Rasmi kibarua cha Antonio Conte chaota nyasi Tottenham

Rasmi kibarua cha Antonio Conte chaota nyasi Tottenham

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baada ya siku kadhaa za presha na tetesi hatimaye pande mbili baina ya klabu na kocha huyo zimeafikiana kuvunja mkataba na sasa timu itakuwa chini ya uangalizi wa kocha wa muda ambaye ni Cristian Stellini.
Kwa maamuzi hayo Spurs inatafuta kocha wa nne ndani ya miaka miwili.

Kabla ya maamuzi hayo Conte hakuwa na uhusiano mzuri na wachezaji na uongozi wa klabu kutoka na kuwashutumu wachezaji wake akidai hawajitumi na kuelezea sababu kadhaa kwa nini timu haitwai mataji.

---------

Antonio Conte FINALLY leaves Tottenham by 'mutual consent' after his extraordinary rant, with Cristian Stellini put in temporary charge as Spurs begin search for a fourth manager in just two years

Tottenham head coach Antonio Conte's departure has finally been confirmed as his turbulent 16 month reign ended.

Daniel Levy was preparing to sack the Italian following his now infamous verbal attack against his own players following the 3-3 draw at Southampton.

And his exit was confirmed just before 10.30pm on Sunday night, though his exit was described as 'mutual' in a club statement.

Conte's No 2 Cristian Stellini will assume the role as acting head coach while Ryan Mason will take on the position as his assistant.

The Italian was due to return to the club's training ground on Tuesday as players start returning from international duty.
 
Conte kawapa makavu live. Hii sio timu, ni wachezaji 11 wanaoingia uwanjani kucheza, hawana ushirikiano, ni wabinafsi. Conte alinukuliwa akisema baada ya sare ya 3-3 soton. Lets go to the problem, kuna mmiliki wa timu ambaye amekaa kwa miaka 20 bila kupata chochote.

Je, shida ni makocha wanaopita hapa au shida ni nini? Aliendelea kuwapiga spana. Levy akashindwa kuvumilia ukweli unao uma akampiga mbele.
 
Chizi huyo Konte...mwaka Jana kamaliza nafasi ya nne Huku Arsenal watano...mwaka huu aitazame Arsenal ilipo...ajilaumu yeye mwenyewe
 
Bado na yule Graham Potter Mandonga wa Chelsea. Ni kocha mzuri kwenye timu ndogo. Kwenye timu kubwa kama Chelsea, naona anambwela mbwela tu.
 
Chizi huyo Konte...mwaka Jana kamaliza nafasi ya nne Huku Arsenal watano...mwaka huu aitazame Arsenal ilipo...ajilaumu yeye mwenyewe
Strong disagree. Mpira hautazamwi hivyo. Kama ndivyo basi liverpool ndio hamna kitu kabisa. Nafasi ya pili kwa 90+ points. Point 1 pungufu kupata ubingwa. Na wamecheza UEFA Champions league fainal dhidi ya Real Madrid. Conte ni mtu anayejitambua na kujiamini. Kumbuka hata alipokuwa inter na chelsea.
 
Utamlaumu mmliki kwa lipi? Unafuatilia mpira kweli wewe?

Mtu wa kulaumiwa Spurs ni pochetino alipewa kila kitu,kwa wakati wake wachezaji walikuwa kwenye pick ya hali ya juu ni upumbavu wake tu alishindwa kuweka kipaumbele kombe lipi la muhimu kwake

Angewekeza Epl kwa asilimia mia moja alikuwa anachukua ubingwa km mara mbili hivi

Wakati pochetino anaondoka wachezaji walishachoka walishafikia pick na kuanza kudrop viwango

Kila kocha aliyejiunga na spurs alipewa fungu la usajili la kutosha! Utamlaumu mmliki kwa lipi?

Mtu anayemlaumu tajiri wa spurs ni tikiti hafuatilii mpira
Conte kawapa makavu live. Hii sio timu, ni wachezaji 11 wanaoingia uwanjani kucheza, hawana ushirikiano, ni wabinafsi. Conte alinukuliwa akisema baada ya sare ya 3-3 soton. Lets go to the problem, kuna mmiliki wa timu ambaye amekaa kwa miaka 20 bila kupata chochote.

Je, shida ni makocha wanaopita hapa au shida ni nini? Aliendelea kuwapiga spana. Levy akashindwa kuvumilia ukweli unao uma akampiga mbele.
 
Inshort Kila timu ina aina yake ya makocha-, ndio maana Kuna timu kubwa ziko makini sana siyo kuchukuachukua tu makocha, conte ni dizaini ya makocha kama kina Mourinho ambao wanafaa kuwa timu kama Chelsea kipindi kile chini ya abrahamovic.

Kuna makocha wakubwa siyo wa Kila timu.
 
pocchetiono alikuwa na wachezaji gani wazuri? Wewe ndio uelewi policy ya Levy. Jamaa ndio anaongoza kwa kuuza wachezaji kwake wazuri tena kwa bei kubwa. Tangu enzi za kina Bebatov mpaka Bale. Hayupo kutafuta vikombe, yupo kwa ajili ya pesa. Hivi unawezaje kuuza mchezaji wa viwango vya Modric afu utegemee kupata vikombe?
 
Kwa kipindi kirefu sana ama hata milele, hawatakaa wapate kocha kama Mauricio Pochettino.
 
Back
Top Bottom