Rasimu ya katiba inasemaje juu ya wajibu wa wazazi kwa watoto wanaowaleta humu duniani?

Joyce Kiria

Member
Joined
Aug 6, 2013
Posts
50
Reaction score
109

Hawa watoto wapo Pugu, baba yao ameondoka yapata mwezi na zaidi, hawajui alipo. kwa mujibu wa hawa watoto baba yao aliwaachia unga wa ugali na tsh 5000 tu. ni vigumu kusema amekimbia watoto kwa sababu hakuna mwenye uhakika na hilo. japo maswali ni mengi ukiwasikiliza hawa watoto.

Rasimu itoe Wajibu kwa wazazi, baadhi ya wababa wanakwepa majukumu ya kulea watoto wao.

Kwenye Rasimu kuna kipengele kinachowabana wazazi hasa BABA kuhusu Wajibu wa Kulea watoto wanaowazaa??? ukiacha hili tukio la hawa watoto ambao hatujui baba yao kapatwa na nini, kuna baadhi ya wakinababa wamekuwa na hulka ya kupenda kuzaa na kukimbia majukumu ya kulea watoto, tena hii tabia inakithiri kila kukicha...KUONA VIDEO YA HAO WATOTO INGIA Joyce Kiria | Wanawake Live™
 
Nilitazama kipindi chako chenye hawa watoto, so sad! Joyce nikupongeze kwa namna unavyoguswa na mambo haya, kuhusu rasimu ya katiba nadhani ina kipengele cha haki za watoto, ingawa sio specifically kuwabana wababa wanaotelekeza familia.
 
Yeah_inasikitisha sana kuona watoto wadogo hivyo wakijilea wenyewe,...anyway_inawezekana hata mzazi wao kauwawa na watu wenye roho mbaya...so sad.
 
Je mama yao nae hayupo?hawana ndugu mwingine wa karibu kuwaangalia?inauma sana
 
Kama baba watoto ni marioo, hatimizi wajibu wake, anachanwa tuu
P
 
Hawa wanaozaa na kutoweka kuskojulikana wapo weng ,,,inauma sana ila mungu atawapa rizik kila moja kwa wakat wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…