Cherenganya
JF-Expert Member
- Jan 21, 2018
- 2,309
- 1,785
Habari wanajamvi wenzangu
Ni siku nyingine tena Alhamdulilah ninaendelea kupumua pumzi ya BURE ambayo bila shaka ni wajibu wangu kuitendea haki ili kesho akhera, nipate cha kujitetea mbele ya Muumba wa Mbingu saba.
Asubuhi ya leo nikiwa katika safari yangu kuelekea kule ninapopatia mkate wangu wa kila siku, nikafanikiwa kuisikia taarifa kupitia MAGIC FM katika kipindi chao cha Asubuhi cha Good morning Magic, Taarifa hii ambayo imenifanya kujivunia kuwa mtanzania, ni kwamba imethibitika rasmi sasa kwamba binadamu wa kwanza aliishi Africa na si tu Africa bali Tanzania kwenye Bonde la Oltupai maarufu kwa kimombo kama Oldivai Gorge, Arusha. Ripoti hii imethibishwa na wataalamu wa mambo ya kale.
Ni muda sasa tutembee kifua mbele kwa kuzaliwa katika nchi hii ambayo inasemekana kuwa nchi ya pili kwa vivutio Duniani, miongoni mwa nchi tatu tu duniani zinapopatikana gesi ya HELIUM, nchi pekee inayotoa madini aina ya Tanzanite duniani, nchi mwenyeji wa ndege aina ya Flamingo, nchi pekee yenye chura anayebeba mimba duniani, nchi pekee unaweza ukaendelea...
Nakupenda Tanzania