RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

MMh mimi ninavyo kutazama katika ulichokiandika nikwamba wewe rasimu yenyewe hujaielewa na possibly wewe ni slow learner....Anyway hii rasimu inaelezea wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano na sio Tanganyika wala Zanzibar
 
Mabunge ni mangapi jamani? Je bunge la tanganyika lipo?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Hili linatekelezeka lakini linahitaji commitment vinginevyo mamabo yaweza kuwa magumu zaidi ya sasa nasema hivyo kwa kuangalia aina ya utawala tulionao sasa.
Tusipokuwa makini huu unaweza kuwa mwanya wa wajanja kupata njia ya kuibia hela kwa sababu kutakuwepo na migawanyo mingi ya mapato kwa serikali zote tatu.
Pia tujiandae kwa mchakato mya wa katiba ya Tanganyika maana hii ni ya Jamhuri ya muungano.
 
Nina wasiwasi na HAKI ZA MAKUNDI MADOGO KATIKA JAMII.makundi gani hayo? .waliberali watakitumia sana hiki kipengele.
 

Hivi mkuu jaribu kuchunguza post yako! ulivyoileta kwa mtu wa kawaida inakuwa na hitimisho! ya kuwa serikali itakuwa hivyo. Mimi naona labda hayo uliyonijibu ungeyaunganisha kwenye post yako hapo juu ungelieleweka vizuri.
 
Ni lini wananchi walikuwa na mzigo mwepesi? Zanzibar, bon voyage and God bless you


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Sidhani kama itakua busara hili linipite bila kutia neno...mwanga mpya na matumaini yanataka kuonekana, Nimeikubali hii rasimu...
 
Mkuu acha kuwapotosha watu! tulia soma vizuri rasimu! hao 15 ni wa shirikisho tu, bado wa Tanganyika! upo hapo?

Mimi nina mawazo tofauti. Hivi ni lazima kuungana? Walishindwa wasenegali na wagambia. Kila upande ubaki kuwa ni nchi na mamlaka yake kama ilivyokuwa kabla ya 1964. Hapo tutapunguza gharama za uendeshaji. Tunaweza kuungana kwenye East Afrika.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Sio kweli Kuwa serikari Tatu ni nafuu ebu toa mfano wa taifa changa lenye serikari tatu lenye maendeleo? ZNZ akiongoza Gavana na Huku Tanganyika akaongoza Gavana mmoja tu huku Rais Akiwa mmoja anayekaa Dodoma Hakuna gharama unakuwa muungano nafuu kuliko Nchi masikini Kuwa na Marais Watatu.
 
Tanzania ni Taifa changa Kuwa na Marais watatu ni mizigo kwa walipa kodi Kama imeshindikana mbinu zote ni bora ifanyike kampeni ya kuwaunganisha watanzania wote Bara na visiwani ikibidi kura ya maoni tuungane tuwe Taifa moja Rais mmoja tu tuepuke hizi Gharama za kuendesha serikari nyingi wakati uwezo wa kituleta pamoja upo
 
Nope, ujue kuna watu wanachangia katiba mpya wakati hata ya zamani hawaijui?

Siamini kama waweza changia kwa ufasaha bila kuijua ile ya zamani

Zipo Rasimu mbili?
 
Reactions: EMT
Kimsingi Watanzania wanaaminishwa kuwa wakitua mizigo miwili iliyowashinda wataweza kubeba mitatu mikubwa zaidi. Mkiwa na serikali tatu ya Tanganyika itakuwa na nguvu zaidi huku wengine wanaeza kuona Zanzibar itakuwa na nguvu zaidi!
 
Natafuta copy ya rasimu ya katiba mpya. mdau yoyote anayejua nnapoweza kuipata please tujuzane
 
Watu wengi hawajui kwanin muungano ulikuwapo? Hatupendi kujiuliza hilo badala yake tunakimbilia ama kuuvunja au kuuimarisha pasipo kujua chanzo cha uwepo wake. Hata watawala wetu wanapata kigugumiza kusema kam tulilazimishwa na mabepari.hil n tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…