno kama tunavozinukuu baadhi yake humu.

Pia jitahidi uweze kuhitimisha (kumaliza kuisoma) Qur-aan japo mara moja katika mwezi huu wa Ramadhwaan kwa sababu mwezi huu ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ
Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). [Al-Baqarah: 185]

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٢١﴾
121. Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo ya kusomwa kwake; hao ndio wanaokiamini, na atakayekikanusha basi hao ndio waliokhasirika. [Al-Baqarah: 121]
Imaam As-Sa’diy (Rahimahu-Allaah) amesema kuhusu Tafsiyr ya Aayah hiyo tukufu: “Allaah (Ta’aalaa) Anatujulisha kwamba wale ambao wamepewa Kitabu na Akawafanyia ihsaan kwa ujumla kwamba wao “Wanakisoma kwa haki ipasavyo kusomwa kwake” inamaanisha: Kuifuata kama ipasavyo kuifuata, na “tilaawah” (kuisoma) ina maana ni kuifuata yaani kuhalalisha Aliyoyahalalisha na wanaharamisha Aliyoyaharamisha, na wanafanyia kazi hukmu zake, na wanaamini Mutashaabihaat (Aayah zisizokukwa wazi maana yake), na hao ndio watu wenye furaha katika Ahlul-Kitaab, ambao hutambua neema za Allaah na wakazishukuru na wakamwamini kila Rasuli wala hawafarikishi baina yao, basi hao ndio Waumini wa kweli, si kama wale wanaosema:
نُؤْمِنُ بِمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ
“Tunaamini yale yaliyoteremshwa kwetu” na wanayakanusha yale yaliyokuja baada yake.” [Al-Baqarah: 91]

Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan



1) Kusoma Qur-aan Ni Kama Kufanya Biashara Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambayo Mtu Hapati Khasara.

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾ لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾
Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri wanataraji tijara isiyoteketea. Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake, hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani. [Faatwir: 29-30]

2) Aliye Bora Kabisa Ni Ambaye Anajifunza Na Kuifundisha Qur-aan
عن عثمانَ بن عفانَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قالَ: ((خَيرُكُم مَنْ تعَلَّمَ القُرآنَ وعَلَّمَه)) صحيح البخاريِّ
Imepokelewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha)) [Al-Bukhaariy]


3) Anayeisoma Kwa Mashaka Hupata Thawabu Mara Mbili

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ، وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ)) البخاري ومسلم
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah watukufu watiifu, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

Imekusudiwa ni mtu mwenye ulimi mzito au ambaye ndio kwanza anaanza kujifunza na hupata shida kuisoma, lakini inampasa Muislamu ajitahidi kujifunza kuisoma kisawasawa ipasavyo.

4) Watu Wanaoshikamana Na Qur-aan Ni Watu Bora Kabisa Mbele Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ لِلَّهِ أَهْلِينَ مِنْ النَّاسِ)) قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ مَنْ هُمْ قَالَ: ((هُمْ أَهْلُ الْقُرْآنِ أَهْلُ اللَّهِ وَخَاصَّتُهُ)) أحمد و إبن ماجه
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Anao watu wake kati ya wanaadam)). Wakamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah ni nani hao? Akasema: ((Hao ni watu wa Qur-aan na ni watu wa Allaah na wateule Wake)) [Ahmad, Ibn Maajah]

5) Mfano Wa Anayeisoma Qur-aan Ni Harufu Na Ladha Nzuri, Kinyume Na Asiyeisoma

عن أبي موسى الأشْعَريِّ رضي الله عنه أنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلّم قالَ ((مثلُ المؤمنِ الَّذِي يقرأ القرآنَ مَثَلُ الأتْرُجَّةِ ريحُها طيبٌ وطعمُها طيّبٌ، ومثَلُ المؤمِن الَّذِي لاَ يقرَأ القرآنَ كمثلِ التمرة لا ريحَ لها وطعمُها حلوٌ)) البخاري ومسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash'ariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Mfano wa Muumini ambaye anayesoma Qur-aan ni kama tunda la Utrujjah; harufu yake nzuri na ladha yake nzuri. Na mfano wa Muumini asiyesoma Qur-aan mfano wake kama tende zisizokuwa na harufu lakini zina ladha tamu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Utrujjah ni tunda linalofanana na ndimu yenye rangi ya chungwa inayokaribia rangi ya dhahabu. Tunda hilo linajulikana kama tufaha la ki-Ajemi, lina harufu nzuri.

