Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,403
- 12,775
Chuo Kikuu cha Laikipia kilichopo mjini Eldoret nchini Kenya, kimemtunuku Mwanariadha bingwa wa dunia wa mbio ndefu Eliud Kipchoge, Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris causa) kutokana na kuipeperusha vema bendera ya Kenya kimataifa kupitia riadha.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Joseph Kibet Rotich amesema uamuzi huo ulifikiwa na Baraza la taaluma la chuo hicho (University senate) kwa mujibu wa hati ya chuo hicho (University Charter) Sehemu ya 3, Kifungu cha 21.4(k) ambacho kinatoa mamlaka kwa Chuo hicho kumtunuku udaktari wa heshima mtu yeyote aliyefanya jambo kubwa lenye mchango chanya katika jamii.