Rasmi: Kupitia kwa Afisa habari wa Simba SC Haji Manara amesema wameachana na kocha msaidizi Mganda Jackson Mayanja

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Kocha msaidizi wa Simba Mganda Jackson Mayanja amekanusha taarifa za kutimuliwa ambazo zinasambaa nchini na kudai kuwa si za kweli kwani hana taarifa yoyote rasmi kutoka kwa uongozi.

Mayanja amesema hajui taarifa hizo zinatoka wapi kwasababu sio za kweli na yeye anaendelea na kazi kama kawaida. “Sijafukuzwa naendelea na kazi yangu kama kawaida”, amesema Mayanja.

Aidha Mayanja amesema hakuwepo nchini kwa siku kadhaa zilizopita kwasababu alisafiri kwenda kwao Uganda ambako alikuwa na mambo ya kifamilia na tayari ameshayamaliza na amerejea kuendelea na kazi.

“Nilienda nyumbani Uganda mara moja kulikuwa na matatizo ya kifamilia sio kwamba nimefukuzwa, ndio mana nimerejea kuendelea na kazi yangu na uongozi wa klabu haujanipa taarifa yoyote, sasa sijui hizo taarifa zimetoka wapi”, ameongeza Mayanja.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba klabu ya Simba inataka kubadili benchi lake la ufundi lakini jana kupitia mkutano na wanahabari, afisa habari wa Simba Haji Manara alikanusha taarifa hizo na kudai kuwa klabu inaendelea na makocha wake Joseph Omog na Jackson Mayanja.
=========================================================================================

UPDATES

Baada ya kukana kuwa hajafukuzwa na kuondolewa na klabu ya Simba SC;

Kupitia kwa Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wameachana na kocha huyo kwa uungwana bila matatizo kwani ana mambo yake binafsi ambayo anahitaji muda zaidi wa kuyashughulikia.

Manara ameweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram wenye maneno haya, “Yes Tumemalizana na kocha Mayanja kiungwana,,,angalia video hyo,,Thanks kocha Jack,,kila la kheri ,,we gonna mic u Sir”.

Mayanja mwenyewe amefunguka kuwa anaishukuru klabu na uongozi mzima kwa muda wote ambao wamefanyakazi pamoja lakini pia kumruhusu akashughulikie matatizo yake nyumbani kwao Uganda.

Tazama video hapa Mayanja akieleza sababu za kuachana na Simba.
 
16 mins ago MICHEZO

Kocha Jackson Mayanja ameamua kuachana na klabu ya Simba nrejea kwao Uganda.

Mayanja ambaye bado yuko jijini Dar es Salaam, ameamua kuachana na Simba akidai ana matatizo yake binafsi.

“Ni matatizo ya kifamilia lakini suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa,” alisema.

Lakini habari kutoka Simba zimeeleza kuwa sasa wako katika hatua za mwisho kuvunja mkataba wake baada ya kukubaliana naye kutokana na uamuzi wake huo.
 
Bado Omog fukuza leta kocha anayejua mpira
 
Ni ngumu sana kama kocha kufanya kazi na viongozi wa simba plus msemaji wao
 
Kwikwi kwiiiiiiiiii
Wanruka na kukanyagana kisa nini Yanga amkaba mtu koo ni mwendo wa kuchezakwa presha tu
Ndugu zetu hawa wana hatariii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…