Rasmi: Donald Ngoma ametua Azam Fc

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Timu ya soka ya Azam FC imeingia makubaliano ya usajili kwa mkataba wa mwaka mmoja na mshambuliaji Donald Ngoma kwa ajili ya msimu ujao wa 2018/2019

- Ngoma alijiunga na Yanga mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili akitokea nchini Zimbabwe




=======

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuthibitisha kuwa umeingia makubaliano ya usajili kwa mkataba wa mwaka mmoja na mshambuliaji Donald Ngoma, kwa ajili ya msimu ujao 2018/2019.

Baada ya kuingia makubaliano hayo, muda wowote kuanzia sasa Azam FC inatarajia kumpeleka mchezaji huyo katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya afya ili kuona ni kwa kiasi gani majeraha yaliyokuwa yakimsumbua yamepona.

Azam FC inaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo kutoka nchini Zimbabwe aliyewahi kuchezea FC Platinum ya huko kabla ya kuhamia Yanga, ni sehemu tu ya mikakati ya benchi la ufundi na uongozi katika kuboresha kikosi kwenye eneo la ushambuliaji kuelekea msimu ujao.

Aidha kama mambo yataenda vizuri, uongozi wa Azam FC unaamini kuwa Ngoma atakuwa ni miongoni mwa nyota wapya wa timu hiyo watakaoonekana kwenye Kombe la Kagame (CECAFA Kagame Cup) linalotarajia kuanza hivi karibuni tukiwa kama mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Tayari mchezaji huyo ameandaliwa jezi namba 11 iliyokuwa ikitumiwa na mshambuliaji Yahaya Mohammed, aliyerejea Aduana Stars ya nchini kwao Ghana.

Tunawaomba mashabiki wetu wa Azam FC wawe watulivu katika kipindi hiki na kuendelea kuisapoti timu, kwani uongozi umejipanga kufanyia kazi ripoti ya benchi ya ufundi na kuboresha kikosi ili kusaka taji la ubingwa msimu ujao.

CHANZO: Azam FC
 
Waende tuu maana pale jangwani njaa imetawala
Viongozi wa kibongo hawana ubunifu kabisa kwenye masuala ya pesa.
Ombi, Dr Tiboroha anafaa sana kuwa Katibu mkuu pale jangwani.
 
Dah, mwaka nzima kalamba mshahara bila kucheza. Apate ushauri kwa Niyonzima.
 
Jamaa ni Injury prone kama alivyo Kapombe....Yanga wanaakili sana kumuacha.
 
Alikuwa na mgomo baridi huyu..!
Bado Chirwa nae kuondoka,ni suala la muda tu.
Mgomo unaotokana na nini hasa? Malipo yake au?

Na viongozi wamechangiaje kwenye hili kama asemavyo sibonike?
 
Yaonyesha alikuwa akiumwa mshahara kutoka kwa[emoji196][emoji196] Lakini hakutenda vema, wamemuuguza hivyo walau angewachezea msimu mmoja
 
Hatuwezi kubeza uwezo wa Ngoma, alitusaidia sana misimu iliopita sema nadhani ni mtu anayejali maslahi yake kwanza. Anyway azam wamelamba dume kama jamaa akipona 100% akawa fit. Pluijm nae dah, watatisha sana. Sitoshangaa kusikia ajibu nae kaenda azam, penye njaa hakuna uvumilivu
 
Alishakuwa liability badala ya asset
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…