RAS Geita na DC Chato wametembelea banda la Chato

RAS Geita na DC Chato wametembelea banda la Chato

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
RAS GEITA NA DC CHATO WATEMBELEA BANDA LA CHATO

Na. Richard Bagolele-Nyamhongolo Mwanza

Katibu Tawala Mkoa wa Geita Prof.Godius Walter Kahyarara na Mkuu wa Wilaya ya Chato Martha Mkupasi kwa nyakati tofauti leo wametembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwenye maonesho ya Nanenane 2022 Kanda ya Ziwa Magharibi yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo Mwanza.

Katibu Tawala Mkoa amevipongeza vikundi mbalimbali vilivyopeleka bidhaa za maonesho ambapo ameshauri vikundi hivyo kuzalisha bidhaa zenye ushindani katika masoko ya ndani na nje ya mkoa au nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chato amevishauri vikundi hivyo kuongeza ubunifu wa kuongeza mitaji ikiwemo ile ya sekta binafsi pasipo kutegemea pekee mikopo inayotolewa na serikali kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani.

Kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane 2022 ni "Ajenda 10/30: Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".
IMG-20220807-WA0033.jpg
IMG-20220807-WA0034.jpg
IMG-20220807-WA0035.jpg
 
Back
Top Bottom