Ramadhani ya 2022 itakuwa ngumu, vyakula vinapanda bei na raia tuko kimya

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Muda kama huu Hayati Magufuli angeshakemea vitu kupanda bei. Leo hii mafuta ya kula lita 10 Tsh. 63, 000 huku lita 20 ikiwa ni Tsh. 117,000.

Wauza mihogo ya kukaanga biashara imewashinda sababu ya mafuta kupanda sana na sio kwamba hakuna wateja.

Tambi na ngano vimepanda bei mapema. Je, mwezi wenyewe wa Ramadhani ukianza hali itakuwaje? Kinachonishangaza hakuna chochote kinachosemwa, kuko kimya hakuna matamko ila wenzetu wa stand wenyewe mafuta yakipanda siku mbili tu nyingi washaanza kuleta migomo.
 
Watu wa mwendazake acheni ramli chonganishi
 
Tafuta hela acha kulialia ramazani ndio kitu gani katika maisha haya..mbona kuna kwa rezima na maisha yanaendelea.

Umasikini + ujinga ni janga la dunia

#MaendeleoHayanaChama
 
Ramadhan inakuwaje ngumu wakati Waislam wanakula mlo mmoja as opposed to other times wanapokula milo 3+?
Actually milo ni miwili, lakini ugumu utakuwepo ikiwa mfumuko wa bei umeambatana na ramadhani, lakini kama si hivyo basi hakuna tofauti yoyote na nyakati zingine.
 
Tafuta hela acha kulialia ramazani ndio kitu gani katika maisha haya..mbona kuna kwa rezima na maisha yanaendelea.

Umasikini + ujinga ni janga la dunia

#MaendeleoHayanaChama
Sijisemei Mimi
Mimi NI mkristo kwanza
Cha pili Nina kazi yenye kipato Cha wastani kunifanya nisihisi mabadiliko ya Bei
Pia sio mnunuaji Sana wa vitu hivyo mafuta,ngano kwa maana Sina familia

Isipokuwa thread ninasemea watu wa chini marafiki zangu mama zangu wafanyabiashara wadogo nimekuta wanalalamika Sana NI muhimu niwasemee tunahoji tu mazao NI yetu,Nchi NI yetu,watu NI wetu.
 
Muda kama huu Hayati Magufuli angeshakemea vitu kupanda bei. Leo hii mafuta ya kula lita 10 Tsh. 63, 000 huku lita 20 ikiwa ni Tsh. 117,000.

Wauza mihogo ya kukaanga biashara imewashinda sababu ya mafuta kupanda sana na sio kwamba hakuna wateja.

Tambi na ngano vimepanda bei mapema. Je, mwezi wenyewe wa Ramadhani ukianza hali itakuwaje? Kinachonishangaza hakuna chochote kinachosemwa, kuko kimya hakuna matamko ila wenzetu wa stand wenyewe mafuta yakipanda siku mbili tu nyingi washaanza kuleta migomo.
Kila siku hayati hayati, kwa nini usitoe maoni yako usikike ? Kwani ukitoa maoni bila kumtaja Magufuli ambaye ameshakufa ndio unahisi hautasikika???

Kama Kuna mafunzo umeyapata kupitia yeye basi nawe tekeleza kwa matendo mnaishi kujilalamisha kila siku kisa muonekane wanyonge?

Wewe toa hoja yako na suggestions zako usikike.
 
Natamani niseme kupiga plan B ya makande na uji, lakin sijui utaratibu wa vyakula vinavohitajika mwez mtukufu, so ntabaki mtazamaji tu. (Na nkialikwa kufuturu sivungi!)
 
Yaani unapinguza idadi ya milo na anasa za kula katika funga halafu unalalamika?
Mbona watu wako Kwaresma na hakuna tofauti?
 
Muda kama huu Hayati Magufuli angeshakemea vitu kupanda bei. Leo hii mafuta ya kula lita 10 Tsh. 63, 000 huku lita 20 ikiwa ni Tsh. 117,000.

Wauza mihogo ya kukaanga biashara imewashinda sababu ya mafuta kupanda sana na sio kwamba hakuna wateja.

Tambi na ngano vimepanda bei mapema. Je, mwezi wenyewe wa Ramadhani ukianza hali itakuwaje? Kinachonishangaza hakuna chochote kinachosemwa, kuko kimya hakuna matamko ila wenzetu wa stand wenyewe mafuta yakipanda siku mbili tu nyingi washaanza kuleta migomo.
😁😁😁😁 Kupanda au kushika kwa bei za vitu hakutokani na kukemea au kutoa matamko ,haaaa.

Sababu za vyakula kupanda ni mafuta,demand kubwa vs supply
 
Back
Top Bottom