6) Anayeisoma Qur-aan Hupata Thawabu Kwa Kila Herufi Anayoitamka

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ الله عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللَّهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا لَا أَقُولُ الم حَرْفٌ وَلَكِنْ أَلِفٌ حَرْفٌ وَلَامٌ حَرْفٌ وَمِيمٌ حَرْفٌ))
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayesoma herufi moja katika Kitabu cha Allaah atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja)) [At-Tirimidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (2910), Swahiyh Al-Jaami' (6469), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (3327)]

7) Anayeisoma Qur-aan Itakuwa Ni Shafaa’ah (Kiombezi) Siku Ya Qiyaamah

عن أبي أُمَامَةَ الْبَاهِلِي رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((اقْرَءُوا الْقُرْآنَ فَإِنَّهُ يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ شَفِيعًا لأَصْحَابِه)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Someni Qur-aan kwani itakuja siku ya Qiyaamah kuwa ni Shafaa’ah kwa swahibu yake [mwenye kuisoma]) [Muslim]

8) Qur-aan Humnyanyua Mtu Daraja Ya Juu Na Humdhalilisha Asiyeandamana Nayo

قَالَ عُمَرُ: أَمَا إِنَّ نَبِيَّكُمْ قَدْ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ يَرْفَعُ بِهَذَا الْكِتَابِ أَقْوَامًا، وَيَضَعُ بِهِ آخَرِينَ)) صحيح مسلم
‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Ama hakika Nabiy wenu amesema: ((Allaah Atawanyanyua baadhi ya watu kwa Kitabu hiki (Qur-aan) na Atawadhalilisha wengine kwa kitabu hiki)) [Muslim]

9) Mwenye Kuihifadhi Qur-aan Na Kuifanyia Kazi Atapandishwa Daraja Za Jannah

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((يُقَالُ لِصَاحِبِ الْقُرْآنِ: اقْرَأْ وَارْتَقِ وَرَتِّلْ، كَمَا كُنْتَ تُرَتِّلُ فِي الدُّنْيَا، فَإِنَّ مَنْزِلَكَ عِنْدَ آخِرِ آيَةٍ تَقْرَؤُهَا)) رواه الترمذي (2914) وقال: هذا حديث حسن صحيح، وصححه الألباني في صحيح الترمذي
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Huambiwa Swahibu wa Qur-aan: “Soma na panda juu (daraja za Jannah) na uisome kwa Tartiyl (ipasavyo kwa hukmu za Tajwiyd) kama ulivyokuwa ukiisoma ulipokuwa duniani, kwani makazi yako ni pale utakapofika katika Aayah ya mwisho utakayoisoma”)). [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy na Swahiyh Al-Jaami’]

Wengi kati ya ‘Ulamaa wamesema kuwa aliyekusudiwa kuwa ni “Swaahibul-Qur-aan” ni mwenye kuihifadhi na kuifanyia kazi wala si kuihifadhi bila ya kuifanyia kazi au kuisoma bila ya kuhifadhi.

Na Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu-Allaah) amesema: “Tambua kwamba iliyokusudiwa kuhusu “Swahibu wa Qur-aan” ni mwenye kuihifadhi moyoni… [Silsilah Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (5/284)

Na amesema Ibn Hajar Al-Haytamiy (Rahimahu-Allaah): “Khabari iliyotajwa ni makhsusi kwa anayeihifadhi moyoni si kwa anayeisoma tu…” [Al-Haytamiy, uk. 113]


10) Wanaosoma Na Kujifunza Qur-aan Huteremka Malaika Kuwazunguka Kwa Utulivu Na Rahmah

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللَّهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إِلَّا نَزَلَتْ عَلَيْهِمْ السَّكِينَةُ وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ وَحَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ وَذَكَرَهُمُ اللَّهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hawakusanyiki pamoja watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma Kitabu cha Allaah, na wanafundishana baina yao, ila huwateremkia utulivu na hufunikwa na Rahmah na Malaika huwazunguka na Allaah Anawataja mbele ya [Malaika] aliokuwa nao)) [Muslim Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]

Pia:

عن أُسَيْدَ بْنَ حُضَيْرٍ بَيْنَمَا هُوَ لَيْلَةً يَقْرَأُ فِي مِرْبَدِه، إِذْ جَالَتْ فَرَسُهُ، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أُخْرَى، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا. قَالَ أُسَيْدٌ: "فَخَشِيتُ أَنْ تَطَأَ يَحْيَى فَقُمْتُ إِلَيْهَا فَإِذَا مِثْلُ الظُّلَّةِ فَوْقَ رَأْسِي فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". قَالَ: "فَغَدَوْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ بَيْنَمَا أَنَا الْبَارِحَةَ مِنْ جَوْفِ اللَّيْلِ أَقْرَأُ فِي مِرْبَدِي إِذْ جَالَتْ فَرَسِي". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَانْصَرَفْتُ وَكَانَ يَحْيَى قَرِيبًا مِنْهَا خَشِيتُ أَنْ تَطَأَهُ, فَرَأَيْتُ مِثْلَ الظُّلَّةِ فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((تِلْكَ الْمَلَائِكَةُ كَانَتْ تَسْتَمِعُ لَكَ وَلَوْ قَرَأْتَ لَأَصْبَحَتْ يَرَاهَا النَّاسُ مَا تَسْتَتِرُ مِنْهُمْ))
Imepokelewa kutoka kwa Usayd bin Khudhwayr, kwamba alipokuwa akisoma akiwa katika mirbad yake, farasi wake alishtuka. Akasoma, akashtuka tena, akasoma akashtuka tena. Akasema Usayd: Nikaogopa asije kumkanyaga Yahyaa (mwanawe). Nikainuka kumwendea (farasi) nikaona kitu kama kivuli juu ya kichwa changu kama kina kandili kikipanda mbinguni hadi kikapotea. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asubuhi yake nikamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, jana usiku nilipokuwa katika mirbad yangu nikisoma Qur-aan, farasi wangu alishtuka! Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr)). Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr)). Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr)). Akasema niliondoka kwani Yahyaa alikuwa karibu naye, nikakhofu asimkanyage. Nikaona kama kivuli kikiwa na taa kinapanda juu hadi kikapotea. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hao ni Malaika walikuwa wakikusikiliza, lau ungeliendelea kusoma hadi asubuhi watu wangelikiona kisingelipotea)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

