Rashidi Matumla aliyeiletea heshima Tanzania miaka hiyo

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
Na Elius Ndabila[0768239284]

Watanzania wengi ukizungumza jina la Rashidi Matumla si geni vinywani mwao hata machoni kwani ni moja ya watanzania wachache waliolitangaza Taifa hili kwa medani ya ngumi. Matumla ambaye historia ya ngumi inamuonyesha alianza kupigana mwaka 1978 chini ya uangalizi wa baba yake alifikia hatua ya kuwa bondia wa 20 bora duniani. Matumla amewahi kushinda mapambano ya ubingwa wa dunia ya WBU, UBO na baadhi ya mikanda ya Afrika .

Pamoja na Rashidi Matumla kuwa na historia kubwa katika Taifa hili, lakini maisha ya MATUMLA ya sasa yanahitaji msaada mkubwa ili kumrudisha Matumla kwenye historia yake au kwenye darasa la kupika akina Matumla wengine. Kisa cha Matumla kinaanzia hapa;-

Matumla anasema mwaka 2005 alienda Afrika Kusini kwenye mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya ngumi. Anasema akiwa huko na Mwalimu wake kuna chuma alichokuwa akifanyia mazoezi alikosea kukiinua juu, kitu kilichopelekea kupata maumivu ya mgongo. Anasema baada ya kupata tatizo hilo alifikiri ni tatizo la kawaida na angeweza kupona kwa muda mfupi. Yaani hakulitilia maanani sana, hivyokuendelea na kaziyake ya ngumi.

Matumla anaendelea kusimulia mkasa wake kwa kusema, alianza kushangaa kadiri miaka ilivyokuwa ikienda maumivu ya mgongo yakawa yanaongezeka na kibaya zaidi hata machoyake yakawa na shida. Anasema ilifikia mahali hata kama kuna kitu kimoja yeye anaona kama kuna vitu vitatu. Anasem hii ilimpa sana shida na ikamfanya aachane kabisa na mashindano ya ngumi kwani maumivu ya mgongo ni makali. Anaendelea kuwa kwa sasa haoni raha ya dunia.

Masimulizi ya ndugu Matumla ambayo yamejaa huzuni na simanzi, yanatutaka Watanzania wazalendo na wenye moyo wa dhati na tuliokuwa mashabiki wake hasa wapenzi wa soka kumsaidia.

Matumla anasema kwamba baada ya kuona hali yake inazidi kuwa dhofu aliamua kumtafuta Mh Jakaya Kikwete Rais wa awamu ya nne kwa kipindi hicho. Anasema juhudi za kumpata Jk zilikuwa ngumu, lakini kama bahati alifanikiwa kukutana na mototo wa Mh Kikwete ambaye alimuomba amfikishie ujumbe huo Baba yake. Anasema baadae Mzee Kikwete alimpigia simu ilikutaka kujua hali yake. Anasema alimusimulia ABCDs zote ndipo JK alipoamua kumuunganisha na Dakitari wake kwa uchunguzi. Anasema baadae mh Rais wa wakati huo Mh Kikwete alisema aende hospitali ili wakamfanyie vipimo vyote. ANASEMA Matumla

Matumla anaendelea kwa kusema baada ya kwenda hospitali alipatiwa vipimo kwa gharama ya shilingi laki nane ambazo Mh Jk alizitoa. Anasema baaa ya vipimo hivyo kutokana na hali aliyokuwa nayo alishauriwa na dakitari kuwa aende Mhimbilikupata matibabu. Anasema alirudi nyumbani ili akajipange kwa safari ya kwenda Mhimbili. Anasema kwa kuwa tiyari alikuwa yupo kwenye mdororo wa kiuchumi alitegemea kupata fedha toka kwa Mh Rais, lakini kwa bahati mbaya akawa amepoteza mawasiliano yake hivyo ikawa ngumu kumpata Mh JK[Rais kwa kipindi hicho]. Anasema baada ya kukosa mawasiliano alianza kutafuta msaada kwa wadau wengine lakini hakufanikiwa.

‘’eee Bwana ee, utu ni fedha. Bila fedha Dunia hii wewe ni takataka. Marafiki nao wanakuja ukiwa na fedha, kama huna fedha unakuwa ni wewe na taabu zako. Hivi unajua hata mke wangu wa ndoa niliyezaa naye watoto watatu alinikimbia na kuolewa kwingine baada ya kuugua? Niliamini fedha inaongeza udugu, lakini umasikini ni upanga wa kuharibu udugu’’

Rashidi Matumla anasema ili kuhakikisha anaokoa hai wake na kulea watoto wake ameshajaribu kuwatafuta baadhi ya viongozi wa serikali ambao aliamini wangeweza kumsaidia kupata matibabu ameshindwa. Anasema amejaribu kwenda kwa Rc wa DSM ili kutoa kilio chake amekuwa hafanikiwi kumfikia kila anapoenda. Anasema pia ameenda mara kadha kumuona Mh Mwakyembe lakini ameshindwa pia kumuona. Anasema Rais wa chama cha ngumi anajua kuwa sasa anaumwa na anahitaji msaada lakini hawajaweza kumsaidia.

