Rasimu ya Katiba Mpya: Chadema Ukonga Kukusanya Maoni ya Wananchi Kesho

Rasimu ya Katiba Mpya: Chadema Ukonga Kukusanya Maoni ya Wananchi Kesho

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2008
Posts
10,565
Reaction score
7,984
Salaam Wadau wa JF.

Kama mnavyofahamu kuwa Viongozi wakuu wa Chadema wamesambaa mikoani wakichukua maoni ya wananchi juu ya rasimu ya katiba mpya.

Uongozi wa Chadema jimbo la Ukonga wameandaa mikutano miwili hapo kesho jumapili kwa lengo la kupata/kukusanya maoni ya wananchi wa Ukonga kuhusu rasimu ya katiba mpya.

Mkutano wa kwanza utakuwa ni mkutano wa ndani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo utakaoanza asubuhi saa 3:00 hadi saa 7:00 mchana.

Baadae mchana kuanzia saa 8:00 kutakuwa na mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Kampala uliopo Gongolamboto.

Wadau wote mnakaribishwa kujumuika nasi ili tushiriki kikamilifu katika kutengeneza katiba bora kwa kizazi chetu na vizazi vijavyo!
 
Kweli katiba mpya ilikuwa ni sera ya chadema, maana wamejipanga vizuri!
 
Ccm walidandia treni ya katiba mpya ambayo kwenye ilani yao ya uchaguzi ya 2010 hawakuigusia kabisa na pale walipoitaja ni kwa namna ya kuipinga. Sasa wanafanya jitihada za kuichakachua ili waturudishie katiba ya zamani katika cover mpya!
 
Ccm walidandia treni ya katiba mpya ambayo kwenye ilani yao ya uchaguzi ya 2010 hawakuigusia kabisa na pale walipoitaja ni kwa namna ya kuipinga. Sasa wanafanya jitihada za kuichakachua ili waturudishie katiba ya zamani katika cover mpya!

Mkuu kila la kheri kwenye mkutano wenu huko maeneo ya Kitunda na Nyantira kuelekea Mwanaghati! Naona vyama mnaanza kuteka mchakato wa katiba mkiwagawana wananchi. Mimi nimeamua kujisakia tonge mimi na wanangu hiyo Katiba wacheni ije tu manake naona kuna dalili za wananchi kuyumbishwa. Huku kuna CCM huku CDM na CUF nao wamo.Achilia mbal akina Mzee Waryoba ambao wametuletea Rasimu na badala ya kacha watu wajadili na kuwapa feedback wao wanataka wananchi waseme ambacho Tume inaona ni sahihi. Vyama navyo vinataka ya kwao na bado akina civil society nao watake ya kwao.

Mkuu miongoni mwa wapigania Katiba Mpya hata kabla ya 2005 ni mtu mmoja anaitwa Leo Lwekamwa ambaye alisigina Katiba ya Mwaka 1977 pale jangwani kwenye mkutano wa hadhara kuonyesha kutoridhika na Katiba ya sasa
 
Back
Top Bottom