Mirbad – makazi ya mifugo ya farasi au ngamia.

11) Kuhifadhi Na Kujifunza Maana Ya Qur-aan Ni Bora Kuliko Mapambo Ya Dunia

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ قَالَ خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ فِي الصُّفَّةِ فَقَالَ: ((أَيُّكُمْ يُحِبُّ أَنْ يَغْدُوَ كُلَّ يَوْمٍ إِلَى بُطْحَانَ أَوْ إِلَى الْعَقِيقِ فَيَأْتِيَ مِنْهُ بِنَاقَتَيْنِ كَوْمَاوَيْنِ فِي غَيْرِ إِثْمٍ وَلَا قَطْعِ رَحِمٍ؟)) فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ نُحِبُّ ذَلِكَ قَالَ: ((أَفَلَا يَغْدُو أَحَدُكُمْ إِلَى الْمَسْجِدِ فَيَعْلَمُ أَوْ يَقْرَأُ آيَتَيْنِ مِنْ كِتَابِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ خَيْرٌ لَهُ مِنْ نَاقَتَيْنِ وَثَلَاثٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ ثَلَاثٍ وَأَرْبَعٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَرْبَعٍ وَمِنْ أَعْدَادِهِنَّ مِنْ الْإِبِلِ))
Imepokelewa toka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitujia wakati tulikuwa katika Swuffah akauliza: ((Kuna yeyote miongoni mwenu anayetaka kwenda soko la Butw-haan au [soko] la Al-'Aqiyq na akapata humo ngamia wawili wakubwa na walionona bila ya kutenda dhambi au kukata undugu?)) Tukajibu kwamba sote tunapenda kufanya na kupata hivyo. Kisha akasema: ((Basi aende mmoja wenu Masjid akajifunze au asome Aayah mbili katika Kitabu cha Allaah (‘Azza wa Jalla), pindi akifanya hivyo, basi ni bora kuliko ngamia wawili. Na Aayah tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na Aayah nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa Aayah kwa ngamia)) [Muslim, Abuu Daawuwd, Ahmad]

Swuffah: Sehemu katika Masjid Ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) waliyokuwa wakikaa Maswahaba ambao hali zao walikuwa ni masikini.

Butw-haan: Bonde lilioko kusini mwa mji wa Madiynah kuelekea upande wa Magharibi karibu na Jabali la Sal’. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitawadha katika bonde hilo siku ya vita vya Khandaq

Al-'Aqiyq: Bonde maarufu kabisa katika mji wa Madiynah au eneo la Al-Hijaaz yote. Liko umbali wa maili kilometa mia Kusini na linaelekea upande wa Mashariki. Linajulikana kuwa ni ‘Bonde lilibarikiwa’.

12) Mwenye Kuhifadhi Qur-aan Huvalishwa Taji Siku Ya Qiyaamah

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَجِيءُ الْقُرْآنُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُ: يَا رَبِّ حَلِّهِ، فَيُلْبَسُ تَاجَ الْكَرَامَةِ، ثُمَّ يَقُولُ: يَا رَبِّ زِدْهُ، فَيُلْبَسُ حُلَّةَ الْكَرَامَةِ، ثُمَّ يَقُولُ: يَا رَبِّ ارْضَ عَنْهُ، فَيَرْضَى عَنْهُ فَيُقَالُ لَهُ: اقْرَأْ وَارْقَ، وَتُزَادُ بِكُلِّ آيَةٍ حَسَنَةً))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Qur-aan itakuja siku ya Qiyaamah na itasema: “Ee Rabb, Mpambe” [Mwenye kuhifadhi Qur-aan]. Kisha atavalishwa taji la takrima. Kisha [Qur-aan] itasema: “Ee Rabb muongeze”. Kisha huyo mtu atavishwa nguo ya takrima. Kisha itasema: “Ee Rabb Ridhika naye”. Allaah, Ataridhika naye. Kisha ataambiwa: “Soma na panda”. Atapokea thawabu zaidi ya mema kwa kila Aayah [atakayosoma])) [At-Tirmidhy na Al-Haakim, ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (2915), Swahiyh At-Targhiyb (1425), Swahiyh Al-Jaami’ (8030)]

