Huwa nikiwaambia watu kwamba wakristo wengi hasa Wakatoliki na Kanisa lao wamehusika sana katika kumhujumu mwafrika huwa naonekana nina chuki za kidini. Lakini siku mwafrika anapata hata kufahamu robo tu ya ukweli nadhani anaweza kuchukia kabisa dini iliyoletwa na wakoloni.
Iko hivi, sehemu kubwa ya historia ya Kanisa la kwanza ilitunzwa na Roma Mashariki (Constantinople) ambao wao ndiyo walikuja kuanzisha dhehebu la kiorthodoksi. Wao sanamu zao zote za kale hasa lile la Yesu na Mama yake(The Black Madonna) na michoro yake (Iconography) ilikuwa inaonesha Yesu akiwa akiwa ni mtu mwenye rangi nyeusi.
Dr. Yossef Ben-Jochannan anasema mbalina ushahidi huu kuwepo, lakini Kanisa Katoliki likawaaminisha wafuasi wake kwamba ilishuka nyota toka mbinguni ikabadilisha rangi ya sanamu la Yesu na Mama yake (The Black Madonna) pamoja na michori mingine. Unaambiwa mara baada ya Wakatoliki kufika nchini India walikuta Kanisa aliloanzisha Mtume Tomaso, na kuona michoro yake ikionesha Yesu akiwa ni mweusi. Ikatolewa amri kwamba iondolewe haraka sana.
Ukifuatilia sana historia utafahamu kwamba huu mchezo mchafu wa kutaka kufuta historia na kuipotosha, Kanisa liliurithi kutoka kwa Roma ya kale, ile ya kipagani (Ancient Rome). Wao walikuwa wakiona kitu kimewashinda, kama wasipokiua basi watakifuta au kukificha kabisa.
Kaisari Vespasian alivyoiangusha Metsada mwaka 71 A.D aliua maelfu ya Wayahudi na kuwafukuaza kwenye ardhi yao na kuamua kuibadilisha jina kutoka Uyahudi (Judea) hadi Ufilisti. Neno Palestine limetokana na neno Ufilisti ambalo Kaisari wa Roma ili kuhakikisha kwamba Wayahudi anawakomesha na kufuta historia yao akaamua kuwapa maaduia zao Wafilisti.
NB: Huu utamaduni mbali na kufanywa na Wakatoliki, umefanywa sana na Wakristo wakizungu kutoka kwenye madhebu mengi sana ili kufanikisha ukoloni na ubaguzi. Hebu angalia wale wanaojiita Walokole wa Marekani walivyofuta historia ya wahindi wekundu (Chereokee Indians) kule Marekani. Yaani kuna baadhi ya mambo ukiyafahamu unaweza kuishia kuwachukia hawa wanaojiita wafia dini.....