Ramani mpya ya ECOWAS baada ya Mali, Niger na Burkina faso kujitoa

Ramani mpya ya ECOWAS baada ya Mali, Niger na Burkina faso kujitoa

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Sasa ni rasmi kuwa Mali, Niger na Burkina Faso si wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu nchi hizo zitoe taarifa rasmi ya kujitoa kwao. Kwa taratibu za ECOWAS, uanachama hukoma takribani mwaka mmoja baada ya nchi mwanachama kutoa taarifa ya kujitoa.

Kujitoa kwa nchi hizo kunasababisha ECOWAS kupoteza asilimia 53 ya eneo lake hasa kutokana na kuzipoteza Mali na Niger ambazo kila mmoja ina eneo kubwa kuliko Tanzania.

Kwa sasa nchi zilizobakia ECOWAS ni Nigeria, Ghana, Ivory Coast, Guinea Bissau, Senegal, Gambia, Cape Verde, Benin, Togo,Liberia, Sierra Leone pamoja na Guinea.

Soma: Burkina Faso, Mali na Niger zajiondoa rasmi Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS)

Ramani mpya ya ECOWAS ni kama inavyoonekana hapa chini
20250127_175800.jpg
 
Afrika inahitaji akina Traore kila kona ili kujinasua dhidi ya mikono dhalimu ya wale wanaoinyonya na kuikandamiza Afrika kupitia rasilima na kiinimacho cha watawala.
 
Back
Top Bottom