MWESIGWA ZAIDI
Member
- Mar 7, 2015
- 21
- 1
UCHAMBUZI KUHUSU MUUNDO WA MUUNGANO KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA (RASIMU YA TUME YA WARIOBA IMEBORESHWA NA HAIKUCHAKACHULIWA)
MAKALA NO. 5
Muundo wa muungano unaopendekezwa umeainishwa katika sura ya saba ya katika inayopendekezwa iliyoandikwa na bunge maalum la katiba. Ibara ya 73 ya katiba inayopendekezwa inasema kwamba jamhuri ya muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa serikali mbili ambazo ni Serikali ya jamhuri ya muungano, na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Hata hivyo ifahamike kwamba muundo uliokuwa umependekezwa wa muungano na tume ya mabadiliko ya katiba ulikuwa wa shirikisho wa serikali tatu mapendekezo yaliyopo katika ibara ya 60 ya rasimu ya katiba iliyopendekezwa na tume ya mabadiliko yakatiba ila siyo kwamba niwanachi wote waliopendekeza muundo wa serikali tatu, pia wapo waliopendekeza muundo wa serikali mbili ila kwa sababu na maoni ya tume ilipendelea muundo wa shirikisho la serikali tatu pia tume ikatoa sababu za mapendekezo hayo uk.47-48 wa randama ya rasimu iliyopendekezwa miongoni mwayo ikiwa nikwamba muundo huo ungeondoa mgonano wa mamlaka kama ilivyo katika muundo wa serikali mbili zilizopo sasa ndani ya katiba ya 1977 kimsingi hapa tume ilikuwa inapendekeza ziwepo dola/mamlaka tatu zenye mamlaka kamili nakwamba muundo huo ungeondoa hofu ya Zanzibar kumezwa na Tanganyika.
Hapa tume ilisahau au inawezekana ilijielekeza vibaya kufahamu kwamba Hakuna mamlaka wala serikali ndani ya muundo wa muungano wasasa inayoitwa Tanganyika kwa mujibu wa sheria No.61ya mwaka 1964 iliyobadili jina la Tanganyika na kuwa Tanzania.
Katika ibara ya 74 ya katiba inayopendekezwa inahusu utekelezaji wa shughuli za mamlaka ya nchi hapa inamaana kwamba jamhuri ya muungano wa tanzania ni nchi moja isipokuwa mamlaka ya utendaji ya nchi yatasimamiwa na vyombo viwili ambavyo ni serikali ya jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hivyo ni muungano wenye serikali mbili zenye mamlaka ya kiutendaji kwa mujibu wa ibara ya 75 ya katiba inayopendekezwa.
Pia katika ibara ya 74 ya katiba inayopendekezwa vimetajwa vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji kuwa nivyombo viwili vyenye mamlaka ya utoaji haki na pia vyombo viwilivyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma, vyombo hivyo ni mahakama ya jamhuri ya muungano pamoja pamoja na mahakama na kuu ya Zanzibar vikiwa ni vyombo vyenye mamlaka ya utoaji haki na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la wawakilishi. Hapa mantiki ya bunge ni bunge la jamhuri ya muungano na mantiki ya baraza la wawakilishi ni baraza la wawakilishi la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Katika ibara ya 74(3) mswada wa katiba umeainisha wazi kwamba kutakuwa na mambo ya muungano na mambo yasiyo ya muungano. Ibara ya 74(4) imeweka wazi kwamba kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitakuwa na majukumu yake na kwa kufuata mashariti ya katiba hii. Hapa mambo muhimu ya kuzingatia katika ibara hii ni nikwamba, katiba imevipa vyombo vya utekelezaji wa shughuli za umma mamlaka yasiyogongana kiutendaji.
Pia serikali zote mbili kila moja ina mamlaka ya kushughulikia mambo yake yasiyo ya muungano bila kuihusisha serikali nyingine kwa mujibu wa ibara ya 74 kila serikali ina muundo na mfumo kamili wa mihimili mitatu ambayo hakuna muhimili unaoingilia muhimili mwingine kwenye serikali nyingine.
Katika ibara ya 76(1) katiba inaainisha mamlaka ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya muungano na katika ibara ndogo ya 2 nikwamba serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha uhusiano au ushirikiano na jumuia au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa na ifahamike kwamba mamlaka ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar yaliyotajwa katika ibara ndogo ya 1 ni mamlaka huru inaweza kuyatekeleza bila kushirikisha serikali ya jamhuri ya muungano, hivyo hoja yakwamba Tanganyika imejivisha koti la muungano inapoteza mashiko ya kisheria labda kwa kufikirika tu kwa kuwa ibara ya 74 ya katiba inayopendekezwa ina ainisha wazi kwamba jamhuri ya muungano inamuundo wa serikali mbili ambazo ni serikali ya jamhuri ya muungano pamoja na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Nivema watanzania mkafahamu kwamba muungano unaotajwa na katiba hii inayopendekezwa katika sura ya saba na ndani ya ibara ya 74 katika vifungu vidogo vya (a) na (b) umejengwa katika misingi ya kisheria toka mwanzo kama ifuatavyo. Mnamo tarehe 25 April 1964 bunge la Tanganyika lilipitisha kile kinachoitwa ( articles of union) kati ya Zanzibar na Tanganyika kwa sheria No.22/1964 na kwa upande wa Zanzibar muungano uliridhiwa na baraza la wawakilishi pale ilipotengenezwa the union of Zanzibar and Tanganyika law of 1964 ambapo sheria hizi mbili kwa pamoja ziliitwa (Acts of union) ambapo tarehe 26 April 1964 muungano ulipita na kutambulika kisheria zilizoutengeneza nakwa pamoja nchi hizi mbili zikaanza kuitwa jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika mwaka huo huo wa 1964 mwezi December the united republic (Declaration of name) Act No. 61 of 1964 ilipitishwa na jina la jamhuri ya muungano wa wa Tanzania lilianza kutumika rasimi kuanzia tarehe 29[SUP]th[/SUP] October 1964 yaani the law was made retrospectively. Kilifanyika kile kinachoitwa cessation of name. Pia ushahidi wa namna hii unapatikana katika kitabu cha Nyerere freedom and unity Uk. 291 kwahiyo hamna Tanganyika iliyojivisha koti la muungano kwa kuwa haipo kisheria vilevile siyo jambo la ajabu nchi kubadili jina au kukasimu mamlaka yake kwa serikali nyingine nijambo linalo ruhusiwa na sheria za kimataifa. ( International Laws), kwa sasa tuna jamhuri ya muungano wa Tanzania nasiyo Tanganyika pia hakuna Tanganyika iliyojificha ila haipo.
Fikra za wanaosema Tanganyika ipo zisiangalie eneo la jiografia ya Tanganyika ilipokuwa isipokuwa fikra zao ziangalie usahihi wa kisheria wa jina Tanganyika kutokuwepo tena ila ardhi iliyokuwa ya Tanganyika kwasasa ndiyo ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kuitaka Tanganyika sasa nisawa nisawa nakumtaka mtu aliyekwishafariki arudi kuwa hai bila shaka nijambo lisilowezekana na likiwezekana hatokuwa mtu wa kawaida kwa mujibu wa maumbile yakawaida ya binaadamu. Napenda kusisitiza kwamba serikali ya jamhuri ya muungano haina mamlaka ya kiutendaji dhidi ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya muunago isipokuwa ina mamlaka ya utekelezaji katika jamhuri ya muungano na kwa yote yasiyo ya muungano yanayohusu Tanzania bara, hii nikwa mujibu wa ibara ya 75 ya katiba inayopendekezwa.
Hivyo wananchi wote wa Zanzibar pamoja na Tanzania bara wasihofu hii katiba kwa kulaghaiwa na baadhi ya wanasiasa kwamba muundo huu wa muungano hauna manufaa kwao, siyo kweli kabisa hao wana ajenda yao ya siri nayo ni kuwagawa watanzania ili warahisishe kututawala kirahisi na kwa manufaa yao baada ya kuona kwamba nguvu yao ya ushawishi kwa wananchi ni ndogo mno kuwawezesha kupata madaraka sehemu zote mbili za muungano.
Nasema hivi kwa sababu wanaokataa muundo huu wa serikali mbili hawataki kutueleza faida na hasara za serikali mbili na tatu, wao wamengangania serikali tatu kana kwamba ndizo zitatuletea maendeleo wakati hata katika majimbo yao yanuchaguzi waliyopewa kwa ridhaa ya wananchi yamewashinda kuyaendeleza sasa wameona waibue ajenda ya kuwapa mtaji wasiasa bila kutathimini kwa kina kwamba muundo wa serikali tatu nihatari kwa muungano uliopo sasa na unaopendekezwa katika katiba pendekezwa. Watanzania tufahamu kwamba kuvunja urafiki au udugu na rafiki au ndugu mmoja nichanzo cha kuvunja udugu au urafiki na rafiki mya. Bora mwenye njaa anaweza kutathimini jambo ila siyo mwenye tamaa. Serikali mbili ndiyo muundo sahihi wa kutatua kero za muungano pamoja na migongano yakikatiba kama ilivyo kwa sasa kwa kuwa mgawanyo wake wa mamlaka za utendaji wa shughuli za umma umewekwa vizuri sana ndani ya rasimu inayopendekezwa.
Katika sura ya nane sehemu yakwanza yakatiba inayopendekezwa ndipo unaainishwa muundo wa uongozi wa jamhuri ya muungano ambapo ibara ya 79(1) ina ainisha kwamba kutakuwa na serikali ya jamhuri ya muungano ambayo itaundwa na Rais, makamu wa Rais na baraza la mawaziri. Ibara ya 96 inaweka bayana kwamba kutakuwana makamu wa Raisi watatu ambao watakuwa ni, makamu wakwanza wa Rais, Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa makamu wa pili wa rais( yaani makamu wapili wa rais wa jamhuri ya muungano) na waziri mkuu ambaye atakuwa makamu wa tatu wa rais( yaani makamu watatu wa rais wa jamhuri ya mungano wa Tanzania.
Huu ni muundo mzuri kwa sababu kwanza unapunguza gharama za utendaji kwa kuwa viongozi hawa watakutana katika mambo ya muungano tu siyo kama ule muundo wa serikali tatu unaoongeza mzigo wa gharama kwa wananchi katika muundo huu viongozi wakitaifa nakatika muungano wanabaki kuwa walewale hivyo hata utekelezaji wamajukumu nirahisi pia muundo huu pia muundo huu unawapunguzia viongozi madaraka ndani ya muungano kwa kuwa hata mambo ya muungano yamepunguzwa, itakuwa rahisi kwa kiongozi kushughulikia majukumu ya watu wake kiurahisi mno kwa mfano Rais wa Zanzibar kuwa makamu wapili wa rais kunampunguzia rais wa jamhuri ya muungano mzigo wa kushughulilia maslahi ya wazanzibar ndani ya muungano.
Kwa kuwa tayari mwakilishi wao ndani ya muungano na kwa upande wa waziri mkuu kuwa makamu wa tatu wa rais itasaidia wepesi wakushughulikia maslahi ya Zanzibar pia ya watu wa jamhuri ya muungano ndani ya muungano, kimsingi hawa niwasaidizi wa rais wa jamhuri ya muungano kwa mambo yanayohusu muungano nayale yasiyohusu muungano. Pia ni muundo unaotengeneza chain of command yakiutawala kuliko ambavyo ingekuwa rahisi katika muundo waserikali tatu Kwa rais wa shirikisho kunyimwa ushirikiano na viongozi wa nchi washirika.
Katika muundo wa serikali tatu ile serikali ya shirikisho ipo kwa kuwategemea nchi washirika wakati ndiyo serikali kuu. Bila shaka lazima tatizo litatokea iwapo baba atamtegemea motto mdogo lakini nisahihi motto kumtegemea baba.
Baada ya uchambuzi huu, kama bado watakuwepo wanaodai serikali tatu zenye mamlakakamili ndani ya shirikisho moja nidhahiri kwamba wao ndio wafadhili wa hatari wanaotaka kuwaletea watanzania ili wao wapate upenyo wa madaraka ingawa pia hata kwa muundo waserikali tatu bado urahisi wa kuyapata madaraka bila kuwashawishi wananchi wakakuelewa na kuridhia kukupa kura bado haitawezekana, itabaki kuwa ndoto za kuingia ikulu na ndoto hizo ndizo zinazosababisha kulazimisha yasiyowezekana ili yawezekane.
Kwa maoni yangu muundo wa serikali tatu nihatari kwa usalama, maendeleo na mahusiano ya watanzania nabadala yake muundo sahihi wa muungano ni huu unaopendekezwa katika rasimu yakatiba wa serikali mbili. Nawashauri watanzania tuamue kusuka au kunyoa na kunyoa nikuwa na muundo wa serikali tatu na kusuka nikuwa namuundo wa serikali mbili.
Ikumbukwe kwamba katika kumbukumbu za nyaraka za tume, Tume yenyewe inakiri kwamba muundo wa serikali tatu una changamoto ambazo ilishindwa kuzitolea ufumbuzi na kulitupia mzigo huo bunge maalum la katiba na bunge maalum lakatiba liliziona changamoto hizo ndiyo maana likaja na pendekezo la serikali mbili ambazo kwa kiasi kikubwa sana bunge maalim la katiba limeweza kuweka mfumo mzuri katika katiba inayopendekezwa wa kutatua changamoto za serikari mbili ambazo zinatatulika ila siyo serikali tatu.
Hata kauli iliyotolewa na mheshimiwa Lisu kwamba sahihi ya Karume ilifojiwa katika hati ya muungano niyakusikitisha naya uongo mtupu kwa sababu hata yeye hakuwahi kuleta sahihi anayoamini niyakweli ili ifanyiwe ulinganifu na iliyopo kwenye hati za muungano.
MWANASHERIA. MWESIGWA ZAIDI SIRAJI. 0784 646220