Rasimu ya II ya katiba yashindwa kutoa tiba ya kansa inayotafuna nchi yetu

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
ndugu watanzania ni nafasi iliyoje kwetu sisi kupata nafasi ya kuandaa katiba mpya. Hapa katika jambo hili ndipo tulitakiwa kuwekeza nguvu zetu zote ili kupata sheria mama inayotuelekeza kutatua matatizo yetu. Katika hili tulitakiwa kujitafakari tulikotoka tumekuwa na matatizo gani na haya matatizo tuliyokumbana nayo ndio wakati wa kuyatafutia ufumbuzi. Nchi yetu hapa tulipo tunayo matatizo mengi lakini ni vema tuangalie tatizo la msingi ni nini. Tatizo kubwa la msingi ambalo linatafuna nchi yetu na litaendelea kulitafuna ni kutokuwepo kwa MFUMO WA KUSIMAMIANA NA KUWAJIBISHANA. Watanzania wote wanaelewa hili kwani nimesikia watu wengi wakisema tatizo la nchi yetu sheria zipo nzuri ila tuna tatizo la kusimamia sheria. hili tatizo ni tatizo la kimfumo ambalo mtu mmoja mmoja hakuna anayeweza kulitatua bali nafasi kama hii ya kutunga katiba ndio operesheni ya kuondoa kansa hii. tulikotoka hivi ni mara ngapi tumesikia wabunge wakilalamika kuwa serikali inakaidi maagizo mengi ya bunge na bunge halina cha kufanya bali kujiona kazi yao ni kulalamika tu. Tutegemee nini katika utendaji wa serikali kama chombo kinachotakiwa kuwasimamia na kuwashauri hakina meno ya kuwang'akia, bado baada ya kuwanyima meno ya kung'ata wasimamizi tuliua muhimili wa mahakama kutoka katika mihimili mikuu mitatu ya kuongoza nchi kwa kuufanya muhimili huu wa mahakama taasisi ya serikali. kwa utaratibu wetu wa watendaji wakuu wa mahakama kuteuliwa na serikali hii imeifanya mahakama si muhimili sambamba na serikali na bunge bali kama taasisi ndani ya serikali. unategemea nini kwa watendaji wa serikali waliopewa dhamana kusimamia rasilimali za taifa kama msimamizi wao ambaye ni bunge ni chombo cha porojo tu hakina la kufanya, mahakama ambayo ambayo ingetazama nani kakiuka taratibu ni mshirika wao kwa maana wanaona ni kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere. Huko nyuma tulifanya makosa makubwa zaidi pia kwa kuweka vichaka vya wahuni katika mifumo yetu. Vichaka hivi ni pale tulipoweka nafasi za uteuzi kwa raisi za kuteua watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya umma. kama si vichaka vya wahuni mashirika yetu ya umma na taasisi ziko wapi leo hii? wengi tulipiga kelele tangu mwanzo kuwa tatizo letu ni mfumo sijui tuliongea mfumo tukijua tunachokisema au tulinukuu tu. inasikitisha kuona sijui ni upeo wetu wa kuona mambo au tunafanya makusudi kwani tunaandika insha ambazo hatuzitafakari na kuziwekea mifumo ya kuhakikisha zinatekelezwa. tulisema tatizo la Tanzania ni mfumo sasa ni wapi tumeelezwa mfumo uliokuwepo una tatizo gani na rasimu inatatuaje tatizo hilo. ni jambo la kusikitisha kuona ibara ya saba ya sita inatamka kuwa wananchi ndio msingi wa mamlaka yote sasa tujiulize ukisoma rasimu ya katiba je imejielekeza katika msemo huu au imetengeneza mfumo ambao madaraka ya wananchi yanaporwa wakishafanya uchaguzi basi raisi ndio anakuwa kila kitu. tunasema nchi ina mihimili mikuu mitatu lakini ili kurejesha mamlaka kwa wananchi lazima tuweke bayana kuwa katika mihimili mitatu ya uongozi wa nchi kila muhimili uwe huru tuondoe mfumo wa kudumbukiza mhimili mmoja ndani ya mwingine lakini lazima tuwe na mhimili uliojuu ya mingine na huo ndio uwajibike kwa wananchi. Kimsingi Bunge ndio mhimili unaotakiwa kuwa juu ya mihimili yote kwani huu ndio uwakilishi wa wananchi na wananchi ndio wenye mamlaka yote na bunge ndio linawajibika kwa wananchi. lakini bunge lipewe meno na hapa mimi naona takukuru ingewekwa taasisi iliyo huru inayowajibika kwa bunge na inapambana na maovu. mahakama tutafute mfumo mzuri wa kupata jaji mkuu na majaji wa mahakama kuu na sio kuteuliwa na raisi na wakabaki kulindana na watendaji wa serikali. tunataka mahakma iwe huru kutoa maamuzi hata kama ni raisi amevunja katiba anafikishwa mahakami. inawezekana