nami nilitaka kumwambia hivyo hivyokama zile za bendela ya chadema
kama zile za bendela ya chadema
no research,no right to speak
kama zile za bendela ya chadema
asante sana mwana. Umewazidi wote ambao walitoa majibu ya mtaani! Mimi kwangu ni Mbagala, nashukuru and I am going to do a simple research on it. Asante sana. I wsill come back to you when I am through!
tupe majibu ya utafiti wako Mkuu!
shukrani mzeeSikuona sababu ya kuidharau thread hii nikajaribu kupata maelezo ya nini hasa asili ya jina hili nilifika Mbagala Rangi Tatu nikamuona Mzee mmoja nikajifanya ni mwenyeji wa eneo lile ili asije akaniona kwanini namuuliza kuhusu Mbagala ili hali natoka mbali sana, nikamuuliza hivi rangi tatu hapa Mbagala zilikuwa wapi???
Aliniambia kuwa usidhani rangi hizo zilikuwa zimepakwa kwenye kuta la hasha. Akaanza kunipa jibu.
Eneo hili lilikaliwa na Wamakonde, kama unavyojua wamakonde wanautamaduni wa kujichanja nyuso zao. Kulikuwa na aina tatu zilizowatofautisha hawa wamakonde. Kuna Wamakonde ambao asili yao ni Mtwara uchanjaji wao wa chale ulitofautiana na wale ambao asili yao ni kutoka Msumbiji ambao nao walikuwa ni wa aina mbili tofauti. Kuna Wamakonde ambao asili yao ni Msumbiji na wale ambao Mreno alijaribu kuiga uchanjaji akaleta style ya aina yake tofauti kidogo na Wamakonde asilia wa Msumbiji. Kwa hiyo utakuta kutoka Msumbiji kulikuwa na Wamakonde aina mbili kwa chale zao na wale ambao asili yao ni Mtwara walipokuja hapa Mbagala wakawa ni kabila moja lenye matawi matatu, wakaita Mbagala Rangi Tatu.
View attachment 85742
View attachment 85751
View attachment 85752