RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Wana jamii

katika mapendekezo ya Rasimu ya Katiba mpya limo suara la raisi kuteua majaji. Sote tumeshuhudia jinsi majaji vihiyo walivyokuwa wanateuriwa na rais pamoja na kwamba kuna tume ya mahakakama inayomshauri Rais katika teuzi za majaji. Kama majaji watendelea kuteuriwa na rais basi tutaendelea kushuhudi muhimili huu ukiendelea kudhibitiwa ipasavyo na mhimili mwingine yaani Selikali kama ilivyo sasa. tukatae pendekezo hili ikiwezekana tuchukue utaratibu wa kuwapata majaji katika katiba ya majirani zetu wakenya.
 
Duh! Acha niwahi jimboni kwangu nianze kutafuta perfect match. Mgombea mwenza wa ubunge. It sounds good. Kama kuna vyama 20 wagombea watakuwa 40. Safi.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
mm naona hapo kwenye kinga ya raisi iondolewe,maana hao wabunge uwezo wa kumshitaki haupo maana ni wanachama wake.
 
Mkuu nadhani hilo ndilo litakalotokea. Tutegemee kuwapata akina Filikunjombe kibao Bungeni kuanzia sasa. Watu sasa watajitoa kwenye utumwa wa vyama watakuwa watumwa wa wananchi. Tume imeenda mbali zaidi na kuruhusu kuwafuta wabunge kazi kabla ya uchaguzi basi hapa utegemee wabunge kujituma kwa wananchi wao aliowachagua
 

mkuu raia fulani hapo kwenye red. isije ikawa ni haki za maliberali!
 

Ni bora hii tume ya mahakama ipewe meno ya kuwahoji wanaotaka kuwa majaji na kupendekeza kwa Rais. Hapa kunatakiwa kuwe na uwazi kama ilivyo kwa Kenya na si kufanya mapendekezo kimya kimya. Kumbuka sakata la Zanzibar.
 

Mkuu itapendeza ukatowa mapendekezo tuwapate kwa mfumo upi?
 

Marekebisho yatafanywa kupitia mabaraza ya katiba na bunge la katiba. Lakini mi ninawasiwasi kwa nini madaraka ya rais hayapunguzwi? Eti kila jimbo kuwe na wagombea wawili -ke na -me,sisi tunataka wabunge wapunguzwe wao wanazid kuwaongeza si bora hata wangesema kila nch iamue aina ya wabunge kwenye katiba zao kuliko huu upuuzi. Wametumia garama kuuubwa rasmu yenyewe ya kawaida tu,si bora hata wangeteuliwa watu kadhaa tu wakaanda rasmu kuliko hizo garama zote walizotumia na mambo waliyoleta ni ya kawaida tu,anyway wamejaribu na hii ndo Tanzania!
 
Lakini kuna ukweli usiopingika kuwa mikoa na wilaya zetu zimewekewa mipaka kikabila. Hata hii mipya iliyotengwa siku za karibuni! Nani anabisha?
 
Kwa nini Tanganyika mnaing'ang'ania zanzibar wakati zanzibar inataka mamlaka yake kamili si uonevu huuu?
 
Hii rasimu hapo kwenye hii mihimili ya dola kujitegemea bado haija paweka vizuri...hasa hapo kwenye mahakama...kwenye bunge pako fresh...
 

wamekopi katiba ya kenya!this is absurd.hata G7,nchi tajiri sana duniani hawana mfumo huu.
 
Ni bora hii tume ya mahakama ipewe meno ya kuwahoji wanaotaka kuwa majaji na kupendekeza kwa Rais. Hapa kunatakiwa kuwe na uwazi kama ilivyo kwa Kenya na si kufanya mapendekezo kimya kimya. Kumbuka sakata la Zanzibar.

Raisi kwakuwa ndiye mkuu wa mhimili mmoja wa dola-serikali haruhusiwi hata kidogo kuweka mkono wake katika kuteua ama kuchagua watumishi wa mhimili mwingine wa dola-mahakama.

Raisi abaki kudeal na serikali yake na tume ya utumishi wa mahakama ndiyo ifanye kazi ya kuajiri majaji ikiwa ni pamoja na Jaji Mkuu na Naibu wake.
 
Haki za akina Mdee na Mbatia

Tume ya warioba wamejitahidi kwa kweli.Madaraka ya raisi ndiyo hawajaliweka vizuri.Rais anatakiwa kuwapendekeza mawaziri/majaji baada ya hapo kuwe na tume huru itakayo wafanyia mchujo (vetting) na baada ya hapo majina ya watakaofaulu yapelekwe bungeni kuwa approved na kurudishwa kwa raisi kwa ajili ya kuwatangaza. Hili la kusema raisi awateue na baada ya hapo wapitishwe na bunge naona bado halijakaa vizuri kwani wabunge wa chama anachotokea rais wanaweza kuwa ni wengi na wakawapitisha hata wale ambao hawafai.
 
Mkuu itapendeza ukatowa mapendekezo tuwapate kwa mfumo upi?

Nafasi za kazi zitangazwe na kisha wenye sifa waombe. Kisha kamati maalumya majaji iwafanyie usaili bila kuingiliwa na mamlaka yo yote.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Si Kikwete aliwambia Dodoma muianzishe lakini muiendeshe wenyewe na nyie mmekomalia iingie kwenye katiba?
Hakuna aliyekataza katiba kuwepo, shida ni kwamba mnataka wale wanaodaiwa kuibeba bakwata iwabebe!
 
HATUTAKI Rais kuteua MAJAJI, Jaji aajiliwe kama Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…