Rasmi ugomvi wa Lady Jay Dee na Clouds umezikwa

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
7,683
Reaction score
15,128
Wakuu kama kichwa kinavyooleza hapo ugomvi wa Komando huyu wa kike kwenye tasnia ya burudani ya Muziki wa Bongo Fleva umezikwa, leo tangu asubuhi bandika bandua ni ngoma tu za Lady Jay Dee zinapigwa kumpa promo kwenye tamasha lake la miaka 20 yake kwenye tasnia.

Hivi ndivyo inavyotakiwa Clouds iwape uwanja sawa wasanii wote bila kubagua tutafika mbali, sifahamu kama amelipia au bure lakini cha msingi promo kama hii ifanyike kwa wasanii wote na kwa vituo vyote itasaidia kukuza mziki.
 
Ile kauli ya "redio yetu tunafanya tutakavyo......" haipo siku hizi.

Wabadilike siku hizi ushindani wa radio umekuwa mkubwa,Jide ana mashabiki wake hata kama ni wachache lkn bado wana umuhimu wake ktk kuongeza idadi ya wasikilizaji.
 
Ni kweli boss miaka 5 nyuma hii redio ilinyoosha watu kwakweli ila kwa sasa haishtui.

Yeah, leo ilikuwa ni bandika bandua nyimbo za Jidee, binafsi nimewapenda bure clouds
 
Clouds ya 2013 kurudi nyuma ndiyo ilikuwa Clouds kwelikweli. Leo inakimbizwa na EFM. Kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha
 
Ni kweli boss miaka 5 nyuma hii redio ilinyoosha watu kwakweli ila kwa sasa haishtui.
Watu walinyooka haswa had watangazaj
Hata kukohoa ilikua shda
 
Ile kauli ya "redio yetu tunafanya tutakavyo......" haipo siku hizi.

Wabadilike siku hizi ushindani wa radio umekuwa mkubwa,Jide ana mashabiki wake hata kama ni wachache lkn bado wana umuhimu wake ktk kuongeza idadi ya wasikilizaji.
Redio ni yao na wanafanya watakavyo ndio..ndo maana leo siku nzima ni Jide tu..ushaona wapi hii tofauti na msiba wa msanii?
 
Nimeona leo sababu moja wanajenga amani ,ila ukweli ushindani wa radio ndio umesababisha haya yote,weakness yako mshindani wako anaitumia kama faida kujijenga kibiashara.
 
True monopoly inapungua kwenye media..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…