Rasmi; Simba waondoa sintofahamu, wamalizana na Kagera sugar, sakata la Mhilu

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Baada ya kuwepo sintofahamu kuhusu usajili wa mshambuliaji nyota wa Kitanzania, Yusuf Mhilu hatimaye klabu yake imetoa baraka kwa mchezaji huyo.

Mhilu alitambulishwa Simba Agosti 4 mwaka huu kuwa mchezaji wao huku uongozi wa Kagera ukisema hawajamalizana na mchezaji huyo kwakuwa wana mkataba nae.

Leo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram wameandika; "Tumefikia makubaliano ya pande zote mbili (Kagera Sugar FC na Simba Sc) juu ya uhamisho wa aliyekuwa mchezaji wetu Nyota Yusuph Valentine Mhilu kwa dau la Sh40 milioni.

Wameendelea kuandika; "Mhilu alisaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Kagera Sugar mwaka jana 2020. Hivyo uhamisho huu wa kwenda Simba ni uhamisho ambao umehusisha kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia ndani ya klabu ya Kagera Sugar,"

Mhilu alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Msimbazi walioenda kwenye kambi ya maandalizi ya msimu mpya nchini Morocco
 
BAADA YA KUCHEZA RAFU MKAGUNDUA MMETOA BOKO NDIO MNAJISAFISHA LEO... MIKIA FC WANA TABU SANA
 
Kagera hawana jinsi kwakua Simba ndio Tff na Tff ndio Simba kwaiyo hawakua na jinsi maana ata wakienda kulalamika bado wangemkosa mchezaji na fedha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…