Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
NATAFUTA NA NATAFITI HISTORIA YA RASHID ALI MELI NA SAFARI YA NYERERE UNO 1955
Tafadhali nitafutie watoto au ndugu wa Rashid Ali Meli hapo Zanzibar.
Kijana wa Kingazija.
Aliishi Dar katika 1950s akifanya kazi Dar es Salaam Municipal Council kama Bwana Fedha.
Ana kisa cha kusisimua sana kati yake yeye, Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na TANU na Ali Mwinyi Tambwe katibu wa jumuiya hiyo katika historia ya TANU na safari ya kwanza ya Julius Kambarage Nyerere UNO February 1955.
Akiishi Mtaa wa Tandamti nyumba yake ikiangalia Soko la Kariakoo.
Alikuwa mume wa Bi. Bihuri.
Kwa miaka mingi nimekuwa nikitafuta habari zake na picha yake bila mafanikio.
Rashid Ali Meli ni kati ya watu wasiozidi 20 waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnautoglou Hall mwezi August 1954.
Miongoni wa waliohudhuria mkutano ule walikuwa: Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ali Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.