Hilo si jina tuu "waziri mkuu". Sala ni anapatikanaje na majumu yake ni nini. sio lazima aitwe hata waziri mkuu. anaweza itwa chief Senetor au Mwagoda wa Tanganyika. Muundo wa sasa una serikali tatu, lakini unafiki umetuzidi.
Unachosema ni kweli.
Hati ya Muungano ina vipengele :
(a) a separate legislature and executive in and for Zanzibar from time to time constituted in accordance with the existing law of Zanzibar and having exclusive authority within Zanzibar for matters other than those reserved to the Parliament and Executive of the united Republic;.......
And the said Parliament and Executive shall have exclusive authority in such matters throughout and for the purposes of the united Republic and in addition exclusive authority in respect of all other matters in and for Tanganyika.(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject-
Muundo wa sasa uko hivi:
Zitakuwepo serikali tatu, Serikali ya mambo ya Tanganyika, serikali ya mambo ya Zanzibar na serikali ya mambo ya Muungano.
Ili kubana matumizi kwa maoni ya Mwalimu, Serikali ya mambo ya Tanganyika itajihifadhi ndani ya Serikali ya Muungano. Hivyo kimwonekano, serikali ya Muungano ni serikali mbili zilizounganishwa pamoja.Kwa lugha ya kisheria,Serikali ya Tanganyika imekasimisha mamlaka yake kwa Serikali ya Muungano. Kwa hiyo Serikali ya muungano ni Serikali iliyojikusanyia mamlaka mbili kwa pamoja. Mamlaka ya mambo ya Muungano na Mamlaka ya mambo ya Tanganyika.
Ipo serikali ya mambo ya Zanzibar inayoitwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mfumo/Muundo huu ndio wanaoulalamikia Zanzibar kwa kusema Tanganyika imejivalisha koti la Muungano.
Serikali mbili zinaonekana na moja iko nyuma ya pazia na mamlaka tatu za kisheria;mamlaka ya mambo ya Tanganyika(Tz bara),mamlaka ya mambo ya Muungano na mamlaka ya mambo ya Zanzibar.
"
Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa nigharama kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangiagharama za kuendesha Serikali ya Shirikisho; na Tanganyika ingefanya vivyo hivyo.Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa Tanganyika ndio hasa ungeendesha SerikaIi yaShirikisho. Kwa hiyo Tanganyika ingeendesha Serikali yake ya watu 12, 000, 000 na piandiyo ingetoa sehemu kubwa ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la watu 1...
Kwa hivyo ilitupasa tujiulize kwa nini tunataka kuibebesha Tanganyikagharama zote hizo; na hasa kwa nini tunataka Serikali ya Tanganyika? Hivituna hofu ya kwamba Tanganyika, bila kuwa na SerikaIi yake, itaoekanakuwa imemezwa na Zanzibar? Hofu yetu ni kwamba tukiwa na SerikaliMoja Tanganyika itaonekana kuwa imeimeza Zanzibar. Basi na tutafutemfumo ambao utaiondolea Zanzibar hofu hii ya kumezwa, bila kuibebesha Tanganyika mzigo wa kuendesha Serikalli mbili zenye uzito unaolingana" uk 10-11
link
Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)