Rasimu imesahau Haki ya Huduma Bora za Afya

Rasimu imesahau Haki ya Huduma Bora za Afya

Pax

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Posts
268
Reaction score
87
Wakuu kwanza niipongeze tume kwa kuja na hii rasimu maana tumepata pa kuanzia sasa. Wajumbe wa tume ni wanadamu kwa hiyo mapungufu yanaweza kuwepo japo naamini bado kuna nafasi za marekebisho.

Ime nishangaza kidogo namna ambavyo haki ya kupata elimu imepewa nguvu lakini haki ya kupata huduma bora za afya imesahaulika. Kwenye sehemu ya Kwanza haki za binadamu, kifungu cha 23 inasomeka "Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kutoka katika Serikali na jamii kwa mujibu wa sheria". Mara nyingi wengi hutafsiri hii kama haki ya huduma za afya pia. Nilitamani ingeandikwa vizuri kabisa kuwa "Kila mtu anayo haki ya kupata huduma bora za afya kutoka kwa serikali na jamii kwa ujumla". Halafu kuwe na vijipengele kuifafanua kidogo. Hii ni haki ya msingi sana kwa raia kuweza kuzipata au kuzifurahia haki nyingine zote. Kama mwananchi hana afya, moja kwa moja uwezo wake kuzipata haki nyingine kama elimu, sheria n.k. Ni jukumu la serikali kufanya kila linalowezekana kuhakikisha raia wake wanapata huduma za afya, kama vile wanavyotakiwa kupata haki ya elimu na vitu vingine.

Ama hicho kifungu cha 23 kingefafanua kuwa haki za kuishi ni zipi, ambapo ingeweza kuandika haki ya huduma bora za afya kama mojawapo ya haki hizo. Ni muhimu jambohili likaingizwa kwenye katiba kwa uwazi kabisa.
 
Back
Top Bottom