Rasmi nimeamua kupaki sitatumia tena gari

wiztech

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2020
Posts
259
Reaction score
511
Kutokana na hali ya uchumi mafuta yamepanda bei vilivyo leo nimeamua kujinyima nikaweka mkebe wangu walau lita 10 za kupashia injini tuu kila baada ya siku saba lkn rasmi nimeamua kupaki sitatumia tena gari labda ubber daladala na bodaboda.
 
Tatizo sio mama kwa kuwa bei ilipanda soko la dunia ukichanganya na kodi siijui 15 kwenye mafuta lazima yawe bei juu
Suluhisho la kushusha bei za mafuta ni kujenga kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi pale TANGA
Fursa hiyo ya kuchakata mafuta ya Uganda
Yaani mkuu tz mikoa yote mafuta unafuu wa bei ni mkoa wa tanga tuu
 
Nilikuwa siipendi passo ya wife Sasa tunanyang'anyana funguo
 
Mama Anaupiga Mwingi...hapo bado Hajaingia ndani ya kumi na nane!

Yupo katikati ya Uwanja, tusubiri kibano zaidi Atapoingia ndani Ya 18 golini mwetu.....!

Kutaja machache yanayoonyesha mbungi linapigwa Jingi.....!

Tozo La Uzalendo anakamua bila kulitolea jasho.

Machinga Wanachafua Mji.
Bei ya Wese juu.

Ziraeli Mtoa Roho ana sisi WaTz, Kazi tunayo..!
 
Season bado inaendelea
Sukari-mafuta ya kupikia-tozo kwenye miamala, kulipia kodi kupitia umeme - vifurushi - gesi na sasa mafuta.
Tabu zote hizo na bado umeme na maji ya mgao.
Tutafika ila tumechoka sana. Kidumu chama cha mapinduzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…