Rasmi sasa: Kenya yaanza kuuza mafuta nje ya nchi

Rasmi sasa: Kenya yaanza kuuza mafuta nje ya nchi

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya leo amezindua rasmi usafirishaji wa mafuta ghafi ya petroli yaliyochimbwa nchini humo na kwa utaratibu huo nchi hiyo imeanza mkakati wa kuuza bidhaa hiyo katika soko la kimataifa.

Akiwa katika katika eneo la visima vya mafuta huko Lokichar katika kaunti ya Turkana kaskazini mwa Kenya, Rais Kenyatta amezindua safari za malori manne yatakayosafirisha mapipa 600 ya mafuta hadi katika kiwanda cha kusafisha mafuta kilichoko Changamwe katika Kaunti ya Mombasa. Rais Kenyatta amesema usafirishaji huo wa majaribio ni mwanzo wa safari ndefu itakayozaa matunda.

Mafuta hayo yanatazmiwa kuuzwa katika soko la kimataifa na hivyo kuifanya Kenya iwe miongoni mwa nchi zinazouza mafuta ghafi ya petroli duniani. Rais Kenyatta amesema serikali ya Kenya itajitahidi kuzalisha bidhaa zitokanazo na mafuta ghafi ya petroli ili kuimarisha ustawi na uwekezaji wa kigeni. Aidha amesema Serikali inatekeleza mkakati wa uchimbaji wa gesi nchini humo.

Rais wa Kenya amesema wenyeji wa eneo lenye visima vya mafuta katika kaunti ya Turkana watafaidika na utajiri huo hasa kwa ujenzi wa miundo msingi muhimu.

Mapipa 2,000 ya mafuta yanatarjiwa kusafirishwa kwa barabara kila siku kutoka Turkana hadi Mombasa katika masafa yenye umbali wa kilomita 1,000. Serikali ya Kenya ina mpango wa kujenga bomba la mafuta kutoka eneo la Turkana hadi bandari ya Mombasa kabla ya mwaka 2021 ili kuharakisha usafirishaji wa mafuta hayo katika masoko ya kimataifa.

My take: Naiona Kenya ikipaa kwa kasi ya 4g kwa miaka 2 ijayo sisi tunapimana tezi dume. tu
4bpq570f4986af168wj_800C450.jpg
 
Naanza kufukuzia uraia wa kenya
 
Africa tuna mbwembwe sana..waliobahatika kutembea watanielewa Maendeleo mnayoyaona ya majiji ya Africa yamewakilisha asilimia ndogo sana kiukweli ufukara mzito,ujinga na maradhi ndo yametawala. Tunajitahidi kuonesha Dunia tumeweza ila bdo hali ni Ngumu...Ukiacha kwa Madiba na juu ya Jangwa la sahara wengine takwimu za wanaolala na njaa au kupata mlo hafifu wa mwili,akili na hata kiroho ni wengi. Imagine hata mahubiri ya Pastors wengi wa Nje ni Heavy yamejaa content kuliko yetu Fanya utafiti...itaendelea
 
With trucks, transportation of only 2000 barrels per day is possible, n to fill one average tanker of 200,000 barrels will take 100 days i.e. over 3 months! I don't see viability of this kangaroo accomplishment!
 
The main aim of this project is to sell this oil to different clients to process at their own prefered refineries and test the product on their machines.... so that by the the time the pipeline is complete, clients would have already tested the oil and seen that it works well with tgeir budget.... kabla hata tumalize ujenzi wa hio pipeline utakuta kuna nchi kadhaa zitakua zimeshapiga order
 
Na kumbe there are still a lot of tests to be done before shipping starts.... I am glad we started this process in Ernest.
 
Kitakacho msaidia kenyata kufanikisha mambo mengi Ni Kwa sababu mambo ya siasa na uchama kaweka pembeni. Anajaribu Sana kuwaunganisha wakenya wawe pamoja.
Kenyatta akili kubwa huwezi kumlinganisha na ujinga!!
 
With trucks, transportation of only 2000 barrels per day is possible, n to fill one average tanker of 200,000 barrels will take 100 days i.e. over 3 months! I don't see viability of this kangaroo accomplishment!

How many barrels has Tanzania exported?
If you ever happen to discover oil, and with your world renowned laziness, bongolala will be exporting 100 barrels a day.
Kenya has taken 6 years from discovery to export. Very few countries have such turnaround time on their minerals.

By 2020 that 2000 barrels a day will have a few more zeros.

Meanwhile your kangaroo minerals like Tanzanite are bringing peanuts decades after they were discovered.
 
Sisi huku tz tunaogopa kutangaza fedha tunazolipwa ili wanaotudai wasije kusikia wakatushtaki.

Hongereni Kenyans
 
Back
Top Bottom