zipo nchi zilizoendelea ambako raisi anateua watu kama hawa lakini wanafanya kazi yao ni kutokana na kuwa wao walitengeneza mfumo unaomlazimisha mtu afuate haki bali sisi katika mazingira yetu tunayoyajua mfumo kama huu hauwezi kufanya kazi. hivi tujiulize mashirika ya umma kwa nini yanakufa? sijui sisi tuna matatizo gani maana hatuchambui mambo yanayofanyika katika jamii yetu. katika shirika mtendaji mkuu anateliwa na raisi lakini shirika liko katika wizara hivyo linawajibika kwa wizara na pia tumeunda bodi ambayo nayo kutona na mfumo huu haina nguvu kabisa za kusimamia utendaji wa shirika. kinachotokea ni kuwa kwa kuweka nafasi nyingi za kuteua watendaji wa mashirika basi wahuni, wavivu, mafisadi na wengine wengi wanaunda vikundi vya kuelekea ikuru. hawa wanaoitwa wapambe wanaanza kufanya kazi ya kumnadi huyu mtu wao akipata basi wanagawiwa nafasi hizi za uteuzi. wanakabidhiwa nyadhifa wahuni ambao kazi yao ni kusimama kwenye majukwaa na kutukana wenzao na kuendesha propaganda lakini kiutendaji hakuna kitu wanajua kufanya ziara na kusaini documents tu huku tukiwaita watunga sera. wizara zinashindwa kuwasimamia hawa watu katika mashirika kutokana na kuwa wengi hawateuliwi kwa uwezo wao bali kwa kambi zao, bodi zinawekwa haziwezi kuwasimamia zinabaki kuchukua posho tu na bodi zinaundwa si kwa uwezo. hatuna tija na mfumo huu katika taifa tena hili ni bomu ambalo linaweza kulipuka siku moja na kutuvuruga kwani hawa wapambe ndio wanaofadhili vurugu pale mwenzao waliyemtegemea anaposhindwa. kichaka kimojawapo ni ibara ya 73 (2) hivi kwa mfumo huu tumepata tija wapi? kwa nini tusiunde mfumo wa kusimamiana kwa raisi kuteua waziri na waziri kuteua bodi ya kusimamia shirika na bodi iendeshe mchakato wa ushindani kutafuta mtendaji mkuu na pale shirika linapokuwa halipigi hatua wa kwanza kuhoji ni bodi kwa kumhoji mtu wao waliyemuajiri na wakishindwa waziri yeye anawajibisha bodi na waziri akishindwa anawajibishwa na raisi na raisi akishindwa anawajibishwa na bunge na bunge likishindwa inarudi kwa wananchi lakini bunge likiwa na chombo kama takukuru kama kuna harufu ya uozo katika shirika si kusubiri kumuwajibisha raisi basi takukuru inaenda kupekua hao panya waliokufa na kuoza. mazingira tuliyomo ni vigumu sana kupiga hatua za kimaendeleo na raisi mzuri wa kwanza Tanzania wa kutufanya tupige tambo kama za china hasa kiuchumi ni yule atakayetuwekea mfumo wa kuwajibika, tunayonafasi watanzania sasa ya kutengeneza mfumo wa kulazimisha utawala wa nchi unafanya matakwa ya wananchi. rasimu inamfanya raisi ndio kila kitu ni vema tukafanya mfumo ndio kila kitu, makosa yalifanyika kwa mwasisi wa nchi yetu hakututengenezea mfumo akawa anasimamia kila kitu mwenyewena baada ya kutoka tukatumbukia katika mikono ya wachumia matumbo. hii ni nafasi yetu sote kwa pamoja kuondoa ubabaishaji katika kuendesha taifa letu. kwa kuweka mfumo mathubuti tutalinda amani, tutajenga uchumi, tutatetea haki kwa wanyonge na faida nyingi ambazo mwisho wake ni ustawi wa taifa letu
 
kwa kifupi hatuna mfumo wa utawala unaoeleweka kwa kuona mihimili mitatu ya juu yaani bunge, serikali na mahakama kila muhimili ukitimiza wajibu wake huku kila mhimili ukitumika ipasavyo kusimamia ustawi wa wananchi na kuelekea chini tuone mtiririko wa madaraka unaofanya kila mmoja kuwajibika. bali tumetengeneza mfumo wa kukonfuse watendaji na mwisho wa siku mnashindwa kujua nani amsimamie nani nani awajibike wakati gani. matokeo yake ni uzembe na ufisadi
 
Yawezekana unayo hoja mkuu ila thread yako is not reader friendly, you know why?
 
Nadhani tatizo ni ushahidi au neno IKITHIBITIKA. Naungana na wewe kwa hilo tumeshindwa.
 
Mimi m sina muda wa kusoma habati kama hii. Ndefu tena hakuna hata sehemu ya kurukia? siwezi kusema hata ngoja niangalie pointi aya y
a 3 au 4 au 7. Soma mwenyewe.
 
Mkuu umekuja kulialia hapa? Tafuta forum za kuwakilisha hoja tukingali na fursa
 
Back
Top Bottom