13) Mwenye Hifdh Na ‘Ilmu Ya Qur-aan Huwa Na Nuru Kaburini Na Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Atakuwa Shahidi Wake Siku Ya Qiyaamah

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضى الله عنهما قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَجْمَعُ بَيْنَ الرَّجُلَيْنِ مِنْ قَتْلَى أُحُدٍ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ ثُمَّ يَقُولُ : ((أَيُّهُمْ أَكْثَرُ أَخْذًا لِلْقُرْآنِ))‏ فَإِذَا أُشِيرَ لَهُ إِلَى أَحَدِهِمَا قَدَّمَهُ فِي اللَّحْدِ، وَقَالَ: ((أَنَا شَهِيدٌ عَلَى هَؤُلاَءِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ)).‏ وَأَمَرَ بِدَفْنِهِمْ فِي دِمَائِهِمْ، وَلَمْ يُغَسَّلُوا وَلَمْ يُصَلَّ عَلَيْهِمْ‏.‏ البخاري
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwakusanya watu wawili waliokufa katika vita vya Uhud katika nguo moja kisha aliuliza: ((Nani katika hao mwenye Qur-aan zaidi?)) Anapojulishwa mmoja kati ya hao, humtanguliza kaburini, na akasema: ((Mimi ni Shahidi wa hawa Siku ya Qiyaamah)) [Al-Bukhaariy]


Wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammadin wa ‘alaa aalihi wa Swahbihi wa sallam






 
Skip to main content



Search form​




Ukurasa Wa Kwanza /Siku Kumi Za Mwisho Za Ramadhwaan

Siku Kumi Za Mwisho Za Ramadhwaan​

Ramadhaan-Swawm

Siku Kumi Za Mwisho Za Ramadhwaan
Shaykh Swaalih Ibn Fawzaan Al-Fawzaan
Imetarjumiwa na: Ummu Iyyaad
www.alhidaaya.com



عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ : "كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا دَخَلَ الْعَشْرُ أَحْيَا اللَّيْلَ وَأَيْقَظَ أَهْلَهُ وَجَدَّ وَشَدَّ الْمِئْزَرَ" رواه البخاري (2024) ومسلم (1174)
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa pindi zilipoinga kumi za mwisho, akikesha usiku na akiamsha ahli zake na akijitahidi na kukaza shuka yake." [Al-Bukhaariy, Muslim]

Hadiyth hii ni uthibitisho kuwa siku kumi za mwisho za Ramadhwaan zina fadhila mahsusi na adhimu kuliko siku nyenginezo ambazo Muislamu inampasa aongeze utiifu na kutekeleza ‘ibaadah kama kuswali, kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kusoma Qur-aan.

‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amtuelezea hali ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inavyokuwa kama ni mfano bora kabisa kwa sifa nne zifuatazo:

1-Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikesha katika ‘ibaadah.

Alikuwa halali usiku. Kwa hiyo yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikesha usiku mzima kufanya ‘ibaadah na akihuisha nafsi yake kwa kutumia usiku wake kukaa macho na kuacha kulala. Hii ni kwa vile kulala usingizi ni mauti madogo. Maana ya "akihuisha (akikesha usiku)" ni kwamba yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitumia wakati huo katika hali ya Qiyaam (kusimama kuswali usiku) na kufanya ‘ibaadah ambazo zinatendwa kwa ajili ya Allaah, Rabb wa walimwengu. Inatupasa tukumbuke kuwa siku kumi za mwisho za Ramadhwaan ni chache zilizokadariwa kwa idadi.

Ama kuhusu ilivyonukuliwa katika Hadiyth ya 'Abdullaah Ibn ‘Amr, imekatazwa kukesha usiku mzima katika Swalaah, hii inahusu mtu anayefanya hivyo kwa mfululizo wa siku zote za mwaka.


2-Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiamsha ahli zake.

Ni wake zake waliotakasika ambao ni Mama wa Waumini, ili nao wanufaike katika ‘ibaadah hizo za kumdhukuru Allaah na ‘ibaadah nyenginezo katika siku hizo zenye baraka nyingi.


3-Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya bidii.

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijizuia na akijitahidi sana katika ‘ibaadah, akiongeza ‘amali njema zaidi kuliko alivyokuwa akifanya siku ishirini za mwanzo (wa Ramadhwaan). Akifanya hivi kwa sababu Laylatul-Qadr inatokea katika usiku mmoja wa siku hizo kumi.


