Rasimu ya katiba mpya

Rasimu ya katiba mpya

kiroba

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
324
Reaction score
114
Habari wana JF
Poleni sana kwa majukumu ya ujenzi wa taifa letu. Kama watanzania hatuna budi kuchukua japo hata mida wetu mchache kupitia na kuelekeza wasiojua mambo ya katiba. Ningeshauri kwa wana jamvi kuwa tuwe tunaipitia na kuijadili rasimu ya katiba hapa jamvini. Kuliko kuandika mambo ambayo hayana tija kwa taifa zaidi ya kulumbana kiitikadi kwa mambo yasio na msingi.

Nimeamua kutoa ushauri wangu kwa kuwa najua katika jukwaa hili kuna wasomi wengi wenye kujua mambo ya sheria. Tuweke hapa michango yetu ili tuweze hata kuwaalika wanasiasa ili nao watoe michango yao kwa kuwa naamini wapo wengi tu humu JF.

Ningependa tuipitie hii rasimu sura hadi sura na pia ibara hadi ibara. Vile vile tuipitie kila kifungu ili tujadili kwa hoja na sio kukosoa tu na unaanza kutoa lugha za mizaha. Tuache ushabiki na dhihaka katika jambo hili nyeti kwa taifa letu. Haya tuanze kama ifuatavyo

SURA YA KWANZA
Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Sehemu ya kwanza
Mipaka, Alama, Lugha, Utamaduni, na Tunu za Taifa.
 
Back
Top Bottom