JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Haki za watu wenye ulemavu: 45.-(1) Mtu mwenye ulemavu anastahiki, kuheshimiwa, kutambuliwa na kutendewa kwa namna ambayo haishushi utu wake
Kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika shughuli za kijamii, kuwekewa miundombinu na mazingira yatakayowezesha kwenda anapotaka, kutumia vyombo vya usafiri na kupata habari
Kutumia lugha za alama, maandishi ya nukta nundu, maandishi yaliyokuzwaau njia nyingine zinazofaa
Kusoma, kujifunzana kuchanganyika na watu wengine na kupata ajira na kugombea nafasi za uongozi katika nyadhifa mbalimbali kwa usawa
Aidha, ibara ndogo ya 2 inasema: Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha watu wenye ulemavu kushiriki katika nafasi za uwakilishi.
Upvote
2