4-Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikaza shuka yake.

Alikuwa akijihimiza na kufanya bidii kubwa katika ‘ibaadah nzito. Inasemekeana vile vile Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijitenga na wake zake. Hii ni kauli iliyo sahihi zaidi kwa vile inakubaliana na ilivyotajwa kabla katika Hadiyth ya Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikunja kitanda chake na akijitenga na wake zake" [Latwaaif-ul-Ma'aarif, Uk. 219]

Vile vile Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya I'tikaaf katika siku za mwisho za Ramadhwaan na watu wenye kuwa katika hali ya I'itikaaf hujizuia kujamii na wake zao.

Kwa hiyo enyi ndugu Waislamu, jitahidini kujizoesha na kuwa katika sifa na khulka hizi. Na tekelezeni Swalaah za usiku pamoja na Imaam hata baada ya kuswali Taraawiyh ili jitihada zenu katika siku hizi kumi za mwisho zipindukie siku ishirini za mwanzo na ili mpate kufaulu kupata sifa ya "kuuhuisha usiku kwa ’ibaadah" kwa kuswali.

Na ni lazima muwe na subira katika utiifu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na ‘ibaadah za usiku kwani hakika Tahajjud ni ngumu lakini thawabu zake ni kubwa sana. Naapa kwa Allaah, ni fursa kubwa katika maisha ya Muislamu na vile vile ni faida kubwa kuitumia fursa hii kwa yule aliyejaaliwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kwani mwana Aadam hawezi kujua kama ataweza kuchuma tena thawabu nyingi kama hizi, ambazo zitamfaa katika maisha yake ya dunia na ya Aakhirah.

Salafus-Swaalih (Wema waliotangulia) wa Ummah huu walikuwa wakijitahidi katika ‘ibaadah za masiku haya kwa kuzirefusha Swalaah za usiku. As-Swaa'ib bin Yaziyd amesema, "'Umar bin Al-Khattwaab alimuamrisha Ubay bin Ka'ab na Tamiym Ad-Daariy kuimamisha watu katika Swalaah kwa Raka'ah kumi na moja. Imaam alikuwa akisoma Aayah mia moja hadi ilibidi tuegemee mkongojo kwa sababu ya kisimamo kirefu, na tulikuwa hatupumziki hadi inapoanza kuingia Alfajiri". [Al-Muwattwa, Mjalada 1, Uk. 154]

'Abdulllaah Bin Abiy Bakr amesema "Nimemsikia baba yangu akisema, wakati wa Ramadhwaan, tulikuwa tukichelewa kumaliza Swalaah za usiku hata tukiwahimiza watumishi kutuwekea suhuwur (daku) kwa kuogopa Alfajiri isitufikie" [Muwattwa ya Imaam Maalik, Mjalada 1, Ukurasa 156]

Nafsi ya Muumini inapambana na jitihada mbili katika Ramadhwaan; Jitihada ya mchana kwa swiyaam na jitihada ya usiku kwa Qiyaam. Kwa hiyo yeyote atakayejumuisha jitihada mbili hizi na akatimiza haki zake, basi yeye atakuwa miongoni mwa wenye subira kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿١٠﴾
Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu. [Az-Zumar: 10]

Siku kumi hizi ni za mwisho katika mwezi mtukufu huu, na ‘amali za Muislamu zinazohesabika zaidi ni zile za mwisho, kwa sababu huenda akafaulu kukutana na usiku wa Laylatul-Qadr wakati akiwa amesimama katika Swalaah ikawa ni fursa nzuri ya kufutiwa madhambi yake yote na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

Ni wajibu wa kila mtu kuamsha na kuhimiza na kushurutisha familia yake kutekeleza ‘ibaadah khasa nyakati hizi tukufu, kwani hakuna atakayedharau kufanya hivi ila yule aliyenyimwa fadhila hizi. Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba wakati wengine wako katika ‘ibaadah khasa za masiku haya kumi, wengine wanatumia wakati wao katika vikao vya maasi. Hakika hii ni khasara kubwa.

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuhifadhi na Atuhidi.

Kwa hiyo Muislamu atakayejishughulisha na ‘ibaadah katika siku kumi hizi za mwisho atakuwa amejiingiza katika milango ya kuchuma mema yaliyobakia katika mwezi huu mtukufu. Ni khasara kwa mtu aliyeanza mwezi wa Ramadhwaan kusimama kwa nguvu kuswali, kusoma Qur-aan na dhikru-Allaah kisha siku za mwisho akawa na mzito na mvivu katika kufanya ‘ibaadah na hali hizi siku za mwisho ndio siku muhimu na zenye uzito wa thawabu za kusimama kuswali na kadhaalika kuliko zote. Hivyo kila mmoja inampasa aongeze bidii zaidi na kujitahidi kwa kadiri awezavyo kuongeza ‘ibaadah katika kumalizia mwezi mtukufu huu. Na kukumbuka kuwa ‘amali za mtu zinahesabika zile za mwisho.

