Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Mkuu umenena vema sana.Mpangilio wa rangi za viti na rangi zenyewe umeleta giza ndani ya uwanja wa Mkapa.
Hata Mpira unapooneshwa na kamera kuelekezwa kwenye maeneo ya vitu visivyo na watu au watu wachache unaona kabisa ule mvuto wa uwanja umepungua kabisa.
Inawezekana lengo la kuweka rangi za bendera yetu ya Taifa uwanjani lilikuwa jema, lakini sidhani mpangilio wake na hizo rangi zenyewe zilifaa kuwepo uwanjani kwa Mkapa.
Ni kweli mkuu ukitaka kujua huko kuna uozo ukimuangalia tu yule mwanasheria wa jamhuri kwenye kesi ya lisu unaona wasomi wetu wanashida.Hiyo ndiyo reflection ya akili za wasomi wa Tanzania.Kama akili zina giza vitu vingi ,miradi mikubwa utaona giza tu.
Nikiangalia Zanzibar naona huko kuna watu wenye akili.
Nikiangalia Rwanda naona wenye akili pia.Tazama tu uwanja wao utajua.
Nikiangalia Kenya naona watu wenye akili,ndio maana ya kusoma haswaa.
Nahisi hapa kwetu kuna matatizo mengi sana maana nikiona hiyo Mkapa eti imetumia bilioni 30 kukarabati,halafu hali yenyewe ndio hiyo,nabaki tu kushangaa hiki kizazi
Hawa watu wanaamka na kufanya maamuzi tu ya kutuhadaa ili waonekane wazalendo zaidi.
Uko sahihi kabisa, wamepaka hayo marangi Sheikh Amri Abeid, Arusha na nadhani Dodoma, uwanja haupati muonekano mzuri kwa hayo marangi, hawajashtuka wanaendelea na kosa hilo hilo. Siasa nyingi kuliko weledi.
Naona dalili huu uwanja wa Mkapa unaenda kufa na kupotea kabisa.