JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Bodi ya Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ umethibitishwa rasmi kupitisha mchakato wa Klabu ya Chelsea kuuzwa kwa paundi bilioni 4.25, ambapo mnunuzi ni Bilionea Todd Boehly.
Klabu hiyo iliwekwa sokoni na aliyekuwa mmiliki wake, Roman Abramovich ambaye amewekewa vikwazo kutokana na ukaribu wake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
Kilichobaki baada ya tamko hilo ni mchakato wa Serikali ya Uingereza katika kuhalaliza leseni ya manunuzi, ambapo baada ya hapo utafanyika utaratibu wa mwisho kukamilisha mauzo.
Kwa sasa Chelsea imeruhusiwa kuendelea kujiendesha kwa lesni maalum ya Serikali hadi Mei 31, 2022.
Source: Daily Mail