Du’aa ya Laylatul-Qadr:

Katika siku hizi kumi za mwisho ni vizuri sana kuisoma du'aa hii kila mara khasa katika usiku wa Laylatul-Qadr kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

عَنْ عَائِشَةَ , أَنَّهَا قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ أَرَأَيْتَ إِنْ وَافَقْتُ لَيْلَةَ الْقَدْرِ مَا أَدْعُو؟ , قَالَ : ((تَقُولِينَ : اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي)) ابن ماجه و صححه الألباني
Imepekelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: “Ee Rasuli wa Allaah! Je nitakapojaaliwa kufikia Laylatul-Qadr niombe nini?" Akasema, ((Sema: Allaahumma Innaka 'Afuwwun Tuhibbul-'Afwa fa'fu 'anniy - Ee Allaah Hakika Wewe Ndiye Mwenye Kusamehe Unapenda Kusamehe basi Nisamehe)) [Ibn Maajah na kaisahihisha Al-Albaaniy]











 
Tuichambue suratul al ma'un,,kuna masomo makubwa sana hapa


107:1 - Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?

107:2 - Huyo ndiye anaye msukuma yatima,

107:3 - Wala hahimizi kumlisha masikini.

107:4 - Basi, ole wao wanao sali,

107:5 - Ambao wanapuuza Sala zao;

107:6 - Ambao wanajionyesha,

107:7 - Nao huku wanazuia msaada.


Aya ya Kwanza inamzungumzia yule mtu ambaye haamini kuhusu malipo ya akhera au kwa maana nyingine haamini kwamba kuna hesabu na malipo kwa mtenda mema na muovu

Aya ya pili inazungumzia moja ya sifa za mtu huyu ni kutomwangalia yatima, hana huruma naye kabisa, hamjali katika shida zake na ustawi wake

Lakini lau mtu huyu angeamini akhera hakika angejihumiza kumjali sana yatima, Katika mfumo wa hadith Mtume (s. a. w) anasema mwenye Kumsaidia yatima ambaye ni ndugu anapata ujira mara mbili, kwanza kama sadaka lakini pili kwa kuunganisha undugu.

Ndugu zangu katika imani tujihimize sana kuwajali mayatima iwe miongoni mwa ndugu zetu au nje ya hapo.

Aya ya tatu bado inaelezea sifa za mtu huyo ambaye anakadhibisha malipo,,, wala hahimizi kulisha masikini, kwanza yeye mwenyewe halishi wala kusaidia maskini lakini vile vile hahimizi wenzake kulisha au kusaidia maskini.

Ndugu zangu nawahimiza kuwasaidia maskini na kuwajali sana kwani huu ni mtihani toka kwa Allah azza wa jalla tutakuja kuulizwa siku moja juu ya watu hawa.

Sura katika aya ya nne inawageukia wale watu wanao swali,kwamba watapata adhabu kali,,,je kwanini?

Aya ya tano inafafanua kwamba Wanao puuzia swala zao
Ndugu zangu hapa kuna sifa kadhaa zimetajwa kutokana na hadithi pamoja na uelewa wa watu wema wenye elimu

Kwanza wale ambao haswali kwa wakati, yani kuna watu ambao wao mda wa swala ukifika basi wanaendelea kufanya mambo yao kisha baadae huko ndio wanaenda kuswali, unakuta adhuhur imeisha yeye ndio anaenda kuiswali wakati wa al Siri, kama sifa hiyo unayo basi aya inakuhusu.
Sifa nyingine ni kutokuwa na utulivu ndani ya swala, utakuta mtu huyu ima awe ana rukuu au kwenye sijida hana utulivu kabisa,kainama kainuka fasta fasta Kana kwamba anakimbizwa,,, Siku moja Mtume swalallahu alayhi wa sallam alikuwa amekaa msikitini na maswahaba wake, kisha akaingia mtu mmoja akaswali bila kutulia katika kila hatua, alipo maliza Mtume akamwambia hujaswali na swali tena, yule aliswali vile vile ndani ya mara tatu, kisha akamwambia mtume hakika sina kingine ninacho kijua zaidi ya hivi ninavyoswali. Hapo Mtume akamwelekeza kila hatua atulie Kidogo,akiwa ktk rukuu ajitulize ndani, akisimama itidali na sujudi hivyo hivyo

Katika hadith nyingine Mtume amenukukiwa akisema msiswali swala yenu kama vile kunguru anavyodonoa mzoga.

Sifa nyingine ya kupuuza swala ni kutokuwa na hushui ndani yake, yaani uko pale kwa kiwiliwili lkn mawazo yako yako mbali kabisa, yaani upo katika swala lkn huku unauza na kununua,,, ingawa kibinadamu ni ngumu sana kutowaza jambo lengine lkn jitahidi usije kukumbwa na mawazo mpaka ukapotea kabisa ndani ya swala, jitahidi kuweka mawazo yako yote ndani ya swala.

