Rashid Sisso mhamasishaji ''extra ordinaire''

Rashid Sisso mhamasishaji ''extra ordinaire''

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
RASHID SISSO MHAMASISHAJI ''EXTRA ORDINAIRE''

Mmoja kati ya wazalendo vijana walioanzisha Bantu Group alikuwa Rashid Sisso.
Wakati wa harakati za kudai uhuru alikuja kuwa karibu sana na Nyerere; na Nyerere akambandika jina la utani, ‘’Ofisa.’’

Katika mikutano ya hadhara Sisso alikuwa akisimama nyuma kabisa ya Nyerere kama mpambe wake.
Nyerere alipotaka kusisitiza nukta fulani katika hotuba yake alikuwa akinyamaza kusema kwa muda na kumgeukia Sisso.

Kisha atamuuliza Sisso, ‘’Je siyo hivyo ofisa?’’
Jibu la Sisso lilikuwa kupiga ukelele katika kipaza sauti.

Wasikilizaji hawakuwa wanaweza kujizuia.
Kwa pamoja walipiga vifijo na kushangilia.

Vibweka hivi vya Nyerere na Sisso vilikuwa havishindwi kuamsha morali za wasikilizaji.

Baadaye Nyerere alipokuja kuwa Waziri Mkuu, Sisso akawa hana tena lolote la maana la kufanya katika TANU.
Baada ya uhuru kupatikana.

Sisso akajigeuza kuwa mchekeshaji, akawa anazubaa kwenye ofisi ya TANU Mtaa wa Lumumba kama kupoteza wakati kuwachekesha watu kwa hadithi zake za enzi ya ukoloni alipokuwa akidai uhuru na Nyerere.

Nyerere alipokuja ofisi ya TANU New Street, kutoka Government House akiwa na msafara wake wa magari na walinzi wake, Sisso alikuwa bila woga akimwendea huku akiwakatiza walinzi hadi alipokuwa Nyerere.

Sisso alikuwa akijihisi vizuri kuonyesha jinsi alivyokuwa anafahamiana na Nyerere.
Baada ya kusalimiana humchekesha na kumkumbusha mambo ya zamani.

Ilikuwa kawaida yake kumwendea Nyerere bila wasiwasi na kupeananae mikono huku akimfanyia dhihaka, walinzi wa karibu wa Nyerere na watu wengine waliokusanyika kuja kumuona Nyerere wakiangalia na kushangaa; huyu mtu gani aliyekuwa akipeana mkono na Nyerere na Nyerere akimsikiliza kwa makini na kucheka?

PICHA:
Kulia ni Rashid Sisso akiwa na Mwalimu Nyerere.

1652206926523.png
 
Alipata kuwa Katika system ya Serikali au aliishia kuwa mchekeshaji tu??
 
Back
Top Bottom