Rapa rick ross anusurika ajali kufuati kugonga gari baada ya kusikia milio ya risasi florida.

Rapa rick ross anusurika ajali kufuati kugonga gari baada ya kusikia milio ya risasi florida.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Rapa mashuhuri nchini Marekani Rick Ross anusurika kuumia baada ya kuigonga katika ukuta wa jengo moja gari yake ya kifahari aina ya Rolls-Royce.

Maafisa katika mji wa Fort Lauderdale huko Florida wamesema rapa huyo pamoja na mtu aliyekuwa naye kwenye gari hilo mbunifu Shateria L Moragne-el, wameripoti kusikia milio kadhaa ya risasi zilizoelekezwa upande wao karibu na walipokuwa wakipita majira ya 11 alfajiri.

Rick Ross ambaye ni muasisi wa Maybach Music Group alipoteza mwelekeo na kuyumba baada ya kusikia risasi hizo ndipo alipopata ajali hiyo.

Hakuna aliyejeruhiwa kati yao na pia hakuna risasi iliyopiga gari hilo la kifahari.

Ross alikuwa akitoka kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo sasa ametimiza miaka 37.
 
Back
Top Bottom