Sifa nyingine ya kupuuza swala ni kuswali kwa kujionyesha, kuna watu wanaswali mathalani ndani ya mwezi huu wa ramadhani ili waonekane wanaswali na watu lkn hawaswali kama ibada kwa ajili ya Allah, ikiwa ndani ya nafsi yako unajijua kuwa unaswali ili uonekane uswali basi tambua huna swala, kwani Allah haikubali amali /kitendo chochote cha ibada ambacho hakijafanywa kwa ajili yake.

Kwahiyo ndugu zangu Katika imani kama tuna sifa hizi basi tujirekebishe.

Aya ya sita inazungumzia wale watu ambao wanafanya mambo mbali mbali ya kiibada au amali kwa ajili ya kujionyesha mbele za watu, hatoi sadaka basi mpaka alete waandishi wa habari, haswali mpaka watu wamwone kuwa anaswali, halishi maskini wala mayatima basi mpaka ahadithie au hamsaidii mtu mpaka amtangaze, hakika watu hawa wamepata hasara na juhudi zao zimeenda bure kwani hawatalipwa au hawatapata thawabu kwa matendo yao haya.

Na aya ya saba imezungumzia watu hawa ambao wanazuia misaada midogo midogo, Amekuja ndugu yako anashida anataka msaada unacho lkn unashundwa kumsaidia, amekuja jirani anakuaziima jembe, fagio au shoka unamnyima bila sababu ya msingi na mango mengine kama hayo.

Allah atuongoze inshallah.
 
Skip to main content



Search form​




Ukurasa Wa Kwanza /Nasiha 40 Za Ramadhwaan – Zitekeleze Ufaidike na Mwezi Mtukufu

Nasiha 40 Za Ramadhwaan – Zitekeleze Ufaidike na Mwezi Mtukufu​

Ramadhaan-Swawm

Nasiha 40 Za Ramadhwaan – Zitekeleze Ufaidike na Mwezi Mtukufu

Alhidaaya.com


1-Anza kwa kuzingatia mwezi huu mtukufu uwe wa kujihesabu, kutenda amali nyingi na kujirekebisha hali yako na uhusiano wako na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) uwe bora zaidi:

2- Kumbuka kwamba huu mwezi ni mgeni ambaye amekutembelea kisha ataondoka, hivyo mpokee mgeni wako na mkirimu kwa mazuri yote anayostahiki.

3-Tahadhari na kutokufunga bila ya sababu au udhuru wowote, kwani kufanya hivyo, Swawm yako haitolipika hata ukifunga mwaka mzima.

4-Swali kwa wakati wake, usiache Swalah ikakupita. Na jua kuwa ukiwa huswali Ramadhwaan huna Swawm kwa mujibu wa fatw za Maulamaa wengi.

5-Soma sana Qur-aan kadiri uwezavyo kwani ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan. Kamilisha msahafu mzima japo mara moja, ukishindwa basi hata nusu yake, robo yake.

6-Zidisha ibada za Sunnah, kama Sunnah zilizo Muakkadah (zilizosisitizwa) na zile Ghayri Muakkadah (zisizosisitizwa). Tazama ratiba katika kiungo kifuatacho:

Ratiba Ya Swalah Za Sunnah Zilizosisitizwa Na Zisizosisitizwa

7-Chukua fursa kuomba du'aa sana kila mara nyakati za kukubaliwa du'aa, khaswa ukiwa bado katika Swawm. Tumia wakati wa baina ya adhana na iqaamah kuomba du'aa na haja zako kwani ni wakati wa kukubaliwa du'aa. Vile vile nyakati za thuluthi ya mwisho ya usiku.

8-Iborishe Swalah yako kwa kuiswali ipasavyo na kuzidisha khushuu (unyenyekevu).

9-Usiache kuswali Taraawiyh pamoja na jama‘ah, usiondoke hadi Imaam amalize upate thawabu za Qiyaamul-Layl.

10-Tahadhari na kufanya israaf ya mali, chakula na neema nyinginezo, kwani israaf ni mbaya na itakuondoshea neema ulizojaaliwa.

11- Tumia wakati wako vizuri na zingatia kwamba umri wako unazidi kupunguka.

12-Mwezi huu ni wa ibada na sio kula, kulala na kufanya ya upuuzi.

13-Zoesha ulimi wako uwe umerutubika kwa kumtaja Mola wako, usiwe miongoni mwa wasiomkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ila kidogo tu.

