Watanzania wakati umefika ni lazima tuondokane na mawazo mgando ya serikali mbili, ambazo utekelezaji wake ni mgumu sana kwa nyakati zetu hizi. Lazima tuambatane na fikra mpya na chanya za kuwa na taasisi zilizojengewa misingi ya kikatiba ya uwajibikaji. Demokrasia inayosemwa, sasa inatakiwa iingie kwenye matendo, kuliko kubaki nadharia tuu.
Mfumo huo mpya wa dola utapunguza sana gharama za uendeshaji wa Serikali na Bunge la Muungano kwa kiasi kikubwa, hivyo kuwapunguzia wananchi mzigo. Mfumo huo mpya wa serikali tatu ni cheaper(una gharama nafuu) kuliko mfumo wa sasa, kwasababu:
1.Mfumo mpya una mawaziri wachache(15) kuliko wa sasa(56).
2.Mfumo mpya una wabunge wachache(75) kuliko wa sasa(375).
3.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye wizara husika kuliko wa sasa.
4.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye ofisi za bunge kuliko wa sasa.
5.Mfumo mpya utakuwa na uwajibikaji mkubwa kuliko wa sasa, ambao mamilioni ya pesa za walipa kodi yanapotea.
6.Mfumo mpya hauna ofisi ya wazili Mkuu, hivyo gharama zote zilizopo sasa za kuiendesha ofisi ya PM na makandokando yake hazitakuwepo.
Hivyo basi, mfumo mpya wa dola unapunguza kwa kiasi kikubwa gahrama za uendeshaji wa dola.
Huu mfumo mpya ni mzuri na unaotekelezeka kirahisi, bila kuhitaji gharama kubwa. Mfumo huo upo Ujerumani,Marekani, Afrika kusini, Uingereza, India Nk
Mfumo huu mpya utatoa ajira nyingi kwa vijana wetu wasomi, kwasababu upatikanaji wa fursa za kazi hautakuwa unatawaliwa na mfumo wa kikilitimba, miungu watu, na kupendeleana kama ulivyo sasa. Kwani kwa sasa kupata kazi lazima uwe ulizaliwa ktk familia ya mwanasiasa fulani au unafahimia na mtu fulani maarufu, au utoe rushwa.
Naipongeza tume kwa kufanya kazi kisayansi.