Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Ramadhani Kingai sasa ndio DCI wetu!
Kama alipitia somo la GPO(General Police Orders) kule Moshi CCP(Chuo Cha Polisi) , basi ni wazi kuwa hakufaulu lakini akaingia kazini hivyo hivyo.
Nasema hivi kutokana na track record yake , hasa katika kesi iliyomuumbua kitaaluma, kesi ya Ugaidi wa Mbowe.
Tuna mshukuru Mama Samia kuwa kesi ile iliwapa waandishi wa habari uhuru unaohitajika.
Na katika uhuru ule waandishi wa habari waliweza kubaini na kuandika mapungufu makubwa kitaaluma yana yo mkabili ndugu yetu Ramadhani Kingai.
Pengine kuna sababu nyingine nje ya hizi tunazo ziona zilizo sababisha Ramadhani Kingai kupandishwa madaraka na kuwa DCI.
Nchi ii huwezi jua.
Sasa kwa mapungufu yale tuliyoyaona yanaweza kuambukiza jeshi zima la Polisi na likawa watu wanaofanya kazi bila weledi wala taaluma.
Idara ya DCI ambayo ndiyo inafanya criminal investigations zote nchini lazima iwe na weledi wa kitaaluma.
Kwa kuanzia namshauri DCI mpya asome masomo ya ziada ya GPO.