KUHUSU KURA YA MAONI na muchakato mzima wa kupata katiba mpya inayokubalika
Nimepata wazo jipya, badala ya kusema tunapigia kura rasimu ya katiba inayopendekezwa, kura ya ndiyo au hapana, Afadhali kuwekwe rasimu ya katiba inayopendekezwa ishindanishe au ipigiwe kura na rasimu ya katiba ya warioba. Hii itatupa wananchi fursa ya kuchagua tunachokitaka badala ya kutuwekea hii moja. Upande moja kuna inayopendekezwa upande mwingine, kuwepo na giza? Ni kama chaguzi zilizokuwa zikiendeshwa enzi za mwalimu Nyerere kila walipokwenda kumpigia kura, huku hakuwa na mshindani.
Kwa kuwa katiba inayopendekezwa inayo makundi mawili yanayoshindana: ya wale wa HAPANA, na wale wa NDIYO, mchakato huu ikiachwa ukiendelea kama ilivyo kwa sasa, itakuwa vigumu kupata katiba inayokubalika. Suala la katiba si suala la nani mwenye nguvu. Suala la katiba ni makubaliano ya kila moja jinsi wanavyotaka kutawaliwa au kuongozwa.
Kwa kuwa tayari yapo makundi mawili yanayopingana, naona kuwa tunaelekea kuunda katiba mbili katika Taifa moja. Hata hivyo, tunaelekea kuwa na katiba 3 kwani Zanzibara wanayo katiba yao, na huku Tanzania bara, tunataka kuwa na katiba mbili tofauti.
Kwa watakao kuwa na kura ya HAPANA, Je watakubali kutawaliwa na katiba wasiokubali AU serikali itatumia nguvu kuwalazimisha walioikata?
Nashauri kwa kura ya maoni kuwa nzuri, heri tusema kuwa: siku ya kupiga kura ya maoni, kuwepo katiba inayopendekezwa na upande wa pili kuwepo na rasimu ya katiba ya warioba. Wananchi waamue wanataka ipi. Nafikiri hii tamaliza matatizo.