Rasilimali Mkakati Katika Miradi (Strategic Resources)

The Consult

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
220
Reaction score
252

Biashara/kampuni zote huwa zina ufanisi (Competency) na rasilimali (Resources) za kipekee ambazo huzitofautisha na washindani wake. Hizi fanisi na rasilimali katika kampuni hutambuliwa katika hali ya umadhubuti na udhaifu wa kampuni (Organization's Strength and Weakness) Umadhubuti (Strengths) huendana na Fursa (Opportunities) wakati udhaifu wa kampuni (Weakness) huendana na vikwazo (limitations). Umadhubuti na Udhaifu wa kampuni hutokea na kutambulika katika kila nyanja ya uongozi, kwa mfano ngazi ya juu ya uongozi (Senior Management) mara nyingi huwa na taswira ya fursa na vikwazo (External Environments) wakati ngazi ya kati ya uongozi katika kampuni huwa na taswira ya umadhubuti na udhaifu wa kampuni (Internal Environments)

Katika mazingira ya kibiashara, kila kampuni/taasisi ina umadhubuti wake na udahifu wake, HAKUNA kampuni /taasisi yenye uwezo wa kufanya vizuri katika kila nyanja. Kwa mfano; makampuni ya vinywaji baridi, Coca Cola na Pepsi yamejiimarisha/ ni madhubuti katika masoko na matangazo (Marketing and Advertisement), kwa maana nyingine tunaweza kusema kwamba "Marketing & Advertisement" ndio maeneo ya haya makampuni kujidai. Kimsingi makampuni makubwa huwa yana umadhubuti wa hali ya juu (Strengths) lakini huakisi mabadiliko ya kimazingira polepole, wakati kampuni ndogo huwa na uhaba wa umadhubuti (Limited Strengths) lakini huakisi mabadiliko ya kimazingira kwa haraka zaidi.

Rasilimali Shikika (Tangible Resources)

Katika usimamizi wa miradi, umadhubuti na udhaifu wa kampuni/Taasisi hupimwa kupitia umiliki wa rasilimali shikika. Rasilimali hizi hujumuisha
  • Vifaa/vitendea kazi (Facilities & Equipments)
  • Rasilimali watu (Man power)
  • Rasilimali fedha (Money)
  • Rasilimali taarifa na teknoljia (Information and Technology)
Rasilimali zisizo shikika (Intangible Resources)

Hizi ni aina za rasilimali ambazo hupimwa pia kupitia umadhubuti na udhaifu wa kampuni/taasisi, rasilimali hizi hujumuisha;

  • Mila na tamaduni za taasisi (Organization's Culture)
  • Mahusiano na wateja
  • Heshima/hadhi (Reputation)
  • Uwepo katika fikra za wateja/Nembo (Brand name)
  • Hakimiliki
  • Uwajibikaji katika jamii (Social Responsibility)
Kama nilivyoainisha hapo juu, hakuna kampuni duniani yenye kufanya vizuri kila nyanja, hivyo basi, ili kampuni/taasisi kuwa mshindani katika soko (Competitive) haina budi kuchagua rasimali baadhi na kujiimarisha kwazo, ambapo kwa kujiimarisha huko kutaipatia kampuni husika faida ya kiushindani (Competitve Advantage)

Ahsante

Karibu kwa huduma za;
  • Uandishi wa miradi na mipango mkakati (Project Proposals & Strategic Plans)
  • Utoaji wa mafunzo (Trainings/Workshops) katika Usimamizi wa Miradi na Mipango Mkakati (Project Management & Strategic Management)
The Consult; +255 719 518 367
Dar es Salaam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…