Rasimu ya katiba iboreshwe kwa kuingiza baraza la vijana la taifa

Rasimu ya katiba iboreshwe kwa kuingiza baraza la vijana la taifa

BAVICHA Taifa

Senior Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
117
Reaction score
661
Baraza la Vijana wa CHADEMA limejipanga kutumia wabunge wa CHADEMA, Vyama vingine vya upinzania, wajumbe wasio na vyama na wale wote wenye mapenzi mema na taifa ili kuhakikisha Ibara ya 44 ya rasimu ya katiba mpya inaboreshwa kwa kuingizwa Kipengeke maalumu cha kuanzisha Baraza la Vijana la Taifa kwa ajili ya kuunganisha na kuratibu masuala muhimu ya vijana nchini ikiwa ni pamoja na kusimamia upatikanaji wa haki inayotajwa kwenye Ibara hiyo ya rasimu ya Katiba Mpya.

BAVICHA inaamini kuwa suala la uwepo wa Baraza la Vijana sasa liwe la kikatiba ili kuondoa dhana kuwa chombo hiki ni zawadi ya serikli kwa vijana ambapo mtoa zawadi anaweza kuitoa pale anapoona inafaa.

Tofauti na dai la Baraza la Vijana la Taifa, BAVICHA inataka sasa Katiba itamke mtoto ni nani kwa maana ya umri ilikuepukana na sheria za hovyo zinazokanganyana kuhusiana na masuala ya watoto nchini. BAVICHA imeshauri kuwa, kwa kuwa kama taifa tunakubaliana na dhana kwamba kijana ni mtu mwenye mri wa miaka 18 -35 basi ni muhimu katiba ikatamka bayana kuwa mtoto ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mtu wa umri wa miaka 0-17.

Kadhalika, BAVICHA imewataka wajumbe wa Katiba kuangalia kwa umakini kipengele kinachompa mtu wa miaka kuanzi 18 -20 na kuendelea kuendelea haki ya kupiga kura kumchagua kiongozi anayemtaka lakini mtu huyo huyo ananyimwa haki ya kugombea. Ni muhimu kuzingatia kuwa kama tunaamini mtu wa miaka 18 hadi 20 ana uwezo wa kumsikiliza mtu, akachambua sera zake na hatimaye akafanya uamuzi wa kumchagua kuwa kiongozi wake basi tuamini kuwa busara hizo hizo zinaweza kutumika kuongoza madhali wapiga kura wameamua kwambu mtu huyo na awe kiongozi wao.

BAVICHA inaendelea kuchambua masuala muhimu hususani yahususyo vijana na Taifa kwa ujumla na kuwasiliana moja kwa moja na wajumbe wa bunge maalumu la katiba ili kuhakikisha masuala hayo yanakuwa sehemu ya katiba hivyo basi , kwa kutumia jukwa hili tunawataka vijana na watu wote kuichambua rasimu na kutoa maoni yao ambayo yatawasilishwa moja kwa moja kwa wajumbe walioko Dodoma ili kuwasaidia kutenda kazi yao vizuri ya kuboresha rasimu hiyo.
 
Naunga mkono hoja kwa kua hili ni jambo muhimu kwa vijana.

Go BAVICHA!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom