Wakuu nimekutana na hii video kuhusu CHADEMA kujitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, hii imekaaje wakuu?
Your browser is not able to display this video.
Tunachokijua
Uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji hufanyika kila baada ya miaka minne nchini Tanzania ambapo wananchi hupata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka katika ngazi za mitaa na vijiji, mara ya mwisho uchaguzi ulifanyika mwaka 2019 huku vyama vya upinzani vikisusia uchaguzi huo madai ya kutozingatiwa kwa taratibu za kidemokrasia za kupitisha wagombea wakati wa uchaguzi huo.
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 kwa matokeo ya jumla kwa nchi nzima, Chama cha Mapinduzi kilishinda nafasi za uongozi kwa Vijiji 12,260 sawa na asilimia 99.9, Mitaa 4263 sawa na asilimia 100 vitongoji 63,970 sawa na Asilimia 99.4 na hivyo kusababisha asilimia kubwa ya nafasi za uongozi katika ngazi hiyo kukaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kumekuwepo na video inayosambaa mtandaoni imuonesha Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akitangaza CHADEMA kujitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji huku video hiyo ikiwa na tarehe 21 oktoba 2024.
Je ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia njia ya utafutaji wa kimtandao umebaini kuwa video hiyo ni ya kweli lakini uhalisia wake unapotoshwa kwani Freeman Mbowe alitangaza uamuzi wa CHADEMA kujitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji wa 2019 siku ya Alhamisi 07, mwezi Novemba 2019 ambapo ndio wakati video hiyo ilirekodiwa na kuchapishwa mtandaoni kwa mara ya kwanza.
Aidha JamiiCheck imepitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za MillardAyo ambapo imebaini kutokuwepo kwa video hiyo inayoonesha kuchapishwa tarehe 21 oktoba 2024 tofauti na ile iliyochapishwaa Novemba 07, 2019.
Hivyo video hiyo haina uhusiano wowote na uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2024 na hakuna chama chochote cha siasa mpaka sasa ambacho kimetangaza kujitoa katika uchaguzi huo.
CCM wana usengerema mwingi sana, habari ya 2019 wanasema ni ya mwaka huu. Video inaeleza Chadema kujiotoa baada ya wagombea wao kuenguliwa, wakati kwa uchaguzi huu hata form bado wagombea hawajachukua , hata mtu ukitaka kudanganya basi jitahidi huo uongo ufanane na ukweli.