RASIMU YA KATIBA MPYA; Haya ndio mapungufu, tuyaainishe

RASIMU YA KATIBA MPYA; Haya ndio mapungufu, tuyaainishe

Wimana

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
2,449
Reaction score
718
Wadau, Rasimu ya Katiba mpya ndio imetoka. Binafsi sijaipata ila nimefuatilia kwenye vyombo mbali mbali vya habari na pamoja na kazi nzuri waliyofanya kina Warioba lakini bado kuna mapungufu makubwa. Najua wengi hatuna Jukwaa linguine la kubainisha hayo mapungufu maana sio wote tuliogombea na kuchaguliwa kuingia kwenye MKatiba Mabarza ya Katiba ambayo ndio yamepewa majukumu ya kuipitia Rasimu hiyo na kushauri. UPUNGUFU niliobaini ni kuhusu kuwa na Serikali ya Zanziba, Serikali ya Tanganyika (Tanzania Bara) na Serikali Kuu ya Shirikisho. KUWA Serikali zinazounda Shirikisho zina Mamlaka ya kuanzisha Vikosi vya Usalama (Ukiondoa Jeshi la Ulinzi). NAjiliza, ufanyaji kazi wa vikosi hya hivyo utakuwaje pindi Mhalifu akikimbilia upande mwingine wa Shirikisho? Polisi wa Tanganyika wataweza kumkamata Jambazi aliyekimbilia Zanzibar? (Maana Polisi hawa Watawajibika kwa Serikali zao nje ya serikali ya Shirikisho).
 
Hilo halina shida mana vyombo vya usalama vitashirikiana, pungufu kuu! Tuletewe haraka mjadala wa katiba ya TANGANYIKA b4 2015
 
Back
Top Bottom