RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

habariyamujini

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Posts
3,094
Reaction score
457
HIVI SASA, Ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na TBC1. mgeni rasmi ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE... KATIBA MPYA KWA TANZANIA YENYE NEEMA

TUFUATILIE

 
Wadau leo ndio rasimu ya katiba mpya Inazinduliwa Karimjee .Uzinduzi huo unatarajiwa kurushwa na vituo vya TBC1, TBC Taifa, ITV, Star TV, Channel Ten, ZBC TV na ZBC, kuanzia sasa.Kila anaeweza na afuatilie.Hata hivyo ni vizuri kila mtu angetoa maoni yake ikiwa ni kitu gani ambacho akiona kimewekwa humo angefurahi sana na ni kitu gani ambacho kikiachwa atasikitika sana.

Nawasilisha!
 
Tusitegemee la maana. Sanasana ni kukamilisha ratiba tu, maana ni kama bora liende!
Kama Tundu Lissu anaundiwa mzengwe wa kumwagwa Bungeni kwaajili ya katiba hii, unategemea kuna jema lolote kwa Mtanzania humo?
Its sadenning, maana nchi zingine kama zinatokea kuwa makini kupita kiasi, basi ni wakati wa kuandaa katiba. Lakini hawa wenzetu issue ni kuangalia maslahi ya makundi katika katiba!
The move is Kill Them Before They Grow!
 
Mimi nitakapoona imepitishwa kwamba mawaziri wasiwe wabunge nitapata faraja kwa kweli.Kwa sasa anaongea Jaji Warioba.
 
Wajumbe wa mabaraza watapata nakala za rasimu ili waisome mapema
 
Nakala ya rasimu ni muhimu ikatangulia kutolewa kwny softcopy wakati mchakato wa kudurufu hardcopy ikiendelea
 
maadili yetu utawala na uongozi yameorodheshwa. tume inapendekeza
1. maadili ya viongozi, miiko na kiundwe chombo cha kusimamia maadili ya uongozi. secretariate ya maadili ibadilishwe iwe tume ya maadili inayo jitegemea. mia

*viti maalum vimeondolewa, wabunge mwisho kugombea miaka 15 na hakutakua na uchaguzi mdogo. spika na naibu spika wasiwe wabunge wala viongozi wa siasa. mia

*viongozi wa kisiasa na asasi za kiraia hawatakua na sifa ya kuwa katika tume ya uchaguzi. mia

*serikali ya shirikisho, serikali ya tanzania bara na serikali ya tanzania visiwani. mia
 
Katiba ya haki na usawa yenye kujali maisha ya mtanzania wa hali ya chini, uwajibikaji, na isiyo ya mrengo wa kisiasa .
 
Endelea kutujuza,tume imependekeza umri wa urais uleule 40
 
Wangefanya mpango hilo zoezi la uzinduzi likaenda sambamba na kuiweka kwenye website ya tume ili kuwezesha watu kuipitia kwa urahisi
 
Mgombea binafsi ruksa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mgombea binafsi kwa nafasi zozote anaruhusiwa ana nafasi hiyo... Warioba
 
Kura zaidi ya 50% ndio kushinda urais

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hoja ya mtikila imepita mgombea binafsi,rais apate kura 50%
 
Matokeo ya raisi yanaruhusiwa kuhojiwa baada ya kutangazwa , aliye mgombea anaruhusiwa kupeleka malalamiko yapelekwe mahakamani ndani ya 30 siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…