Raphia Ally Kimaro, Mjasiriamali na Mwezeshaji wa semina za ujasiriamali kwa wanawake na vijana, amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuwania Ubunge wa Viti Maalum vya Wanawake mkoa wa Dodoma.
Mbali na kuwa mbunifu wa mfumo wa uratibu wa biashara kwa wajasiriamali, Raphia pia ni mhitimu wa Shule ya Uongozi kwa wanawake (Uongozi Institute) na mjumbe Mwanzilishi wa jumuiya ya wana taaluma ya Masoko Tanzania.