14-Chukua fursa kufanya da‘awah. Amrisha mema na kataza maovu, kwani yule unayemuongoza atakapotekeleza mema, utazibeba nawe thawabu zake pia. Tuma ujumbe wa dini kwa wenzako. Chapisha idadi nyingi ya makala zenye mafunzo ya dini, chapisha du'aa ugawe misikitini, vyuoni, majumbani. Unaweza kupata makala na du'aa mbali mbali katika Alhidaaya.com Pia kama una uwezo zaidi rekodi mawaidha yaliyomo ndani ya tovuti na wagawie wenzako upate ujira zaidi. Gawa bure na usiuze, kwani si ya kuuzwa.

15-Fanya kila aina ya wema uwezavyo, patanisha waliokhasimiana, msaidie mwenye haja na muokoe mwenye shida.

16-Wakumbuke wazazi, ndugu, jamaa na marafiki katika du'aa zako kwani kuwaombea wao bila ya wao kujua Malaika hukuombea na wewe vile vile.

17-Wasiliana na ndugu, jamaa kwani ni jambo lililosisitizwa sana na lenye kukuongeza umri, kheri na baraka nyingi. Walio mbali na wewe wasiliana nao kwa simu.

18-Unapohisi njaa, wafikirie masikini wasio na uwezo wa kula, na utambue kuwa uko katika neema ya Mola wako.

19-Muombe msamaha uliyemdhulumu kabla hajalipwa mema yako.

20-Mfuturishe aliyefunga upate thawabu zake juu ya thawabu zako.

21-Omba maghfirah na msamaha kwa Mola wako, kwani tambua kwamba Yeye ni Mwingi wa Msamaha na Mwingi wa Rahma.

22-Ikiwa umetenda maasi kisha Akakusitiri Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), tambua kuwa hiyo ni onyo utubie na weka azma kutokurudia tena.

23- elimu ya dini yako kwa kujifunza tafsiyr ya Qur-aan, Hadiyth, Fiqhi n.k. upate kuongeza taqwa.

24-Sikiiza mawaidha japo moja kwa siku kwani kusikiliza kunaleta taathira kubwa ya kuongeza Iymaan na Taqwa.

25-Jiepushe na marafiki waovu na vikao vyao na ungamana na marafiki wema na vikao vya kheri.

26-Usipoteze muda wako kutazama televisheni vipindi visivyokupa faida na dini yako, bali tumia wakati wako kwa yatakayokuongezea elimu na Taqwa.

27-Usiharibu Swawm yako kwa kunena ya upuuzi, au Ghiybah (kusengenya), au kubishana au kupandisha sauti. Jizuie unapokuwa na hamaki.

28-Fika msikitini mapema zaidi, kwani hivyo ni dalili ya hamu na mapenzi ya ibada na kuwa karibu na Mola wako.

29-Waamrishe na kuwafunza mema ya dini yao walio katika majukumu yako; mke, mume, watoto, ndugu, jamaa n.k. kwani wako karibu yako zaidi na kukutii.

30-Usijaze tumbo sana katika suhuur (daku) kwani itakufanya uwe mvivu na ushindwe kukaa macho nyakati za asubuhi na mchana na ushindwe kufanya ibada vizuri na kusoma sana Qur-aan.

31-Usijaze tumbo sana katika iftwaar (kufuturu) kwani itakushinda kusimama Qiyaamul-Layl au kuzingatia Aayah za Qur-aan zinaposomwa na Imaam.

32-Punguza kwenda madukani/sokoni khaswa kumi la mwisho kwani utakosa kheri na thawabu nyingi zilizomo katika masiku hayo ya thamani kubwa.

33-Tilia hima kubwa kuswali Qiyaamul-Layl kumi la mwisho upate Laylatul-Qadr, usiku ambao ibada yake ni bora kuliko miezi elfu.

34-Jitahidi ufanye I'tikaaf msikitini katika kumi la mwisho japo siku chache, upate fadhila zake na uchume mema mengi pamoja na kupata Laylatul-Qadr.

35-Tambua kwamba siku ya 'Iyd ni siku ya kumshukuru Mola wako na sio siku ya kutenda yale uliyojizuia ya maovu katika Ramadhwaan.

36-Siku ya 'Iyd , wafanyie wema wazazi, watembelee ndugu, jamaa na marafiki kuboresha uhusiano wako nao.

37-Usiache kutoa Zakatul-Fitwr - wakumbuke maskini, yatima na wanaohitaji na wasaidie na kuwagawia chochote wabakie katika furaha.

38-Tamka Takbiyrah siku ya 'Iyd kwa sauti unapokwenda msikitini ili kuwakumbusha wengine wanaokwenda au kufuatana nawe ili nawe waweze kupiga Takbiyrah hizo.

39-Weka azma baada ya Ramadhwaan kujiendeleza katika hali ya ibada uliyokuwa nayo katika Ramadhwaan, ukifanya hivyo itakuwa ni dalili ya kukubaliwa Swawm yako.

40- Funga Sita Shawwaal upate thawabu za Swawm ya mwaka mzima.










 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…