Ni bora nikasaidiwa sasa kupata msaada nikatibiwa nikaendelea kulea wanangu. Hivi nikifa hizo rambi rambi zitanisaidia nini? Nikiumwa nikalala kitandani siwezi hata kuamka hizo pole na fedha zitasaidia nini? Ukinisaidia leo nikipona na mimi nitaendelea kulitumikia Taifa kwa njia nyingine. Sasa umarufu wangu ulikwisha. Hata watu wasiojua kuwa ninaumwa wakiniona kwenye dalala wananyosheana vidole kuwa huyu kafuata nini? Hawajui sasa mimi si Matumla wa miaka ile, ni Matumla ambaye wakati mwingine hata ukinywa chai unamshujuru Mungu., Anasema Matumla.

Matumla anasema anaomba kilio chake kimfikia Mh Rais wa Tanzania DKT John Magufuli, mzalendo wa kweli wa Taifa hili na watanzania wengine wazalendo ili aweze kupata matibabu. Anasema akipona ataendelea kuwafundisha Watanzania wengine ngumi ili kuendelea kuitangaza Tanzania katika medani ya kimataifa.

Matumla anawaasa wanandondi wengine na michezo mingine kuwa na nidhamu ya fedha wanapokuwa wanazipata. Anasema yeye sasa anaweza kuwa mwalimu. Anasisitiz kuwa umaarufu walionao na marafiki walionao ni kwa sababuya fedha, lakini bila fedha marafiki wote watawakimbia. Anatolea mfano kwake kuwa, yeye enzi zake alikuwa akipigiwa simu nyingi za ndugu, jamaa na marafiki, lakini siku hizi ni watu wachache wanampigia na wengine hata akiwapigia huwa hawapokei simu zake. Anawashauri wengine wajifunze kwake kwa kuwa na nidhamu ya maisha kwani siku ya kuanguka kwao hawaijui kama yeye ambavyo alikuwa hajui.

Matumla anaomba msaada kwa Mtanzania yeyote ili aweze kutibiwa. Namba yake ya simu ni 0672219223.
 
Inasikitisha na inatoa funzo kwamba kijana ukipata pesa kuwa na mipango yambele, pia habari ingekuwa na mkazo zaidi kama kungekuwa na picha yake.
 
Pole sana kwa brother Matumla. Watu maarufu(wasanii, wanasiasa etc) wajifunze. Unapokuwa juu muda fulani jifunze kuwekeza hata kile kidogo unachopata, na pia tuwe na heshima kwa kila mtu regardless status. Masuperstar wengi wana dharau na majivuno huku account zao zina mil 5, kesho na kesho kutwa yakiwapata wanalalamika kutengwa.

Get well soon, I hope utasaidiwa soon.
 
Daaaa umeandika andiko la kusikitisha. Mungu amuvushe salama, nitampigia. Unaitendea haki akili yako. Siku hizi unaandika mambo makubwa.
 
Huo mchezo nadhani hawalipwi chochote baada ya kutwangana, yule wa Morogoro alisema amejenga nyumba kwa kuuza chupa za plastiki alizo kusanya mtaani.
Mwingine alipigwa hadi kifo kikamkuta kisa nauli ya Bodaboda...
Ikitokea mzee Magu kanipigia simu, nikaongea nae, hadi kifo kinikute, si maneno au namba yake nitakacho kisahau... Sauti ya Rais masikioni mwangu?!!!!
Pole sana Matumla
 
Rashid aliibeba sana Tanzania kwenye ndondi...natumaini viongozi wataona andiko hili na kumsaidia ipasavyo.

Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi kwa mitihani upitiayo Matumla.
 
Inasikitisha na inatoa funzo kwamba kijana ukipata pesa kuwa na mipango yambele, pia habari ingekuwa na mkazo zaidi kama kungekuwa na picha yake.
Hii imemaliza kabisa. Umeongea ukweli japo najua kuna watakao kupinga lakini ukweli ndio huo. Huwa watu wengi tukipata pesa tunasahau kuna kesho baada ya leo.

Mwenyezi Mungu ampe wepesi bondia wetu mpendwa apate kupona
 
Duuuh pole sana mkurugenzi "nidhamu ya fedha kwa kua haujui anguko lako"
ni rahisi kulaumu lakini ukifuatilia utaona nyotanyota promota huwa wanafaidika zaidi .niliskia hivi karibuni kuwa siku za nyuma bondia anaweza kwenda pigana nje ya nchi akalipwa dola 1000 huku promota akitia kibindoni karibu dola 8000 ama zaidi na hakurusha hata kwenzi kazi za sanaa na michezo ni ngumu sana Tanzania ,ukiwa nje unaona tofauti kuna mtu anayo historia ya malipo ya mapambano ya Matumla alilipwaje? Dula Mbabe juzi kashinda lakini akihojiwa kiasi alicholipwa na radio clouds mmoja wa wahuska wa ndondi akasema hiyo ni siri na moja ya sharti la mkataba ni kutotamka hadharani lakini tunajua floyd au furry atacholipwa hata kabla ya pambano ...asaidiwe tu michezo tanzania ni ridhaa bado
 
Pole zake blaza matumla, ili mwandishi kuna sehemu kaandika soka badala ya ndondi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…